Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie amewataka watu kuitambua Nguvu ya Nabii Mkuu na Lugha anayoitumia maana kuna tofauti kati ya Nabii na Nabii Mkuu.
Amesema unapomuona Nabii Mkuu umemuona Mtu mwenye Mamlaka katika Serikali Tukufu ya Ufalme wa Mungu na kwamba Neno lake analotamka ndilo linalokuwa.
Ameongeza kuwa Nabii Mkuu anapoingia ni Serikali Tukufu ya Ufalme wa Mungu imeingia na kwamba watu wakitambua jambo hilo lazima watafanikiwa kiroho na kimwili kwa kuyashika matamko ya kinabii.
Na Beatrice Maina@NYU ARUSHA.
No comments:
Post a Comment