Wednesday, May 30, 2018

Petroli yasafirishwa kwa chupa kutoka Dar es Salaam hadi Mafia

Vibanda vya kuuza mafuta kama hivi vimekuwa msaada mkubwa kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri 
Kisiwani Mafia Tanzania, Mafuta ya petrol na dizeli huuzwa kwa reja reja katika vibanda, huku kukiwa hakuna sheli ya mafuta kwa ajili ya mahitaji ya matumizi ya watu wenye vyombo vya usafiri kisiwani humo.

Walioshtakiwa ulaji rushwa Kenya kukaa rumande wiki moja

Mkurugenzi Mkuu wa NYS Richard Ndubai akiwa mahakamani Jumanne 
Watuhumiwa 24 walioshtakiwa kuhusiana na kashfa ya ufujaji wa pesa katika Shirika la Vijana wa huduma kwa Taifa (NYS) watakaa rumande kwa wiki moja.

Bashiru Ali Kakurwa atangazwa kuwa katibu Mkuu mpya wa CCM

Rais Magufuli na Bashiru Ali Katibu Mkuu mpya wa CCM 
Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM nchini Tanzania imemteua Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Lugola Akiri Changamoto Upatikanaji Taarifa Sahihi Za Wazanzibar


Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imesema changamoto iliyopo katika kupata taarifa sahihi za Wazanzibar wanaopata ajira katika Taasisi za Muungano anuani ya makazi.

Wednesday, May 23, 2018

Rais Trump atilia shaka mkutano adimu na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un

Rais Trump



Rais Trump ametilia shaka kufanyika mkutano adimu na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mwezi june huko Singapore .

Rwanda kushirikiana na Arsenal kuimarisha utalii

Arsenal kutangaza utalii wa Rwanda




Rwanda imetangaza mpango wa ushirikiano na timu ya Arsenal inayocheza ligi kuu ya England.Ushirikiano huo wa miaka 3 unalenga kuimarisha sekta ya utalii nchini Rwanda,uwekezaji na maendeleo ya mchezo wa soka.

Mahiga: Watanzania Waishio Nje Hutuma Fedha Nyingi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga amesema Watanzania waishio nje ya nchi wanatuma zaidi ya Sh trilioni moja nchini kwa mwaka.

Hakuna Mtu Aliyethibitika Kuwa Na Ugonjwa Wa Ebola Na Hakuna Ugonjwa Huu Tanzania


NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto dkt. Faustine Ndugulile amethibitisha kuwa hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa EBOLA hapa nchini wala hakuna ugonjwa huo hapa Tanzania.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 23

Maofisa Watatu Kituo cha Uwekezaji cha nchini ( TIC ) Wafariki kwa Ajali

Maofisa watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini  (Tanzania Investment Center (TIC) wamefariki dunia katika  ajali ya gari usiku wa kuamkia jana Mei 22, 2018 maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.

Tibaijuka: Kwa Hili Serikali ni Lazima Iwajibike.....Utawala wa Sheria Uheshimiwe

Mbunge wa Muleba Kusini(CCM), Profesa Anna Tibaijuka ameitaka serikali ya awamu ya tano iwajibike kuwanunulia ng'ombe wafugaji walioshinda kesi zao Mahakamani kama sheria inavyosema nasio vinginevyo.

Friday, May 18, 2018

Korea Kaskazini na Marekani: Kwa nini Kim Jong-un anamuogopa Donald Trump

Kim Jong-un (L) talking with South Korea's President Moon Jae-in (R) before the inter-Korean summit at the Peace House building on the southern side of the truce village of Panmunjom on 27 April (picture released by North Korean state media)\
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa matamshi yanayokinzana na ya mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa, akisema mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia hauwezi kutumiwa nchini Korea Kaskazini.

Trump Amgeuka Mshauri Wake Kuhusu Kuifanya Korea Kaskazini Kama Libya

Rais wa Marekani, Donald Trump amepinga kauli ya mshauri wake mkuu wa masuala ya ulinzi, John Bolton aliyedai kuwa mfumo wa kuondoa silaha za kinyuklia nchini Korea Kaskazini utafanana na uliotumika Libya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 18

Mwakyembe Awataka Vijana kuiga Mfano Wa Flaviana Matata


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amempongeza mwanamitindo wa kimataifa Bibi. Flaviana Matata kwa juhudi za kusaidia watoto wa kike kupata elimu kwa kuwawezesha  vifaa muhimu vya shule ikiwemo ada na madaftari.

Saturday, May 12, 2018

breaking news:Watu 26 wauawa katika shambulio Burundi

Raia waliokuwa wakiandamana nchini Burundi wakipinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu 2015 
serikali ya Burundi inasema kuwa watu 26 wameuawa wakati wa shambulio kaskazini magharibi wa taifa hilo.

KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA SINGIDA UNITED LEO


simba_1wg9iatlvvie114248gh77zh68
Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Singida United, mchezo wa Ligi Kuu Bara

WAAMUZI WAWILI WAONDOLEWA KUCHEZESHA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KWA MCHEZO MCHAFU


Nembo-ya-TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limewaondoa Waamuzi wawili kwenye orodha ya Waamuzi wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inayoendelea kwenye vituo vinne vya Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KATIBU MKUU SEKRETARIETI YA NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU OFISINI KWAKE MJINI DODOMA


V25A6390

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na mgeni wake Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

Waziri Ummy Mwalimu apewa tuzo ya heshima


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM), amepewa tuzo ya heshima na klabu ya soka ya Coastal Union ya jijini Tanga.

Forbes yatangaza watu 10 wenye ushawishi zaidi Duniani


Kiongozi wa China Xi Jinping ndiye mtu mwenye ushawishi Zaidi duniani, kwa mujibu wa jarida la Forbes. Amechukua nafasi hiyo baada ya bunge China kumpa mamlaka zaidi na kuondoa kikomo cha muhula wa rais.

Waziri Mkuu Azuiwa Kusafiri


Waziri Mkuu wa zamani Najib Razak na mkewe Rosmah Mansor wamezuiwa kuondoka nchini, Idara ya Uhamiaji imesema Jumamosi.

Thursday, May 10, 2018

Watu 27 wafariki baada ya bwawa la Patel kuvunja kuta zake Nakuru Kenya

Mamia ya makaazi ya watu yaliosombwa na maji 

Watu 27 wamefariki na maelfu wengine wameachwa bila ya makaazi wakati bwawa moja mjini Nakuru nchini Kenya lilipovunja kuta zake Jumatano usiku.

Malaysia yapata kiongozi mkongwe zaidi duniani aliyechaguliwa

Dr.Mahathir Mohamad aibuka mshindi akiwa na miaka 92
Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia Dr.Mahathir Mohamad amepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi mkuu uliofanyika katika hilo. Kiongozi huyo ameweza kukiangusha chama ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1957 ambacho kimekuwa kikidaiwa kujihusisha na nasuala ya rushwa na ufisadi.

KAULI CHANYA AMBAZO HUTASIKIA POPOTE KUHUSU ''MATATIZO /MAKOSA''

Nashindwa hata niongelee vipi neno tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi jamii.na taifa hadi taifa.

Serikali yaja na Mbinu mpya kudhibiti wizi wa bili za maji na wakwepaji kodi

Katika kuongeza mapato kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na kupunguza malalamiko ya wananchi ya kulalamikia kuibiwa pindi wanapolipa bili ya maji serikali ya halmashauri hio chini ya Shirika lisilo la kiselikari lijulikanalo kwajina la Water aid limeunda mfumo mpya wa upatikanaji wa maji ujulikanao kwa jina la e water ambao utadhibiti mianya ya ukwepaji kodi

MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEP MBILINYI “SUGU” AACHIWA HURU LEO


index
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wakilakiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mh. Freeman Mbowe mara baada ya kuachiwa huru leo Alhamis Mei 10,2018 jijini Mbeya.

Friday, May 4, 2018

Atletico Madrid 1-0 Arsenal: Diego Costa afunga na kuwazuia Gunners kufika fainali Europa League

Diego Costa 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alipoteza fursa pekee ya kushinda kombe msimu wake wa mwisho akiwa katika klabu hiyo baada ya kuchapwa na Atletico Madrid katika nusu fainali ya ligi ndogo ya klabu Ulaya Europa League.

Dhlakama kiongozi wa RENAMO afariki

Afonso Dhlakama 

Chama cha Upinzani nchini Msumbiji kimesema kuwa kiongozi wake wa muda mrefu Afonso Dhlakama amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, akiwa na miaka 65.

Manara apewa onyo kali na Bodi ya Ligi Kuu, aomba radhi


Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amepewa onyo kali na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutoka na yeye kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 29, 2018.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 4


Ndalichako Apinga Walimu Wakuu Kusimamishwa Kazi Kisa Matokeo Mabovu


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewajia juu baadhi ya watumishi wa serikali ambao wanatabia ya kuwafukuza kazi walimu wakuu wa shule ambao hutoa matokeo mabaya katika mitihani ya Taifa.

Thursday, May 3, 2018

Rais Magufuli ahoji :Kwani kusoma ni kujua Kiingereza?


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amehoji wanafunzi wa chuo cha Mkwawa iwapo  kujua kusoma ni kujua Kiingereza.

Wabunge, Wahadhiri Acheni Ukware Waacheni Wanafunzi Wasome


Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ametoa wito kwa wabunge kutojihusisha na vitendo vya kingono na wafunzi wa vyuo vikuu na wawaache wasome.

Watakaopandisha Bei Ya Sukari Ramadhani Kukiona


Serikali imeagiza wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa biashara kufuatilia na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaopandisha bei ya sukari kwa makusudi katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi wa mfungo wa Ramadhani.

Wednesday, May 2, 2018

Ajira 10,140 za walimu wa shule za msingi kutolewa Juni


Serikali imesema Juni 30, 2018 inatarajia kutoa ajira 10,140 za walimu wa shule za msingi nchini.

Bei ya petroli yashuka, mafuta ya taa yapaa


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), juzi  ilitangaza kushuka kwa bei ya petroli na dizeli kwa asilimia 2.7 na asilimia 3.8; na ongezeko la asilimia 0.09 kwa mafuta ya taa.

Serikali Yasema Bungeni Hakuna Njaa Nchini


Serikali imesema inapata tabu kukiri kuwa kuna hali ya njaa nchini kwa kuwa mvua zimenyesha za kutosha mwaka huu.

Tuesday, May 1, 2018

Hii ndio idadi ya watumishi serikali inayotarajia kuwaajiri



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa tangu aingie madarakani wameajiri jumla ya watumishi 18,101 katika sekta mbalimbali nchini.

Akizungumza leo Mei 1 mkoa Iringa katika siku ya Wafanyakazi ambapo amesema jumla ya watumishi 22,150 wanatarajia kuwaajiri.

Mbwana Samatta awaonya Serengeti Boys kufuatia ushindi wao wa kombe la CECAFA


Tokeo la picha la MBWANA SAMATTA
Mshambuliaji wa Taifa Stars  na Klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amewaonya vijana wa timu ya taifa ya mpira wa miguu waliochini ya miaka 17, Serengeti Boys kwa kuwataka waache kubweteka kufuatia ushindi wa kombe la CECAFA mwaka 2018.
Mbwana Samatta

Waziri Mahiga aomba radhi kwa Rais Magufuli

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga ameomba radhi kwa Rais Magufuli kwa niaba ya watu wa Iringa kwa kukosa kura 25 kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka 2015.

Rais Magufuli akataa ombi la nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekataa ombi la kuongeza mshahara kwa wafanyakazi iliyoombwa na TUCTA.

SIKILIZA LIVE SASA IBADA YA CHUO CHA MANABII..

 


SIKILIZA N.Y.U REDIO 99.3 FM ,SASA UWEZE  KUFUATILIA  IBADA YA CHUO CHA MANABII IBADA HIYO INAFANYIKA KATIKA HEMA LA KUKUTANIA KISONGO ARUSHA .