Showing posts with label HABARI ZA KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA KIMATAIFA. Show all posts

Tuesday, July 28, 2026

DAGLO ASEMA WAPIGANAJI WAKE "HURU SASA" KUPAMBANA NA JESHI

Mkuu wa wanamgambo wa RSF nchini Sudan Mohamed Hamdan Daglo amewaambia wapiganaji wake kuwa "wameachiliwa huru" sasa kupambana na jeshi la nchi hiyo.

Ujumbe huu wa Daglo kwa wapiganaji wake ambao wametuhumiwa kwa mauaji ya kimbari unakuja siku moja baada ya kupoteza udhibiti wa barabara moja kuu kati ya Mji Mkuu Khartoum na mji mkubwa wa eneo la Kordofan wa El-Obeid.

Kwa wiki kadhaa sasa Umoja wa Mataifa umeonya kuwa huenda wapiganaji wa RSF wakasababisha mauaji makubwa katika eneo la Kordofan, wakati wanapotafuta kuuzingira mji wa El-Obeid kuelekea uvamizi mkubwa wanaotazamia kuufanya.

Wafanyakazi wa misaada ya kiutu wanakadiria kuwa tangu Aprili 2023, vita kati ya wapiganaji wa Daglo na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan vimesababisha vifo vya zaidi ya watu laki mbili na kusababisha mgogoro mkubwa zaidi duniani wa njaa na raia kuyakimbia makaazi yao.

 

Chanzo: DW


UNAIDS: DUNIA IKO HATARINI KWA MLIPUKO MWENGINE WA UKIMWI



Umoja wa Mataifa unasema kuna dunia iko kwenye hatari ya kuzuka tena kwa mlipuko wa virusi vya ukimwi.

Shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI UNAIDS limesema hii ni kutokana na ufadhili duniani kupungua pakubwa mwaka jana.

Katika ripoti yake ya kurasa 60 iliyozinduliwa huko Brazil kuelekea kuanza kwa Kongamano la Kimataifa la UKIMWI, Umoja wa Mataifa unasema jamii ya kimataifa imeingia katika enzi za siasa na ubanaji wa fedha mambo yanayotishia kuharibu mazuri yote yaliyopatikana kwa miongo kadhaa katika vita dhidi ya virusi hivyo.

Shirika la UNAIDS linasema ufadhili ulipungua kwa asilimia 18 mwaka 2025 hadi dola bilioni 7.3 hicho kikiwa kiwango cha chini zaidi katika karibu miongo miwili.

Kabla kuingia madarakani kwa Donald Trump, Marekani ndiyo iliyokuwa mfadhili mkuu ikichangia asilimia 75 ya ufadhili jumla wa dunia.

Chanzo: DW


Monday, July 27, 2026

MAAMBUKIZI YA EBOLA YAPINDUKIA 3,000 KONGO

 


Haya yanafanyika wakati ambapo maambukizi yameripotiwa kuongezeka kwa karibu 1,000 katika kipindi cha siku kumi tu.

Takwimu rasmi zinaonesha kuwa jumla ya visa 3,075 sasa vimethibitishwa katika mikoa mitano baada ya mlipuko huo wa Ebola kuvuka maambukizi 2,000 mnamo Julai 15.

Mamlaka zinasema ugunduzi wa maambukizi na juhudi za kupima zimechangia katika kugundua maambukizi zaidi.

Mlipuko huo uliotangazwa mnamo Mei 15, unasababishwa na aina ya kirusi cha Bundibugyo ambacho bado hakijapata chanjo au tiba.

Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, karibu asilimia 90 ya visa vimeripotiwa katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Ituri, ambao unapakana na Sudan Kusini na Uganda.

Mlipuko huo huenda ukadumu kwa miezi kadhaa zaidi kutokana na mgomo wa wahudumu wa afya wanaolalamikia kutolipwa mishara yao na kutatiza utoaji huduma katika baadhi ya hospitali.

Thursday, July 23, 2026

MALI, NIGER NA BURKINA FASO ZATAFUTA KUANDAA AFCON 2032


Mali, Niger na Burkina Faso, nchi tatu zinazoongozwa na serikali za kijeshi zinawania kwa pamoja kuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2032.

Shirikisho la Soka la Mali lilisema katika taarifa kwamba maafisa wake walikutana na rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe, Jumamosi mjini New York, "kwa lengo la kuandaa zabuni ya pamoja ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2032."



Nchi hizo tatu jirani, ambazo pia ni washirika ndani ya Muungano wa Nchi za Sahel (Alliance of Sahel States - AES), zinaongozwa na tawala za kijeshi zilizochukua madaraka kupitia mapinduzi.

Aidha, zinakabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama kutokana na mashambulizi ya makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali, ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu.


Wednesday, July 8, 2026

MAREKANI YAANZISHA UPYA MASHAMBULIZI NCHINI IRAN


Marekani imefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya Iran mapema leo, hatua iliyojibiwa na Iran kwa kuyalenga mataifa ya Bahrain, Kuwait na Qatar. Hali hii inaongeza mvutano na kuhatarisha tena makubaliano ya muda yaliyolenga kutafuta njia ya kumaliza vita.

Jeshi la Marekani lilishambulia maeneo mbalimbali ya kijeshi na miundombinu ya bandari mapema Jumatano, kufuatia mashambulizi ya Iran dhidi ya meli kadhaa za biashara katika pwani ya Oman, hali iliyosababisha Iran kujibu kwa mashambulizi mengine.

Mashambulizi ya Marekani yalifanywa saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema makubaliano hayo yamefika mwisho kufuatia mashambulizi hayo ya Iran.

Hata hivyo, mashambulizi ya Alhamisi yalionekana kuwa makubwa zaidi kuliko ya awali huku Jeshi la Kuwait likisema limezuia na kudungua droni pamoja na makombora yaliyoelekezwa nchini humo.

Vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliripoti milipuko katika maeneo kadhaa, yakiwemo Bushehr, ambako kuna kituo cha nishati ya nyuklia cha Iran, pamoja na miji ya bandari ya kusini ya Chabahar, Konarak, Bandar Abbas na Sirik.

Chanzo: DW

WAIRAN KUMZIKA AYATOLLAH ALI KHAMENEI NYUMBANI KWAKE MASSHAD

Raia nchini Iran hii leo wanajiandaa kumzika kiongozi wao Ali Khamenei, katika mji alikozaliwa wa Mashhad, huku mashambulizi mapya ya Marekani yakitishia kusababisha ongezeko jipya la mvutano.

Mazishi ya kiongozi huyo mkuu wa zamani yanafuatia ibada za maombolezo zilizodumu kwa siku kadhaa na kuhudhuriwa na mamilioni ya waombolezaji katika miji mbalimbali nchini Iran na Iraq.

Ali Khamenei aliuawa Februari 28, siku ya kwanza ya mashambulizi ya Marekani na Israel nchini Iran yaliyochochea vita hivyo.

Baada ya maandamano makubwa ya mazishi yaliyopita katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq siku ya Jumatano, mwili wake ulitarajiwa kufikishwa katika makazi yake ya mwisho katika mji mtakatifu wa Mashhad.

Gavana wa Mashhad, Hassan Hosseini alinukuliwa na televisheni ya serikali akisema kuwa "anatarajia watu milioni 15” kuhudhuria mazishi hayo ya Khamenei.

Chanzo: DW


Monday, July 22, 2019

Filamu ya ‘The Lion King’ imeingia kwenye rekodi hii ya mauzoSHARE


Leo July 22,2019 filamu ya The Lion King imechukua headlines baada ya kutajwa kuwa mpaka sasa imefanikiwa kuingiza kiasi cha zaidi ya shilingi Trilioni 1 za Kitanzania duniani kote tokea iachiwe rasmi July 19,2019.

Tuesday, July 9, 2019

Ambassador 'has PM's full support' despite Trump criticism

Composite image of President Trump and Sir Kim Darroch

Downing Street has reaffirmed its "full support" for the UK's ambassador to the US after Donald Trump said he will no longer work with him.

Sunday, June 23, 2019

Wakala wa CIA anyongwa nchini Iran


Taarifa iliyotolewa na mahakama ya kijeshi nchini Iran inasema adhabu ya kunyongwa hadi kufa aliyopewa jasusi wa CIA na Marekani,Jalal Haji Zevar imetekelezwa katika gereza la Recai Shar lililopo kerec kaskazini magharibi mwa Tehran.

Iran yaionya Marekani na njama zake za kutaka kuishambulia kijeshi nchi hiyo


Image result for IRAN VS MAREKANI
Msemaji wa makao makuu ya jeshi la Iran, Meja Jenerali Ebulfazl Shikarchi amesema shambulizi lolote la kijeshi kutoka kwa Marekani litajibiwa vikali kwa wao kushambulia maslahi ya Marekani katika eneo hilo pamoja na kushambulia washirika wa Marekani.

Sunday, June 16, 2019

Hong Kong protest: 'Nearly two million' join demonstration

The street can no longer be seen beneath the heaving crowd in this shot of a light rail station, the ring and arches of its architecture visible above them


Nearly two million people have taken part in a mass protest in Hong Kong against a controversial extradition bill, organisers say.

Friday, June 14, 2019

Shambulizi la meli ya mafuta katika Ghuba: Iran yasema madai ya Marekani hayana msingi


Iran imesema kuwa imepuuzilia mbali madai ya Marekani kwamba ndio iliotekeleza shambulio dhidi ya meli mbili za mafuta katka Ghuba ya Oman.

Uturuki kulipiza kisasi ikiwekewa vikwazo na Marekani


Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amesema nchi yake italipiza kisasi dhidi ya uwezekano wowote ule wa Marekani kuiwekea vikwazo nchi yake kutokana na makubaliano yake na Urusi ya kununua mfumo wa kukinga makombora aina ya S-400. 

Thursday, June 13, 2019

Uturuki Kupokea ngao ya makombora ya S-400 ya Urusi Mwezi Ujao


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema serikali yake tayari imenunua mtambo wa kujikinga na makombora kutoka Urusi. 

Iran Yatupiwa Lawama baada ya Wahouthi wa Yemen kuushambulia uwanja wa ndege Saudia


Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umeapa kujibu vikali shambulizi la kombora lililofanywa jana na wapiganaji wa Houthi nchini Yemen kwenye uwanja wa kiraia wa ndege kusini mwa Saudia na kuwajeruhi watu 23.

Tuesday, June 11, 2019

Ivan Golunov, accused Russian reporter, to go free after outcry

Russian investigative journalist Ivan Golunov, who was detained by police and accused of drug offences, reacts inside a defendants" cage as he attends a court hearing in Moscow, Russia June 8, 2019.


All charges against Russian reporter Ivan Golunov have been dropped, after a huge public outcry.
Mr Golunov, an investigative journalist, had been accused of drug dealing - but his lawyers said the drugs were planted by authorities.

Tuesday, June 12, 2018

Updates: Trump aridhika na mazungumzo pamoja na Kim, Wasaini Makubaliano Maalumu


Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamemaliza mazungumzo ya kwanza ya kihistoria kwa kutia saini taarifa juu ya ahadi za kuangamiza silaha za nuklia za Korea Kaskaizni.

Wednesday, May 30, 2018

Walioshtakiwa ulaji rushwa Kenya kukaa rumande wiki moja

Mkurugenzi Mkuu wa NYS Richard Ndubai akiwa mahakamani Jumanne 
Watuhumiwa 24 walioshtakiwa kuhusiana na kashfa ya ufujaji wa pesa katika Shirika la Vijana wa huduma kwa Taifa (NYS) watakaa rumande kwa wiki moja.

Wednesday, May 23, 2018

Friday, May 18, 2018

Korea Kaskazini na Marekani: Kwa nini Kim Jong-un anamuogopa Donald Trump

Kim Jong-un (L) talking with South Korea's President Moon Jae-in (R) before the inter-Korean summit at the Peace House building on the southern side of the truce village of Panmunjom on 27 April (picture released by North Korean state media)\
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa matamshi yanayokinzana na ya mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa, akisema mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia hauwezi kutumiwa nchini Korea Kaskazini.