Thursday, July 16, 2026

FIFA KUANGALIA UWEZEKANO WA KUIADHIBU ARGENTINA

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) linachunguza uwezekano wa kuichukulia hatua za kinidhamu timu ya taifa ya Argentina, baada ya wachezaji wake kuinua bango lenye ujumbe wa kisiasa kuhusu Visiwa vya Falkland.

Tukio hilo lilitokea Jumatano usiku mara baada ya Argentina kuifunga England mabao mawili kwa moja katika nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Wachezaji wa Argentina walisherehekea ushindi huo kwa kubeba bango lililoandikwa "Visiwa vya Falkland ni vya Argentina."

Serikali ya Uingereza, kupitia ofisi ya Waziri Mkuu, imeunga mkono wito wa kutaka FIFA ichukue hatua kali dhidi ya mabingwa hao watetezi. Visiwa vya Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza tangu vita vya mwaka 1982, na wananchi wake walipiga kura mwaka 2013 kusalia chini ya Uingereza.

Sheria za FIFA zinakataza vikali ujumbe wa kisiasa uwanjani, na tayari Argentina ilishawahi kupigwa faini kwa kosa kama hili mwaka 2024.

No comments:

Post a Comment