Tuesday, December 26, 2017

RPC SHANNA: ATAKAEFUNGA BARABARA NA KUCHOMA MATAIRI MKESHA WA MWAKA MPYA KUKIONA.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna ,ametoa onyo kwa watu wenye tabia ya kufunga barabara kwa kuchoma matairi katika mkesha wa mwaka mpya na kupelekea usumbufu kwa watuamiaji wengine wa barabara kuacha kufanya kitendo hicho .

Amesema atakaejaribu kuchoma moto matairi kwenye mkesha huo,jeshi la polisi mkoani hapo litamchukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya kiusalama

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATANO,DEC27,2017


CHADEMA YAPATA PIGO JINGINE, DIWANI SIHA AJIUZULU NA KUHAMIA CCM

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Siha ambaye pia ni diwani wa Gararagua, Zakaria Lukumay amejiuzulu uanachama wa (Chadema) na kujiunga na CCM.
Lukumay ametangaza kujiuzulu siku kadhaa baada ya aliyekuwa mbunge wa Siha (Chadema), Dk Godwin Mollel kujivua ubunge na kujiunga na CCM.
Sawa na Dk Mollel, diwani huyo amesema uamuzi wake unatokana na kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kutetea na kulinda rasilimali za Taifa.

Thursday, December 7, 2017

Marekani Kumuonya Odinga

Raila Odinga
Marekani imemtaka kiongozi wa upinzani nchini kenya Raila Odinga kuacha mpango wake wa kuapishwa kama raisi wan nchi hiyo wiki ijayo.

Saudi Arabia yalaani hatua ya Trump kuutambua Jerusalem kuwa mji mku wa Israel

US President Donald Trump delivers a statement on Jerusalem from the Diplomatic Reception Room of the White House in Washington, DC on December 6, 2017 
Saudi Arabia imelaani hatua ya Marekani ya kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel huku pia shutuma zikizidi kuongezeka kufuatia hatua hiyo.

Trump ameutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel

Israel 
Rais Trump amefanya maamuzi ya kihistoria ya kuipindua sera za miaka mingi ya Marekani kwa kuutambua mji wa Yerusalem kuwa ndio mji mkuu wa Israel.
Rais huyo pia ametangaza kuwa Ubalozi wa Marekani utahamishwa kutoka katika eneo la sasa la Tel Aviv kwenda Yerusalem. 

Polepole Awapiga Dongo CHADEMA.......Kadai Wamefulia, Wanajiandaa Kususia Uchaguzi

Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema  CHADEMA wamefanya kikao cha dharura  kususia uchaguzi wa marudio wa majimbo na kata unaotarajiwa kufanyika January 13 mwakani.

Watuhumiwa watatu wauawa kwa risasi na Polisi

Watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani Kilimanjaro.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo JAlhamisi ya Disemba 7