Wednesday, February 25, 2015

Majeshi ya DRC yashambulia ngome ya FDLR.



 
Vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo FARDC, vimeanzisha hatua za kijeshi dhidi ya waasi wa Rwanda wa kundi la FDLR.Katika vijiji vya Ruvuye na Mulindi katika misitu ya maeneo ya mji wa Lemera tarafani Uvira mkoani Kivu ya kusini.
Baadhi wa wajumbe wa kundi hilo wanashutumiwa kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda kabla ya kutoroka katika nchi jirani ya Jammuhuri ya kidemokrasi ya Congo

Friday, February 20, 2015

IBADA YA CHUO CHA UPONYAJI,TAREHE 19/February/2015




Maelfu ya watu waliohudhuria katika chuo cha uponyaji  leo katika hema la kukutania kisongo nje kidogo ya Jiji La Arusha   wametoa sadaka ya kujiepusha na majanga, ambapo hivi karibuni Nabii Mkuu Mheshimiwa Dr.GeorDavie alitoa unabii utakaodumu hadi mwezi wa sita kuwa kutatokea majanga mbalimbali nchini.

Monday, February 16, 2015

IBADA YA JUMAPILI.TAREHE 15/February/2015




Baraka mbalimbali za kinabii zimeendelea kumiminika kwa Maelfu ya watu walioudhuria ibada ya Jiji Chuo Kikuu cha Manabii Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Katika ibada hiyo Nabii Mkuu Mheshimiwa Dr GeorDavie  ametangaza Baraka mpya ya

Thursday, February 12, 2015

IBADA YA CHUO CHA UPONYAJI TAREHE 12/February/2015.



Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie ametoa Unabii wa Muda wa miezi mitano kuanzia Februari hadi June mwaka huu kuwa kuna mambo yatakayotokea ambayo yatakuwa ya kushangaza. Mh.Dr.GeorDavie ametoa Unabii huo leo wakati wa ibada ya Chuo cha Uponyaji iliyofanyika katika hema la Kukutania la Ngurumo ya Upako Chuo Kikuu cha Manabii  Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.

Wednesday, February 11, 2015

NIGER YACHAGUA VITA DHIDI YA BOKO HARAM.


Bunge la Niger limepiga kura kwa kauli moja, kutuma vikosi nchini Nigeria kujiunga na mapambano ya kikanda dhidi ya kundi la Boko Haram. Kulingana na azimio la bunge hilo, Niger itatuma wanajeshi 750 nchini Nigeria. 

Wavuvi hawaendi tena ziwani kuvua, wakulima hawaendi tena mashambani, shule zimefungwa. Wakaazi wa maeneo ya mpakani ya Diffa na Bosso, kusini mwa Niger wamejawa na hofu, kutokana na magaidi waliojigeuza wapiganaji wa jihadi, ambao wanatishia usalama wa taifa lao." Hao ni makatili tu wasioheshimu sheria, wanaiba, kuuwa, na kubaka," alisema Abdou Lokoko, mfanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali nchini Niger.

Monday, February 9, 2015

IBADA YA JUMAPILI. TAREHE 8/February/2015




Wakazi wa Mkoa wa Arusha  na maeneo mbalimbali walihudhuria jumapili hii  katika ibada ya jiji katika hema la kukutania Chuo Kikuu cha Manabii Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha wamepokea  Baraka mbalimbali za Kinabii.

Thursday, February 5, 2015

HUDUMA YA NGURUMO YA UPAKO ILIYOKO CHINI YA NABII MKUU MH.DR.GEORDAVIE IMETOA MSAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI KUMI .



Huduma ya Ngurumo ya Upako iliyoko chini ya Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie leo imetoa msaada kwa vituo sita vya watoto yatima wenye thamani ya shilingi milioni kumi .

Msaada huo ambao ni vitu mbalimbali kama Mchele, sukari, mafuta ya kupikia pamoja na sabuni umekabidhiwa kwa walezi wa vituo hivyo lengo likiwa ni kuwasaidia watoto hao ili nao wajione kuwa sawa na watoto wengine wenye wazazi.

Monday, February 2, 2015

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 2/February/2015


Maelfu ya watu wamekusanyika katika chuo kikuu cha manabii kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha kwenye ibada ya jiji ambayo iliongozwa na Nabii mkuu Dr. GeorDavie na kupokea Baraka mbalimbali za kinabii.