Tuesday, July 28, 2026

UNAIDS: DUNIA IKO HATARINI KWA MLIPUKO MWENGINE WA UKIMWI



Umoja wa Mataifa unasema kuna dunia iko kwenye hatari ya kuzuka tena kwa mlipuko wa virusi vya ukimwi.

Shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI UNAIDS limesema hii ni kutokana na ufadhili duniani kupungua pakubwa mwaka jana.

Katika ripoti yake ya kurasa 60 iliyozinduliwa huko Brazil kuelekea kuanza kwa Kongamano la Kimataifa la UKIMWI, Umoja wa Mataifa unasema jamii ya kimataifa imeingia katika enzi za siasa na ubanaji wa fedha mambo yanayotishia kuharibu mazuri yote yaliyopatikana kwa miongo kadhaa katika vita dhidi ya virusi hivyo.

Shirika la UNAIDS linasema ufadhili ulipungua kwa asilimia 18 mwaka 2025 hadi dola bilioni 7.3 hicho kikiwa kiwango cha chini zaidi katika karibu miongo miwili.

Kabla kuingia madarakani kwa Donald Trump, Marekani ndiyo iliyokuwa mfadhili mkuu ikichangia asilimia 75 ya ufadhili jumla wa dunia.

Chanzo: DW


No comments:

Post a Comment