Showing posts with label HABARI ZA MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA MICHEZO. Show all posts

Monday, July 27, 2026

MOROCCO, ALGERIA ZAANZA VIZURI WAFCON


Timu za Taifa za soka za wanawake za Morocco na Algeria zimeanza vyema kampeni zao za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 kwa kuibuka na ushindi katika michezo yao ya kwanza ya hatua ya makundi.

Wenyeji Morocco wameonyesha ubora kwa kuichapa Kenya (Harambee Starlets) mabao 4-0 katika mchezo wa Kundi A, huku Algeria ikiifunga Senegal mabao 2-0 na kuanza michuano hiyo kwa pointi tatu muhimu.

Michuano hiyo inaendelea leo ambapo Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, itashuka dimbani kuivaa Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi B utakaochezwa saa 2:00 usiku.

 


Thursday, July 23, 2026

MALI, NIGER NA BURKINA FASO ZATAFUTA KUANDAA AFCON 2032


Mali, Niger na Burkina Faso, nchi tatu zinazoongozwa na serikali za kijeshi zinawania kwa pamoja kuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2032.

Shirikisho la Soka la Mali lilisema katika taarifa kwamba maafisa wake walikutana na rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, Jumamosi mjini New York, "kwa lengo la kuandaa zabuni ya pamoja ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2032."



Nchi hizo tatu jirani, ambazo pia ni washirika ndani ya Muungano wa Nchi za Sahel (Alliance of Sahel States - AES), zinaongozwa na tawala za kijeshi zilizochukua madaraka kupitia mapinduzi.

Aidha, zinakabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama kutokana na mashambulizi ya makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali, ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu.


Thursday, July 16, 2026

FIFA KUANGALIA UWEZEKANO WA KUIADHIBU ARGENTINA

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) linachunguza uwezekano wa kuichukulia hatua za kinidhamu timu ya taifa ya Argentina, baada ya wachezaji wake kuinua bango lenye ujumbe wa kisiasa kuhusu Visiwa vya Falkland.

Tukio hilo lilitokea Jumatano usiku mara baada ya Argentina kuifunga England mabao mawili kwa moja katika nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Wachezaji wa Argentina walisherehekea ushindi huo kwa kubeba bango lililoandikwa "Visiwa vya Falkland ni vya Argentina."

Serikali ya Uingereza, kupitia ofisi ya Waziri Mkuu, imeunga mkono wito wa kutaka FIFA ichukue hatua kali dhidi ya mabingwa hao watetezi. Visiwa vya Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza tangu vita vya mwaka 1982, na wananchi wake walipiga kura mwaka 2013 kusalia chini ya Uingereza.

Sheria za FIFA zinakataza vikali ujumbe wa kisiasa uwanjani, na tayari Argentina ilishawahi kupigwa faini kwa kosa kama hili mwaka 2024.

Wednesday, July 8, 2026

MANCHESTER UNITED YAANGUKIA KWA ANDREY SANTOS BAADA YA KUMKOSA MATEUS FERNANDES


Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na Chelsea juu ya kumsajili kiungo, Andrey Santos kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 56 pamoja na nyongeza ya Euro milioni 2.4 huku Chelsea akipachika kifungu cha asilimia 10 za mauzo ya siku za usoni.

Santos 22, raia wa Brazil tayari amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na mashetani hao Wekundu na tayari amepata ruhusa ya kufanya vipimo vya afya kabla ya kukamilika uhamisho huo.

Mashetani hao Wekundu ambao pia wanatarajiwa kumtangaza, Mbrazil mwingine, Ederson kama mchezaji mpya walilazimika kutafuta kiungo mwingine kwa ajili ya kurithi mikoba ya Casemiro ikiwa ni baada ya kuangukia pua katika jitihada zao za kuinasa saini ya Mateus Fernandes aliyetimkia Tottenham Hotspur.

Monday, July 6, 2026

HUENDA WACHEZAJI HAWA TUSIWAONE FANALI ZA WORLD CUP 2030

Hizi ni Picha za Ma-legendi kutoka Mataifa mbali mbali yaliyoshiriki kombe la Dunia 2026 Huko Mexico, Marekani na Canada na tayari wameshaondolewa

Christiano Ronaldo Mwenye Miaka 41 Ureno 

Luca Modric Mwenye Miaka 40 Croatia 

Manuel Neur Mwenye Miaka 40 Ujerumani 

Neymar Santos Jr Miaka 34 Brazil 

Ma-legendi hawa wote huenda tusiwaone katika Kombe la Dunia 2030 kwani tayari baadhi yao wametangaza kustafu soka la kimataifa wakiwa timu na zao za taifa

Tizama wanavyohuzunika



RAIS DKT. SAMIA AMTEMBELEA PACOME HOSPITALINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtembelea kiungo wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Pacome alilazwa hospitalini baada ya kupata majeraha ya mguu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, ambapo Yanga SC ilicheza dhidi ya JKT Tanzania. Tukio hilo lilitokea Juni 30, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.



RONALDO NA URENO YAKE YAONDOLEWA KOMBE LA DUNIA NA UHISPANIA

Cristiano na na wenzake wa Ureno wameaga mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 kufuatia kipigo cha 1-0 dhidi ya Uhispania kwenye hatua ya 16 bora katika dimba la Dallas, Texas Marekani.
Uhispania imetinga hatua ya robo fainali na itachuana na mshindi wa mchezo mwingine wa hatua ya 16 bora kati ya wenyeji, Marekani dhidi ya Ubelgiji.
FT: Portugal 🇵🇹 0-1 🇪🇸 Spain
⚽ 90+1 Merino.





WENYEJI MAREKANI WATUPWA NJE WORLD CUP, UBELGIJI IKIIFUATA HISPANIA ROBO FAINALI


Timu ya Taifa ya Ubelgiji ‘The Red Devils’ imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji wenza wa michuano hiyo, Marekani katika dimba la Seattle, Washington kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.

Ubelgiji itachuana na Uhispania kwenye hatua ya robo fainali, Uhispania ikitinga hatua baada ya kuisukumiza nje Ureno kwenye hatua ya 16 bora.




Wednesday, July 3, 2019

RASMI IBRAHIM AJIBU MIGOMBA AMEREJEA SIMBA SC KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI



KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Ajibu Migomba amesaini mkataba wa miaka miwili kurejea klabu yake ya zamani, Simba SC kutoka kwa mahasimu, Yanga SC.

Hizi hapa Timu 16 zilizotinga hatua ya 16 bora AFCON 2019 Pamoja na Ratiba


Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kupoeza mechi zake zote kwenye kundi C michuano ya Afcon zilizotinga hatua ya 18 hizi hapa na ratiba yake ipo namna hii:-

Sunday, June 23, 2019

Taifa Stars kushuka dimbani leo dhidi ya Senegal .....Mchezo Utapigwa Saa Mbili Usiku


Timu yetu ya Tanzania, Stars  leo Jumapili June 23  itachuana na Senegal katika mchezo wa Fainali za Afcon, mechi itakayopigwa saa 2 usiku kwa saa za nyumbani (Tanzania).

Thursday, June 13, 2019

Kocha Amunike Apitisha Rungu Taifa Stars Misri....Mastaa 9 Watemwa


BENCHI la Ufundi la Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) likiongozwa na Kocha Mkuu, Emmanul Amunike, raia wa Nigeria limefanya mchujo wa kikosi cha wachezaji watakaoshiriki michuano ya AFCON2019 nchini Misri kutoka achezaji 32 hadi achezaji 23 huku wachezaji 9 wakitemwa.

Tuesday, June 11, 2019

Kenya na Uganda wametangaza vikosi vyao kamili vya AFCON 2019

Timu ya taifa ya Kenya na Uganda kwa pamoja wote leo wamefanikiwa kutangaza vikosi vyao vya wachezaji 23 vitakavyoshiriki fainali za mataifa ya Afrika 2019 nchini Misri, Kenya wametangaza kikosi hicho ikiwa ni siku moja

Saturday, October 13, 2018

Taifa Stars Yapigwa 3-0 Na Cape Verde

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'  jana usiku kimekubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Cape Verde  na sasa kitalazimika kuanza kupiga mahesabu ya mataifa yaliyopo kundi L ili kuona kama kinaweza kufuzu fainali za AFCON 2019 nchini Cameroon.

Tuesday, June 12, 2018

Saturday, June 9, 2018

KARIA AWAPA YANGA SAA 48 KUTENGUA KAULI YA KUJITOA KOMBE LA KAGAME, VINGINEVYO…



RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameutaka uongozi wa klabu ya Yanga kutoa jibu linaloeleweka hadi kufika Jumapili juu ya kujitoa kwao kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Kauli hiyo ya Karia leo, inafuatia Yanga kuiandikia barua TFF kuwaarifu kutoshiriki michuano hiyo kutokana na kubanwa na ratiba ya mashindano mengine.

Wednesday, May 23, 2018

Rwanda kushirikiana na Arsenal kuimarisha utalii

Arsenal kutangaza utalii wa Rwanda




Rwanda imetangaza mpango wa ushirikiano na timu ya Arsenal inayocheza ligi kuu ya England.Ushirikiano huo wa miaka 3 unalenga kuimarisha sekta ya utalii nchini Rwanda,uwekezaji na maendeleo ya mchezo wa soka.

Saturday, May 12, 2018

KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA SINGIDA UNITED LEO


simba_1wg9iatlvvie114248gh77zh68
Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Singida United, mchezo wa Ligi Kuu Bara

WAAMUZI WAWILI WAONDOLEWA KUCHEZESHA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KWA MCHEZO MCHAFU


Nembo-ya-TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limewaondoa Waamuzi wawili kwenye orodha ya Waamuzi wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inayoendelea kwenye vituo vinne vya Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro.

Friday, May 4, 2018

Atletico Madrid 1-0 Arsenal: Diego Costa afunga na kuwazuia Gunners kufika fainali Europa League

Diego Costa 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alipoteza fursa pekee ya kushinda kombe msimu wake wa mwisho akiwa katika klabu hiyo baada ya kuchapwa na Atletico Madrid katika nusu fainali ya ligi ndogo ya klabu Ulaya Europa League.