Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amesema Upako alioubeba unaishi na wanaopokea upako huo wataubeba na kuupeleka mataifa mbalimbali duniani.
Ameyasema hayo novemba 01, 2026 wakati akiwapaka mafuta watumishi
kutoka mataifa mbalimbali waliofika katika ibada ya kimataifa ya chuo kikuu cha manabii
iliyofanyika katika nyumba ya matamko ngurumo ya upako ambapo ilikuwa ni ibada ya kusimamisha Nguzo Betheli ili kumjengea Bwana Madhabahu.
Akiwapaka mafuta watumishi hao Nabii Mkuu amesema Mungu
hajampa upako huo ili abaki nao hivyo kazi yake ni kuachilia upako huo kwa
watumishi wote waaminifu wa Yesu Kristo na waliotayari wataupokea na kufanya
mabadiliko makubwa kwa mataifa.








