Sunday, September 20, 2026

WATU WAPASWA KUKAZA KATIKA KUMFUATA MTU ALIYEBEBA KUSUDI LA MAISHA YAO

Imeelezwa kuwa adui anajua mtu aliyebeba hatma ya maisha ya watu ndio maana anapiga vita watu kumfuata mtu aliyebeba hatma ya maisha yao.

Hayo yamesemwa hii leo na Mwalimu wa Neno la Mungu Isaya Benson wakati akihubiri katika ibada ya kusanyiko la vituo juu ya mwamba ya maandalizi ya ibada kuu ya tar 27 sept ambayo Nabii Mkuu Mhe. Prof. GeorDavie atakuwepo.

Amesema kuwa watu wanapaswa kukaza katika kumfuata Mtu aliyebeba kusudi kwa sababu hatma Mungu ameiunganisha na Mtu Mkuu wa Mungu ambaye ni Nabii Mkuu.

Kwa upande wake Mchungaji Restituta Melchiades amesema ili tuweze kupokea kile anachokuja nacho Mtu Mkuu wa Mungu ni lazima tujiweke katika utii, umoja, nidhamu na utakatifu huku tukiwa na Moyo safi na Imani ya kupokea kutoka kwa Mtu Mkuu wa Mungu.

Awali wasimamizi wa vituo juu ya mwamba wamepata nafasi ya kufundisha neno ambapo wamewataka watu kuendelea kuwa watii, wanyenyekevu na kuyashika matamko ya kinabii ili waweze kufanikiwa maeneo mbalimbali maishani mwao.

TUNAPOTENGENEZA NJIA YA BABA TUNATENGENEZA NJIA YA KRISTO YESU

Imeelezwa kuwa tunapotengeneza njia ya Bwana, na kwamba tunapotengeneza njia ya Baba tunatengeneza njia ya Kristo yesu.

Hayo yameelezwa hii leo na Mchungaji Kiongozi Mama Anna Davie wakati akiongoza ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko Ngurumo ya Upako Kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni ibada ya kuimarishwa hatua zako kwa imani.

Kwa upande Mtume Petro Mwamba akihubiri katika ibada hiyo kupitia somo lililokuwa na kichwa kisemacho wewe ni Mshindi amesema kuwa ndani ya ushindi kuna majibu na maombi yako yana ushindi hata kama hujayaona bado yanaishi.

Naye Mtume Ester Robert akifundisha kuhusu Mashujaa Watatu amesema kuwa shujaa ni mtu mwenye ujasiri mkubwa anayekabili hatari, matatizo au changamoto ngumu kwa ajili ya kusaidia wengine au kutetea haki bila kuogopa ana nguvu ya kuamini ushindi tu na siku zote haamini katika kushindwa, ana nia ya ndani ya moyo na msukumo wa ndani wa nguvu ya imani.

Kijana Moses Elias naye amepata nafasi katika ibada hiyo ambapo amesema kuwa watu wanatakiwa kuangalia ni kitu gani wanachozungumza wakati wakiwa kwenye mapito au furaha kwa sababu kuna maneno unayoweza kuzungumza yakaiharibu kesho yako.