Thursday, March 28, 2019

AJENGEWA NYUMBA, WENGINE WASAPOTIWA FEDHA..

Kanisa dogo la mkoani Kilimanjaro lililopatiwa msaada na Nabii Mkuu.

Nyumba mpya anayojengewa Bi. Nawasa ikiwa inaendelea na ujenzi.
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa msaada wa jumla ya sh. 2,300,000 (milioni mbili na laki tatu), kwa watu watatu tofauti huku mwingine akipata neema ya kujengewa nyumba.
Hayo yamejiri wiki hii baada ya Nabii Mkuu kuguswa kuwasaidia watu wawili tofauti mtaji wa sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kila mmoja kwa ajili ya kuwawezesha kupata mtaji wa kuanzisha biashara.
Kwa upande mwingine Mchungaji mmoja wa kanisa dogo mkoani Kilimanjaro (jina lake na la kanisa linahifadhiwa) amebarikiwa sh. 300,000 (laki tatu) mara baada ya Nabii Mkuu kuliona kanisa hilo la mbao (kama linavyoonekana pichani) wakati akipita na msafara wake na kuwakuta katika ibada yao ambapo aliguswa kushuka na kuwasapoti kifedha na kisha kuendelea na safari yake.
Mchungaji huyo pamoja na waumini wake wasiozidi kumi (10) wakizungumza mara baada ya kupokea baraka hiyo ya kifedha walionyesha furaha yao na kutoa shukurani zao za dhati kwa Nabii Mkuu kutokana na msaada huo.
Wakati huohuo mwanamke mmoja muumini wa huduma ya Ngurumo Ya Upako anayefahamika kwa jina la Nawasa Saibulu, amepata neema ya kipekee ya kujengewa nyumba na Nabii Mkuu (kama inavyoonekana pichani ikiwa inaendelea na ujenzi) baada ya nyumba ya awali aliyokuwa akiishi iliyokuwa ya udongo kuharibika na kuwa na tatizo la kuingiza maji kipindi cha mvua.
Mwanamke huyo ni miongoni mwa watu waliopata neema hiyo ya kuboreshewa makazi yao kwa mwaka huu wa 2019.
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali ya kifedha ambapo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2019 ametumia zaidi ya sh. 40,000,000 (milioni arobaini) katika kugusa mahitaji mbalimbali ya watu kutoka sehemu tofauti tofauti duniani.


NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Wednesday, March 27, 2019

WABARIKIWA FEDHA KWAAJILI YA KUKUZA BIASHARA ZAO..



Neema ya kifedha imewatembelea baadhi ya watu waliokuwa na mahitaji ya fedha kwaajili ya kukuza biashara zao pamoja na kulipa madeni, ambapo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie aliwapatia fedha taslimu kwaajili ya kukidhi mahitaji yao.
Ni siku ya jumapili katika Ibada ya jiji, iliyofanyika katika katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako.. Kisongo, Arusha ambapo jumla ya 1,200,000 (milioni moja na laki mbili) ilitolewa nae Nabii Mkuu kwaajili ya kuwa-support kwenye shughuli zao waweze kujikimu kimaisha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watu hao wameelezea ugumu waliokuwa wakiupata kiuchumi na wepesi waliouona mara baada ya kubarikiwa kifedha nae Nabii Mkuu na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanaitendea haki fedha waliyopewa na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie.
Aidha siku ya jumapili katika Ibada ya Chuo Kikuu Cha Manabii ilikuwa ibada ya "Kupatiwa uelekeo mpya na sahihi maishani" ambapo Nabii Mkuu alifanya Huduma ya Unabii wa mtu mmoja mmoja wa kupita katikati ya maelfu ya watu waliofika siku ya jana na kuwahudumia kila mmoja kwa nafasi yake.
Akizungumza Nabii Mkuu alisema kuwa watu wengi wanateseka maishani kwa sababu ya uelekeo mbaya/ usiokuwa sahihi waliokuwa nao ambao huwapelekea kuteseka kwa maumivu na vifungo mbalimbali vya nguvu za giza, ambapo Nabii Mkuu aliwafungua na kuwatamkia matamko mbalimbali ya kuwapatia uelekeo mpya.
Wakati huo huo Nabii Mkuu ametangaza kuwepo tena jumapili ya tarehe 31/3/019 itakayokuwa ibada kufidiwa muda uliopotea.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio