Hatua
hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo wenye uwezo
wa kuzalisha jumla ya megawati 50 na kuingizwa katika Gridi ya Taifa, jambo
lililoongeza uwezo na uthabiti wa gridi hiyo na kuimarisha upatikanaji wa umeme
katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza
katika hafla hiyo Julai 27, 2026, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi,
amesema sekta ya nishati ni mhimili wa maendeleo ya Taifa ambapo Serikali
inaendelea kufanya jitihada za kuongeza vyanzo mseto vya uzalishaji wa umeme
(Energy Mix) ili kuhakikisha Tanzania haitegemei chanzo kimoja pekee cha
uzalishaji wa umeme.

No comments:
Post a Comment