Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri mkuu, kazi, ajira na
mahusiano ya kazi Deusi Sangu amewaomba watumishi wa mungu waendelee
kudumisha umaadili, mshikamano na amani ya nchi.
Ameyasema hayo katika kongamano la kurejesha thamani, lililofanyika Mkoani Morogoro ambalo pia
lilikuwa na lengo la kuiombea nchi ambapo ameongeza kuwa serikali inawatambua
na kuwathamani watumishi wa mungu.
Amesema katika kuishi dhamira hiyo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani wakati akizindua bunge la
13 aliipa wizara yake jukumu la kuratibu mahusiano baina ya serikali na makundi
ya kijamii ambapo uratibu huo unahusisha wadau wa siasa, taasisi za dini, Asasi
za Kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali na kwamba wanafanya kazi na wadau
hao wote kwa karibu ili kuhakikisha wanaimarisha amani, utulivu upendo,
mshikamano na maridhiano ya kitaifa.
Amesema mambo hayo ndio nguzo kuu na mahusiano na dhamira ya
maendeleo ya taifa ya mwaka 2026.

No comments:
Post a Comment