Wednesday, August 19, 2026

SERIKALI YATOA MAELEKEZO KUADIMIKA KWA SARUJI

Serikali imewapa siku saba wamiliki wa viwanda vya kuzalisha saruji nchini kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto ya bei ya saruji inayotajwa kuwa juu katika soko pamoja na upatikanaji wake.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, kukutana na kufanya mazungumzo na wamiliki wa viwanda vya saruji Agosti 18, 2026 jijini Dodoma.

Salum amesema, kikao kimelenga kutafuta suluhu ya changamoto iliyosababisha kuadimika kwa bidhaa hiyo na bei kuwa juu sokoni.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika na udhibiti, viwango na masoko, ikiwemo Tume ya Ushindani (FCC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), TanTrade, pamoja na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Salum amesisitiza umuhimu wa kupata suluhu ya kudumu itakayosaidia kuhakikisha saruji inapatikana kwa bei inayozingatia maslahi ya wazalishaji, wafanyabiashara na wananchi.

No comments:

Post a Comment