Thursday, August 31, 2017

Sampuli ya ukuta kujengwa Marekani

Marekani 
Utawala wa rais Donald Trump umechagua makampuni manne kwa kazi ya kujenga sampuli ya ukuta ambao rais Trump ulitangaza sana juu ya mpaka wa Mexico na nchi yake.

Harbinder Sethi wa Escrow kawekewa Maputo tumboni


Wakili wa mshtakiwa Harbinder Sethi, Joseph Makandege ameulalamikia upande wa Jamhuri kwa kushindwa kumpeleka mteja wake Hospitali ya Taifa Muhimbili kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilivyoamuru.

Rugemalira wa Escrow agonga mwamba Mahakama ya Mafisadi


 Mshtakiwa wa kesi ya uchotaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, James Rugemalira amegonga ukuta katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi) baada ya kunyimwa dhamana.

Rugemalira ambaye anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yenye mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana, alikimbilia mahakamani hapo kuomba afutiwe mashtaka ya utakatishaji fedha kisha aachiwe huru kwa dhamana kwa madai hati ya mashtaka yanayowakabili ina kasoro za kisheria.

Jana, Jaji Mfawidhi Firmin Matogolo alitupilia mbali maombi hayo akisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpa nafuu alizokuwa akiziomba.

Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga Akamatwa kwa Amri ya Mahakama Kuu


Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.

KUWENI NA IMANI KWA MUNGU.



        BALOZI WA NABII MKUU TANZANIA MTUME SEKELA N'TONDOLO

watu wametakiwa kuwa na imani kwa mungu kupitia watumishi wake anaowatumia kwani itawasaidia kufanikiwa katika mambo  mbalimbali maishani .

Wednesday, August 30, 2017

WATU WAKUMBUSHWA KUFIKA HEMAINI MWA BWANA.

Kadinali wa pili wa huduma ya ngurumo ya upako mchungaji Elizabeth Hamphrey amewakumbusha watu wote kuhudhuria ibada ya Baraka ya chuo cha manabii itakayofanyika siku ya kesho katika hema la kukutania kuanzia saa sita kamili mchana.
Akizungumza na N.Y.U Radio  Mchungaji Elizabeth Humphrey amesema kuwa ni vyema kila mmoja kufika mbele za bwana ili kufundiswa neno la Mungu ikiwa ni

LIVERPOOL KUMSAJILI OXLADE CHAMBERLAIN.

Liverpool imekubali kuilipa Arsenal dau la £40m kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Alex Oxlade Chamberlain.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikataa uhamisho wa Chelsea siku ya Jumanne baada ya makubaliano kuafikiwa, atajiunga na Liverpool kwa kandarasi ya miaka mitano ambapo atakuwa akipokea £120,000 kwa wiki.
Liverpool imekubali kuilipa Arsenal dau la £40m kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Alex Oxlade Chamberlain
Oxlade Chamberlain ambaye yuko mwaka wake wa mwisho wa

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO, Alhamisu,August31,2017.


Tuesday, August 29, 2017

BUNGE LA CHINA LAUWEKEA SHERIA WIMBO WA TAIFA.

Bunge la China linatafakari juu ya rasimu ya sheria ambayo itarasimisha kuwa ni kosa la jinai linalostahili hukumu ama kifungo juu ya tabia ya kudharau wimbo wa kitaifa wa nchi hiyo.
China
Kosa kubwa zaidi litakalochukuliwa kama uhalifu mkubwa ni kwa wale,

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO, Jumanne,August30,2017.


WAFUNGWA KUPATIWA KAZI MAGEREZA KWA MIKATABA MAALUMU

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la Magereza na idara zingine zenye mashirika ya uzalishaji ambazo zipo chini ya wizara yake zifanye uzalishaji mali pamoja na kuwatumia wafungwa katika kufanya kazi ndani ya jeshi.
Waziri Nchemba ameongea hayo akiwa katika ufunguzi wa nyumba tano za

Monday, August 28, 2017

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO, Jumanne,August29,2017.


BODABODA WASIOVAA KOFIA NGUMU KUKAMATWA.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwakamata wamiliki wapikipiki ambao watashindwa kuwa na kofia ngumu za pikipiki maarufu kama bodaboda.
Waziri Mwigulu ameyaongea hayo akiongea na madareva wa pikipiki wa wilaya ya shinyanga ambao wanapatiwa mafunzo ya usalama barabarani mkoani

POLISI, JAJI MKUU WATOA ONYO KUHUSU MGOMO WA MAWAIKILI NCHINI

Kaimu  Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini, wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi, vinavyochunguza tukio la mlipuko, uliotokea kwenye ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.
Profesa Juma jana  alisema TLS hawana haki ya kutoa agizo kwa mawakili, kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza mengine, kwa kuwa kila wakili ana mkataba binafsi na mteja wake.

POLISI SINGIDA WAUA MTU MMOJA AKIDAIWA KUWA JAMBAZI.

Mkazi wa kijiji cha Shiponga, Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.

Saturday, August 26, 2017

Zitto Kabwe Aeleza Kwa Nini Yeye Hakamatwi na Polisi Licha ya Kuikosoa Serikali


Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe, amesema pamoja na kuwa ni mwanasiasa na upinzani na miongoni mwa watu wanaokosoa serikali, atahakikisha anafanya hivyo pasipo kukamatwa na jeshi la polisi.

Akiwajibu wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter ambao walikuwa wanashangaa kwa nini yeye hasumbuliwi na polisi licha ya kuongea maneno ya kuikosoa serikali kama inavyotokea kwa wengine, Zitto Kabwe amesema hataki na hapendi kufanyiwa hivyo, na atajitahidi kukwepa kitendo hicho.

“Sitaki na sipendi kukamatwa, itokee kwa kuwa imebidi, lakini kama ipo ndani ya uwezo wangu kukwepa kukamatwa nitahakikisha sikamatwi”, aliandika Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe aliendelea kutoa maelezo ya suala hilo akitolea mfano wa viongozi mbali mbali wa Afrika ambao walikuwa wanaharakati na wanasiasa waliokuwa wakikososa serikali, lakini hawakuwahi kusumbuliwa kisheria mpaka ndoto zao zilipotimia.

“Kagame alikuwa mpiganaji na leo yupo madarakani kwa kuwa hakutaka kukamatwa, Meles mpiganaji dhidi ya The Derg akiwa na umri mdogo wa miaka 19 mpaka 36 akawa Rais wa Ethiopia 39 hakukamatwa”, aliandika Zitto Kabwe.

Hivi karibuni mwanasiasa na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alikamatwa na polisi kwa kile kilichoelezwa kutoa taarifa za uchochezi.

Tembo Avamia Kijiji......Aua Mtu Mmoja Kwa Kumkanyaga na Kujeruhi Mwingine


Kijana Emmanuel Ernest wa kitongoji cha Ilolo, Mvumi Misheni wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo huku mwingine akijeruhiwa vibaya baada ya tembo huyo kuvamia mashamba ya zabibu.

Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Feri Dar na kutoa maagizo kwa RC Makonda


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 25 Agosti, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Feri na kisha kuvuka bahari kwa kutumia kivuko cha MV Kigamboni ambako amekutana na wananchi wa Kigamboni, ametembelea Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere na ametembelea Daraja la Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya August 26



Polisi Yaanza Kuchunguza Mlipuko Ulioteketeza Ofisi za Mawakili Fatma Karume na Lawrence Marsha


Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Agosti 26.

Friday, August 25, 2017

NDUGAI ATOA ONYO KWA WABUNGE WATAKAOFANYA VURUGU BUNGENI.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wabunge watakaofanya vitendo vya utovu wa nidhamu bungeni hawatavumiliwa na huenda adhabu ikaongezeka maradufu kwa wasiozingatia kanuni.
Ndugai aliyekuwa nje ya nchi kwa mwezi mmoja akitembelea Nigeria, Dubai na

RAIS MAGUFULI ATAKA WALA RUSHWA WAFUNGWE.

Rais Magufuli, amesema anataka walarushwa wengi wafungwe licha ya kuwa kuna baadhi ya watu hawataki kusikia kauli hiyo.
Hayo aliyasema jana Ikulu Dar es Salaam baada ya kumwapisha Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Brigedia Jenerali John Mbungo.
Alisema wakifungwa walarushwa nchi haitakuwa na rushwa kwani  ndio

Thursday, August 24, 2017

WATU WAALIKWA KATIKA IBADA YA CHUO CHA MANABII NGURUMO YA UPAKO

Kadinali wa pili wa huduma ya ngurumo ya upako Mchungaji Elizabeth Humphrey amewaalika watu wote kuhudhuria ibada ya chu cha manabii inayofanyika hii leo katika hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo Arusha.
Akizungumza na N.Y.U Radio ofisini kwake Mchungaji Elizabeth Humphrey amesema kuwa ni vyema kila mmoja kushiriki ibada ili kuendelea kujaa neno la mungu kutoka kwa watumishi wa mungu wanaotumika chini ya nabii mkuu Mh

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO Jumatano,August23,2017.


Tuesday, August 22, 2017

WATU WAALIKWA KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII.

Kadinali wa pili wa huduma ya Ngurumo ya Upako mchungaji Elizabeth Humphrey amewaalika watu kuhudhuria ibada ya chuo cha manabii inayofanyika hii leo katika hema la kukutania kisongo Arusha.

Akizungumza na N.Y.U Radio Ofisini kwake Mchungaji Elizabeth Humphrey

NABII MKUU MH DK. GEORDAVIE ATOA WITO KWA WAKAZI WA KISONGO.

Wito umetolewa kwa wakazi wa kisongo Mkoani Arusha  kujenga hotel  za kisasa sawasawa na neno la kinabii ya kuwa mara baada ya GeorDavie Tv kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja wageni kutoka mataifa mbalimbali watakuja kushiriki ibada pamoja na kujifunza mafundisho yanayotolewa  na Nabii mkuu Mh. Dk GeorDavie.

Hayo yamesemwa na Nabii Mkuu Mh Dk. GeorDavie katika kipindi cha kusapoti

SERIKALI KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUDHIBITI AJALI BARABARANI.

Serikali imetoa mwezi mmoja kwa Mamlaka zinazohusika na masuala ya usalama barabarani kuhakikisha zinakamilisha uboreshaji wa mfumo wa kielektroniki wa uwekaji wa vifaa vya kufuatilia udhibiti mwendo barabarani ikiwa lengo ni kushughulikia matatizo ya kiusalama barabarani kupitia vyombo vya usafiri.
Akizungumza hayo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AMBAKA MWANAFUNZI NA KUMSABABSHIA UJAUZITO.

Mwalimu wa shule ya msingi katika kata ya Ligunga tarafa ya Matemanga wilaya Tunduru mkoani Ruvuma Rajabu Morisi amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake na kumsababishia ujauzito.
 

IGP SIRRO AZUNGUMZIA SAKATA LA MIILI YA WATU KUKUTWA KWENYE VIROBA KATIKA FUKWE ZA BAHARI YA HINDI.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amezungumzia suala la kuokotwa miili ya watu kwenye viroba katika fukwe za bahari ya Hindi, na kusema suala hilo tayari lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.



Sirro amesema kweli taarifa hizo zimelifikia Jeshi la Polisi, na kwamba tayari miili ipo

IBADA LIVE YA CHUO CHA MANABII.

Sikiliza ibada ya chuo cha manabii moja kwa moja kupitia N.Y.U RADIO 99.3 na kupiti www.nyufmradio.radio12345.com
 NGURUMO YA UPAKO .

MAJENGO 22 YA ZAHANATI YAKOSA WATUMISHI NA VIFAA TIBA MBEYA.

Majengo 22 yaliyojengwa na wananchi kwa makusudi ya kutumika kama zahanati katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa miaka minne sasa, hayatumika kwa kukosa watumishi na vifaa tiba.
Responsive image

Monday, August 21, 2017

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO. Jumanne, August22,2017.


Rais Buhari asisitiza umoja hotuba ya kwanza baada ya kurejea Nigeria

Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameihutubia taifa baada ya kuwa Uingereza kwa miezi mitatu akipata matibabu.

Jenerali wa Jeshi Ateuliwa na Rais Magufuli Kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU

Raisi John Magufuli leo August 21, 2017 amemteua Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Madereva Daladala Kituo cha Simu 2000 Wagoma


Baadhi ya madereva wa daladala zinazotumia kituo cha mabasi cha Simu-2000 Mawasiliano kuongezewa ushuru kutoka Sh 500 hadi 1000 wakati wa kutoka ndiyo sababu mojawapo iliyofanya wagome.

Rais Magufuli Akutana Na Rais Wa Shirika La Kimataifa La Maendeleo La Japan (Jica) Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 21 Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA),Bwana Shinichi Kitaoka Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Friday, August 18, 2017

MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI AFRIKA KUSINI KUMUWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA 37 WA SADC.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika ya Kusini tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC unaoaanza tarehe 19 na 20 ambapo kesho tarehe 18 atahudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit).


POLISI WATIBUA JARIBIO LA PILI LA SHAMBULIZI UHISPANIA.

Maafisa wa polisi wa Uhispania wanasema kuwa wamewaua watu watano katika mji wa Cambrils ili kuzuia jaribio la pili la shambulio baada ya shambulio la hapo awali kufanyika mjini Barcelona.
Washambuliaji walikuwa wamevalia vilipuzi , polisi wamesema.
Watu 13 walifariki huku makumi wakijeruhiwa baada ya gari dogo kuingia katika eneo la watu mjini Barcelona eneo la Las Ramblas siku ya alhamisi mchana
Polisi watibua jaribio la pili la shambulizi mjini Cambrils Uhispania

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO Ijumaa, August18, 2017.


Thursday, August 17, 2017

AKAMATWA NA POLISI KWA KUMPAKA MWANAE KINYESI.

Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumfanyia ukatili mtoto wake wa kumpaka mavi ya mbuzi kwenye majeraha aliyoungua na  moto wilayani Nyamagana.
 
Kwamba tarehe 15.08.2017 majira ya saa 16:30hrs jioni katika Mtaa wa Chakechake – Mkuyuni Wilaya ya Nyamagana Jiji na Mkoa wa Mwanza, Sospeter Rajabu miaka 42, mvuvi na mkazi wa mtaa wa Chakechake – Mkuyuni, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumfanyia ukatili mtoto wake aitwaye Neema Sospeter miaka 10, mwanafunzi wa darasa la kwanza, kwa kumpaka mavi ya mbuzi kwenye majeraha ya moto aliyoungua maeneo ya mapaja ya miguu yote miwili kwa muda wa wiki mbili na kupelekea majeruhi kuwa na hali mbaya kiafya, kitendo ambacho ni kinyume na sheria.

MAPOROMOKO YASITISHA MAISHA YA WENGI NCHINI SIERRA LEONE.

Zaidi ya watu 500 wametoweka kufuatia maporomoko ya matope na mafuriko kwa mujibu wa msemaji wa Rais maporomoko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Free town nchini Sierra Leone.
Responsive image

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO. Alhamisi, August 17, 2017.


KAMA ULIKOSA KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII SIKU YA JUMAMOSI HIVI NDIVYO ILIKUWA .
AMBAPO MCHUNGAJI ANNA SALANJE WA HUDUMA YA NGURUMO YA UPAKO PAMOJA NA MCHUNGAJI LAMECK PALANJO. 
WALIWEZA KUHUBIRI KATIKA IBADA HIYO.
 

SERIKALI KUKUTANA NA WAWEKEZAJI WA VIWANDA ILIVYOTANGAZA NIA YA KUVITWAA SABABU YA KUSUASUA KATIKA UZALISHAJI.





Wednesday, August 16, 2017

MTOTO MCHANGA WA MIEZI 6 ALIYEJERUHIWA NA POLISI AFARIKI DUNIA.

Mtoto wa miezi sita aliyejeruhiwa na maafisa wa polisi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yaliozua utata nchini Kenya amefariki, kulingana na familia yake.

Samantha Pendo alikuwa mahututi tangu siku ya Ijumaa baada ya kupata majeraha ya kichwa wakati polisi walipovamia nyumba yao katika mtaa wa mabanda magharibi mwa mji wa Kisumu.
 
Babake Joseph Abanja , ameliambia gazeti la Daily Nation: "Nataka haki kwa

MARUFUKU BODABODA KUBEBA WANAFUNZI NA WATOTO CHINI YA MIAKA 10 .

Jeshi la Polisi  August 15, 2017 limetoa tamko la kupiga marufuku Waendesha Bodaboda kubeba watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 na kwamba atakayekiuka agizo hilo pamoja na mzazi aliyeruhusu mwanawe kubebwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na faini, kifungo au vyote viwili.