Mali, Niger na Burkina Faso, nchi tatu zinazoongozwa na
serikali za kijeshi zinawania kwa pamoja kuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya
Afrika AFCON mwaka
2032.
Shirikisho la Soka la Mali lilisema katika taarifa kwamba
maafisa wake walikutana na rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice
Motsepe, Jumamosi mjini New York, "kwa lengo la kuandaa zabuni ya pamoja
ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2032."
Nchi hizo tatu jirani, ambazo pia ni washirika ndani ya Muungano wa
Nchi za Sahel (Alliance of Sahel States - AES), zinaongozwa na
tawala za kijeshi zilizochukua madaraka kupitia mapinduzi.
Aidha, zinakabiliwa na changamoto kubwa za kiusalama kutokana
na mashambulizi ya makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali, ambayo
yamesababisha vifo vya maelfu ya watu.


No comments:
Post a Comment