Thursday, July 24, 2025

NABII MKUU MHE DKT. GEORDAVIE LEO AMETOA ZAWADI YA GARI AINA YA BMW KWA MWALIMU ISAYA BENSON.

Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie mchana wa Leo amemzawadia Mwalimu wa NENO la Mungu Isaya Benson Gari aina ya BMW X5 na shilingi milioni mbili kwa msikilizaji wa NYU FM RADIO kijana Makochali ambaye alizungumza jambo lililomgusa Nabii Mkuu.

‎‎Nabii Mkuu ametoa zawadi hizo mchana wa Leo kupitia kipindi cha zijue TABIA ZA MITUME NA MANABII kinachorushwa na NYU RADIO kila siku ya jumamosi kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saa Saba kamili mchana.

‎‎Akitoa zawadi hiyo ya gari kwa Mwalimu Isaya Nabii Mkuu amesema anampongeza kwa kazi nzuri anayofanya ikiwemo kipindi cha Maswali na Majibu, Tabia za Mitume na Manabii na kipindi cha Hazina katika Historia huku akimuelezea Mwalimu Isaya kuwa ni kijana mchapa kazi ,anayefanya tafiti mbalimbali na anaeleza kiustarabu.

‎‎Kwa upande wake Mwalimu Isaya Benson amemshukuru Nabii Mkuu kwa kumpandisha thamani kwa mara nyingine kwa kumpa BMW X5.

‎‎Aidha mpaka muda huu ambapo habari hii inakwenda hewani bado Nabii Mkuu anaendelea na zoezi la utoaji wa zawadi kwa wasikilizaji ambao wanapata nafasi ya kupiga simu studio za NYU RADIO na kuulizwa maswali kisha kuzawadiwa shilingi elfu hamsini(50) kwa kila mtu ambapo hadi sasa watu 10 tayari wamejipatia zawadi hizo.

‎Na Beatrice Maina @NYU ARUSHA. #GeorDavietv YouTube #GeorDavietv Instagram #GeorDavie Facebook #GeorDavie TikTok #GeorDavie Maarifa



No comments:

Post a Comment