Friday, February 20, 2015

IBADA YA CHUO CHA UPONYAJI,TAREHE 19/February/2015




Maelfu ya watu waliohudhuria katika chuo cha uponyaji  leo katika hema la kukutania kisongo nje kidogo ya Jiji La Arusha   wametoa sadaka ya kujiepusha na majanga, ambapo hivi karibuni Nabii Mkuu Mheshimiwa Dr.GeorDavie alitoa unabii utakaodumu hadi mwezi wa sita kuwa kutatokea majanga mbalimbali nchini.


 Katika ibada hiyo watu wamefunguliwa katika vifungo mbalimbali huku watu wakishuhudia matendo makuu anayotenda Mungu kupitia mtumishi wake Nabii Mkuu Mheshimiwa Dr GeorDvie.

Akishuhudia Bi.Maria ambaye kwa muda wa miaka 37 amekuwa akisumbuliwa  na ugonjwa  wa akili amesema kuwa katika kipindi chote hicho amekuwa akiishi katika mazingira  magumu na kutafuta huduma ya uponyaji kwa watumishi mbalimbali bila mafanikio.
Kuhusu Unabii huo alioutoa Dr.GeorDavie amewataka Wanangurumo na wale wote wanaomini nguvu ya kinabii kuendelea kufuatilia matakamko mbalimbali ya kinabii aliyotoa.

Aidha Nabii Mkuu Mheshimiwa Dr.GeorDavie amesema atakuwepo tena siku ya alhamisi ya tarehe 26 mwezi huu wa February ambapo watu watafunguliwa katika vifungo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment