Wednesday, September 30, 2026

NABII MKUU MHE. PROF. GEORDAVIE LEO HII KUSHIRIKI KONGAMANO LA 15 LA UMOJA WA MATAIFA ABU DHABI, FALME ZA KIARABU.

Nabii Mkuu Mhe. Prof. GeorDavie amepata mwaliko wa kushiriki katika Kongamano la 15 la Umoja wa Mataifa kuhusu Kuzuia Uhalifu na Haki Jinai, linalofanyika mjini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.

Kwa mujibu wa barua rasmi kutoka International Association of World Peace Advocates (IAWPA), Prof. GeorDavie amealikwa kushiriki katika kongamano hilo tarehe 1 Oktoba 2026.


Mwaliko huo unatokana na kutambua uongozi wake na dhamira yake katika kujenga amani, huku akiteuliwa kuwa miongoni mwa wazungumzaji katika kongamano hilo.

Kongamano hilo linawakutanisha wadau mbalimbali wa kimataifa kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu kuzuia uhalifu, haki jinai pamoja na juhudi za kukuza amani na usalama katika jamii na duniani kwa ujumla.

Katika ushiriki wake Prof. GeorDavie anatarajia kutoa mchango wake kupitia uzoefu na mtazamo wake katika masuala ya amani, umoja na maendeleo ya jamii, akiwa sehemu ya jukwaa hilo la kimataifa.

Ushiriki huo pia unaiweka Tanzania katika nafasi ya kuwakilishwa kwenye jukwaa la kimataifa linalojadili masuala muhimu yanayohusu amani, haki na usalama wa jamii.


No comments:

Post a Comment