Thursday, October 8, 2026

TAZAMA PICHA ZA MHE. NABII MKUU PROF. GEORDAVIE KATIKA MKUTANO WA UN-PAF JIJINI DOHA QATAR

Mhe. Nabii Mkuu Profesa GeorDavie ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Agenda  ya Amani na Diplomasia UN-PAF Doha International Peace & Diplomatic Forum 2026, jijini Doha Qatar.

Jukwaa la Kimataifa la Amani, Diploasia, Maendeleo Endelevu na ushirikiano wa Kimataifa.

Katika Mkutano huo Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie alizungumzia kuhusu umuhimu wa kuimarisha ujenzi wa amani katika ukanda wa Ghuba.

Nabii Mkuu amesema "Ghuba ni eneo lenye umuhimu wa kimkakati kwa dunia, likiunganisha mataifa, tamaduni, uchumi na ustaarabu mbalimbali huku akiongeza kuwa kuendelea kwa utulivu wake si jukumu la kikanda pekee, bali ni maslahi ya dunia nzima". 


Pia, amesema kuwa kunapaswa kuimarishwa kwa diplomasia ya kuzuia migogorona kuongeza kuwa ni bora zaidi kutatua tofauti kupitia mazungumzo na uelewano kabla hazijageuka kuwa migogoro.


Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amesema Nchi za Ghuba zimeonesha kwamba diplomasia inaweza kuleta matokeo ya kushangaza na kuongeza kuwa Amani si tu kutokuwepo kwa migogoro, Amani ni uwepo wa haki, utu, fursa, kuheshimiana na uwajibikaji wa pamoja.

“Kwa hiyo, tujenge madaraja badala ya kuta, tuimarishe mazungumzo badala ya mgawanyiko, na tuchague ushirikiano badala ya makabiliano”.

“Tukifanya kazi Pamoja kwa ujasiri, hekima na kujitolea kwa dhati tunaweza kujenga ukanda wa Ghuba ambako amani inadumishwa, maendeleo yanawafikia wote, na vizazi vijavyo vinarithi utulivu na ustawi”.

“Tufanye amani isiwe tu matarajio yetu, bali iwe jukumu letu la Pamoja”.

“Asanteni, na amani, ustawi na ushirikiano viendelee kuuongoza ukanda wa Ghuba na dunia”. Naibu Mwenyekiti (UN-PAF) Mhe. Prof. GeorDavie 

 


 

Wednesday, October 7, 2026

MHE. PROF. GEORDAVIE: AMANI SI TU KUTOKUWEPO KWA MIGOGORO, AMANI NI UWEPO WA HAKI, UTU, FURSA, KUHESHIMIANA NA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA

Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa United Nations Peace Ambassadors Foundation (UN-PAF) amesema kuwa Ujenzi wa amani lazima uanze na mazungumzo ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa majukwaa imara zaidi ambapo serikali,wanadiplomasia, mashirika ya kiraia,viongozi wa dini, vijana na jamii wanaweza kuwasiliana kwa uwazi, heshima na kwa njia yenye kujenga.

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika mkutano UN-PAF Doha International Peace & Diplomatic Forum 2026, uliofanyika jijini Doha, Qatar ambapo alikuwa akizungumzia kuhusu umuhimu wa kuimarisha ujenzi wa amani katika ukanda wa Ghuba.

Katika hotuba yake Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amesema Ghuba ni eneo lenye umuhimu wa kimkakati kwa dunia, likiunganisha mataifa, tamaduni, uchumi na ustaarabu mbalimbali huku akiongeza kuwa kuendelea kwa utulivu wake si jukumu la kikanda pekee, bali ni maslahi ya dunia nzima. Pia, amesema kuwa kunapaswa kuimarishwa kwa diplomasia ya kuzuia migogorona kuongeza kuwa ni bora zaidi kutatua tofauti kupitia mazungumzo na uelewano kabla hazijageuka kuwa migogoro. 

Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amesema Nchi za Ghuba zimeonesha kwamba diplomasia inaweza kuleta matokeo ya kushangaza. Tunapaswa kujenga juu ya utamaduni huu kwa kuendeleza mazungumzo ya kikanda, ushirikiano wa kibinadamu, uendelevu wa mazingira na utatuzi wa migogoro kwa njia ya aman. Amesema Amani si tu kutokuwepo kwa migogoro, Amani ni uwepo wa haki, utu, fursa, kuheshimiana na uwajibikaji wa pamoja.

“Kwa hiyo, tujenge madaraja badala ya kuta, tuimarishe mazungumzo badala ya mgawanyiko, na tuchague ushirikiano badala ya makabiliano”.

“Tukifanya kazi Pamoja kwa ujasiri, hekima na kujitolea kwa dhati tunaweza kujenga ukanda wa Ghuba ambako amani inadumishwa, maendeleo yanawafikia wote, na vizazi vijavyo vinarithi utulivu na ustawi”.

“Tufanye amani isiwe tu matarajio yetu, bali iwe jukumu letu la Pamoja”.

“Asanteni, na amani, ustawi na ushirikiano viendelee kuuongoza ukanda wa Ghuba na dunia”. Naibu Mwenyekiti (UN-PAF) Mhe. Prof. GeorDavie 

MHE. NABII MKUU PROF. GEORDAVIE ASHIRIKI MKUTANO WA UN-PAF DOHA INTERNATIONAL PEACE & DIPLOMATIC FORUM 2026 JIJINI DOHA QATAR

Mhe. Nabii Mkuu Profesa GeorDavie (Balozi Wa Amani) ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa United Nations Peace Ambassadors Foundation (UN-PAF), tarehe 7 oktoba 2026 ameshiriki katika mkutano UN-PAF Doha International Peace & Diplomatic Forum 2026, uliofanyika jijini Doha, Qatar.

Mkutano huo umebeba kaulimbiu inayolenga kujenga madaraja kwa ajili ya amani, diplomasia, maendeleo endelevu na ushirikiano wa kimataifa.

Profesa GeorDavie ametoa hotuba ya Naibu Mwenyekiti, akizungumzia masuala ya diplomasia na amani katika ngazi ya kimataifa.

Jukwaa hilo pia limewahusisha viongozi, mabalozi, wajumbe na wageni mbalimbali kutoka mataifa tofauti, pamoja na utambuzi wa wageni mashuhuri na utoaji wa tuzo na vyeti kwa watu wanaotambuliwa kwa mchango wao katika amani, diplomasia, huduma za kibinadamu na maendeleo endelevu.

Mkutano huo umefanyika katika Best Plaza Hotel, West Bay, Doha, Qatar.


Sunday, October 4, 2026

WATU WAMETAKIWA KUTAMBUA YA KUWA YESU KRISTO YUKO NDANI YA NABII MKUU MHE. PROF. GEORDAVIE

Watu wametakiwa kuendelea kufungua macho na kumtazama Nabii Mkuu Mhe. Prof. GeorDavie kwa sababu Yesu Kristo yu ndani yake.

Hayo yamesemwa hii leo na Mchungaji Kiongozi Mama Anna Davie wakati akiongoza ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko ngurumo ya upako kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni ibada ya kumshukuru Mungu kwa kumuweka Nabii Mkuu katika Taifa letu.

Naye Mtume Modekai katika somo lake la kufungua mioyo ya watu waliofunga kwa ajili yako amesema kuwa ipo mioyo wa watu iliyofungwa kwa ajili yako ili usiweze kuvuka na kufanikiwa.

Kwa upande wake kijana Teresia Teit amesema kuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumuweka Nabii Mkuu katika Taifa hili la Tanzania.

Kijana Moses Elias pia alipata nafasi ya kufundisha katika ibada hiyo kuhusu Hofu na kusema kuwa hofu ni hisia ya asili, wasiwasi au woga unaomjia mtu na inawatesa watu wengi.

Wednesday, September 30, 2026

SERIKALI YAJA NA MIKAKATI KUTOKOMEZA MIGOGORO YA ARDHI

Serikali imetangaza kuunda timu ya wataalamu itakayochunguza migogoro ya ardhi nchini kwa kuangalia vyanzo vyake, ilipofikia na namna ya kuishughulikia.

Timu hiyo itakuwa na wataalamu watakaopitia migogoro hiyo kwa upana, kubaini vyanzo vyake, hatua ilipofikia na hatua zinazoweza kuchukuliwa kuitatua.


Hayo yamebainishwa Septemba 30, 2026 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo wakati wa maadhimisho ya miaka 40 wa Habitat for Humanity Tanzania.

Dkt. Akwilapo amesema Serikali inatambua uwepo wa migogoro ya ardhi na inaendelea kuchukua hatua kuishughulikia.

Amesema kuna migogoro ya aina tofauti ya ardhi akibainisha kuwa baadhi ni halisi huku mingine ikiwa ni migogoro inayotengenezwa, lakini yote inaendelea kushughulikiwa.

CP KOMBO KHAMIS KOMBO AWATAKA MAAFISA HABARI WA JESHI LA POLISI KUENDELEA KUWA NGUZO IMARA.

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo amewataka Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kuendelea kuwa nguzo imara katika kuelimisha na kuhabarisha umma kuhusu masuala ya ulinzi na usalama.

Hayo amezungumza Septemba 28, wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi wa Makao Makuu ya Polisi, Mikoa, Vikosi na Vyuo vya Polisi katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.

CP Kombo, amehimiza nafasi ya Maafisa Habari katika kujenga na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na jamii, huku akiwataka kutumia taaluma yao kuhakikisha umma unapata elimu na taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu Jeshi la Polisi ikiwemo kazi na mafanikio.

Naye, Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama, amesema kuwa kitengo cha habari na uhusiano ndani ya Jeshi la Polisi kimekuwa na mchango mkubwa katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwani jamii imekuwa ikihabarishwa na kujengewa uwezo wa kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu kabla haujatokea katika  maeneo yao.


NABII MKUU MHE. PROF. GEORDAVIE LEO HII KUSHIRIKI KONGAMANO LA 15 LA UMOJA WA MATAIFA ABU DHABI, FALME ZA KIARABU.

Nabii Mkuu Mhe. Prof. GeorDavie amepata mwaliko wa kushiriki katika Kongamano la 15 la Umoja wa Mataifa kuhusu Kuzuia Uhalifu na Haki Jinai, linalofanyika mjini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.

Kwa mujibu wa barua rasmi kutoka International Association of World Peace Advocates (IAWPA), Prof. GeorDavie amealikwa kushiriki katika kongamano hilo tarehe 1 Oktoba 2026.


Mwaliko huo unatokana na kutambua uongozi wake na dhamira yake katika kujenga amani, huku akiteuliwa kuwa miongoni mwa wazungumzaji katika kongamano hilo.

Kongamano hilo linawakutanisha wadau mbalimbali wa kimataifa kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu kuzuia uhalifu, haki jinai pamoja na juhudi za kukuza amani na usalama katika jamii na duniani kwa ujumla.

Katika ushiriki wake Prof. GeorDavie anatarajia kutoa mchango wake kupitia uzoefu na mtazamo wake katika masuala ya amani, umoja na maendeleo ya jamii, akiwa sehemu ya jukwaa hilo la kimataifa.

Ushiriki huo pia unaiweka Tanzania katika nafasi ya kuwakilishwa kwenye jukwaa la kimataifa linalojadili masuala muhimu yanayohusu amani, haki na usalama wa jamii.


Monday, September 28, 2026

PROF. GEORDAVIE: UKIWA MTU MWENYE AKILI YA KIFALME INAKUPA WEPESI WA KUPOKEA MIUJIZA NA BARAKA MBALIMBALI

Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amemtaka kila mmoja kufikiri kama mtu wenye akili ya kifalme kwani itamsidia kupokea miujiza na baraka mbalimbali katika maisha

Ameyasema hayo jumapili ya tar. 27 Oktoba 2026 katika ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni ibada ya KUPOKEA UTAYARI KWA AJILI YA KUFANIKISHA KILA JAMBO LAKO.

Mhe. Nabii mkuu amesema kuwa kwa sababu ufalme wa Mungu uko ndani ya mtu hata napokuwa akitamka neno kwa ajili yako inakuwa na urahisi wa wewe kupokea.

Pia katika ibada hiyo Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie alizindua kitabu kingine kinachosema ELEWA MFUMO WA MAMLAKA YA UFALME ambapo amesema kitabu hicho kitakusaidia kujifunza kujua tofauti ya neno la Mungu na kujua jinsi ya UFALME unavyofanya kazi.

Aidha hicho ni kitabu cha sita tangu aanze kuandika vitabu ambapo vitabu vingine alivyoviandika Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie ni Pamoja na AFRIKA MOJA, AMANI NA DIPLOMASIA, UCHUMI NA MAENDELEO YA SERIKALI YA UFALME WA MUNGU, KUENENDA NA VIWANGO VYA SERIKALI TUKUFU YA UFALME WA MUNGU Pamoja na MTUMISHI ALIYEJERUHIWA UPONYAJI NA UREJESHO.


Saturday, September 26, 2026

MHE. NABII MKUU PROF. GEORDAVIE KUZINDUA KITABU KIPYA CHA ELEWA MFUMO WA MAMLAKA YA UFALME

Mhe.Nabii Mkuu Prof. GeorDavie Jumapili ya tar. 27 septemba 2026 anatarajia kuzindua kitabu kipya cha ELEWA MFUMO WA MAMLAKA YA UFALME kikiwa ni kitabu cha 6 tangu Nabii Mkuu aanze kuandika vitabu.

Uzinduzi huo utafanyika kupitia ibada ya KUPOKEA UTAYARI KWA AJILI YA KUFANIKISHA KILA JAMBO LAKO itakayofanyika katika nyumba ya matamko ngurumo ya upako kisongo Arusha.

Katika ibada hiyo pia watu watu wote watapata nafasi ya kuleta sadaka ya mavuno ghalani ili kuzidi kuenzi kazi kubwa ya kiroho aliyoifanya Mhe. Nabii Mkuu katika maisha yetu.

Aidha ibada hiyo itaambatana na sherehe ya kumkaribisha Nabii Mkuu na itahudhuriwa na maelfu ya watu kutoka ndani ya nchi huku wengine wakitoka mataifa mbalimbali duniani.

 



Sunday, September 20, 2026

WATU WAPASWA KUKAZA KATIKA KUMFUATA MTU ALIYEBEBA KUSUDI LA MAISHA YAO

Imeelezwa kuwa adui anajua mtu aliyebeba hatma ya maisha ya watu ndio maana anapiga vita watu kumfuata mtu aliyebeba hatma ya maisha yao.

Hayo yamesemwa hii leo na Mwalimu wa Neno la Mungu Isaya Benson wakati akihubiri katika ibada ya kusanyiko la vituo juu ya mwamba ya maandalizi ya ibada kuu ya tar 27 sept ambayo Nabii Mkuu Mhe. Prof. GeorDavie atakuwepo.

Amesema kuwa watu wanapaswa kukaza katika kumfuata Mtu aliyebeba kusudi kwa sababu hatma Mungu ameiunganisha na Mtu Mkuu wa Mungu ambaye ni Nabii Mkuu.

Kwa upande wake Mchungaji Restituta Melchiades amesema ili tuweze kupokea kile anachokuja nacho Mtu Mkuu wa Mungu ni lazima tujiweke katika utii, umoja, nidhamu na utakatifu huku tukiwa na Moyo safi na Imani ya kupokea kutoka kwa Mtu Mkuu wa Mungu.

Awali wasimamizi wa vituo juu ya mwamba wamepata nafasi ya kufundisha neno ambapo wamewataka watu kuendelea kuwa watii, wanyenyekevu na kuyashika matamko ya kinabii ili waweze kufanikiwa maeneo mbalimbali maishani mwao.

TUNAPOTENGENEZA NJIA YA BABA TUNATENGENEZA NJIA YA KRISTO YESU

Imeelezwa kuwa tunapotengeneza njia ya Bwana, na kwamba tunapotengeneza njia ya Baba tunatengeneza njia ya Kristo yesu.

Hayo yameelezwa hii leo na Mchungaji Kiongozi Mama Anna Davie wakati akiongoza ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko Ngurumo ya Upako Kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni ibada ya kuimarishwa hatua zako kwa imani.

Kwa upande Mtume Petro Mwamba akihubiri katika ibada hiyo kupitia somo lililokuwa na kichwa kisemacho wewe ni Mshindi amesema kuwa ndani ya ushindi kuna majibu na maombi yako yana ushindi hata kama hujayaona bado yanaishi.

Naye Mtume Ester Robert akifundisha kuhusu Mashujaa Watatu amesema kuwa shujaa ni mtu mwenye ujasiri mkubwa anayekabili hatari, matatizo au changamoto ngumu kwa ajili ya kusaidia wengine au kutetea haki bila kuogopa ana nguvu ya kuamini ushindi tu na siku zote haamini katika kushindwa, ana nia ya ndani ya moyo na msukumo wa ndani wa nguvu ya imani.

Kijana Moses Elias naye amepata nafasi katika ibada hiyo ambapo amesema kuwa watu wanatakiwa kuangalia ni kitu gani wanachozungumza wakati wakiwa kwenye mapito au furaha kwa sababu kuna maneno unayoweza kuzungumza yakaiharibu kesho yako.


Monday, August 24, 2026

MTUME KATHRYN KRICK ASEMA ANAWEZA KUFANYA CHOCHOTE AMBACHO MUNGU AMEMUAGIZA KUFANYA

Kiongozi wa kanisa la @5fchurch @apostlekathrynkrick amesema anaweza kufanya chochote ambacho Mungu amemuagiza kukifanya bila kujali watu watasemaje kuhusu jambo hilo.

Ameyasema hayoo siku ya jana kwenye ibada katika kanisa la 5F church lililopo los angles Marekani.

Ameeleza amejinza hayo kutoka kwa baba yake wa kiroho Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie ambaye ni mtu jasiri na anayefanya mambo ambayo Mungu amemuamrisha kuyafanya bila kujali maneno ya watu.

Aidha amesema anamuheshimu baba yake wa kiroho Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie kama Biblia inaelekeza kuwaheshimu wanaoshtahili heshima.

Mtume Kathryine krick amekuwa akifanya huduma za kiroho katika nchi mbalimbali duniani Zaidi ya 190 huku akiowaombea Baraka na uponyaji kwa nguvu ya Mungu inayowashangaza mataifa.