Mkuu wa
wanamgambo wa RSF nchini Sudan Mohamed Hamdan Daglo amewaambia wapiganaji wake
kuwa "wameachiliwa huru" sasa kupambana na jeshi la nchi hiyo.
Ujumbe huu wa
Daglo kwa wapiganaji wake ambao wametuhumiwa kwa mauaji ya kimbari unakuja siku
moja baada ya kupoteza udhibiti wa barabara moja kuu kati ya Mji Mkuu Khartoum
na mji mkubwa wa eneo la Kordofan wa El-Obeid.
Kwa wiki
kadhaa sasa Umoja wa Mataifa umeonya kuwa huenda wapiganaji wa RSF
wakasababisha mauaji makubwa katika eneo la Kordofan, wakati wanapotafuta
kuuzingira mji wa El-Obeid kuelekea uvamizi mkubwa wanaotazamia kuufanya.
Wafanyakazi wa
misaada ya kiutu wanakadiria kuwa tangu Aprili 2023, vita kati ya wapiganaji wa
Daglo na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan vimesababisha vifo vya zaidi ya
watu laki mbili na kusababisha mgogoro mkubwa zaidi duniani wa njaa na raia
kuyakimbia makaazi yao.
Chanzo: DW

No comments:
Post a Comment