HABARI ZA KIMATAIFA

Thursday,  17.8.2017

MAPOROMOKO YASITISHA MAISHA YA WENGI NCHINI SIERRA LEONE. 

Zaidi ya watu 500 wametoweka kufuatia maporomoko ya matope na mafuriko kwa mujibu wa msemaji wa Rais maporomoko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Free town nchini Sierra Leone.

Responsive image
Mapema Rais Ernest Bai Koroma aliomba usaidizi wa dharura  kwa kusema kwamba  jamii nzima ilikuwa imeangamia.
Siku ya Jumatatu takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki baada ya maporomoko ya matope katika eneo la Regent na mafuriko katika maeneo mengine mjini Freertown .
Shirika la msalaba mwekundu limeonya kuwa hakuna muda wa kutosha kuweza kuwaokoa manusura.  Mazishi ya pamoja ya waathiriwa yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano ili kupunguza idadi ya wafu katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Msemaji wa Rais Abdulai Baraytay aliambia BBC kwamba miili ilikuwa ikitolewa katika matope hayo na vifusi.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa kwamba wafanyakazi wake nchini Sierra Leone wamekuwa wakisaidia katika juhudi za kuwaokoa manusura.

Chanzo BBC Swahili.

 TUESDAY 15/08/2017

 KIM JONG-UN AKABIDHIWA MPANGO WA KUSHAMBULIA GUAM.

Kiongozi wa Korea Kaskazini amepokezwa habari kuhusu mpango wa taifa hilo wa kutaka kurusha kombora hadi katika kisiwa cha eneo la pacific cha Guam kinachomilikiwa na Marekani kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

Lakini ripoti hiyo imesema kuwa itachunguza vitendo vya Marekani kabla ya kuchukua hatua ya kurusha kombora hilo katika kisiwa cha Guam.

Wiki iliopita, Korea Kaskazini ilionya kwamba mikakati inawekwa kushambulia eneo ambalo ndege za kijeshi za Marekani zimekita kambi.


Kumekuwa na cheche za maneno kati ya Marekani na Korea kaskazini.

Ripoti hiyo ya kitengo cha habari cha KCNA ilisema kuwa Kim Jong un aliutazama mpango huo kwa muda mrefu na kuujadili na maafisa wakuu wa
jeshi.

Kamanda wa jeshi la kimkakati la Korea Kaskazini sasa anasubiri agizo baada ya kuandaa shambulio hilo la Guam.

Wanahewa wa Marekani wamepiga kambi katika kiswa cha Guam

Lakini ripoti hiyo pia imeongezea kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini atachunguza mienendo ya Marekani kabla ya kutoa uamuzi wowote, hatua inayoonekana kupunguza kasi ya cheche za maeneo kati ya mataifa hayo mawili.

Mwandishi wa BBC Yogita Limaye mjini Seoul anasema kuwa hatua hiyo itapunguza wasiwasi na kuzuia mgogoro wa kijeshi katika eneo la Korea.

Mwandishi mwengine ameongeza kuwa baada ya siku kadhaa za vitisho kutoka Pyongyang ,inaonekana kwamba rais Kim Jong Un sasa anataka kunyamaza na kutazama hali ,lakini katika taifa lenye siri kubwa kama Korea Kaskazini huwezi kuwa na hakika.

Kisiwa cha Guam

Wachanganuzi wanasema inamaanisha kwamba Pyongyang haiko tayari kutekeleza shambulio katika kisiwa cha Guam, kwa hivyo huenda inachukua muda.

Hatua hiyo inajiri baada ya waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis kuonya kwamba shambulio lolote linaweza kusababisha vita vikali, na iwapo Pyongyang itarusha kombora kuelekea Guam basi ''itakuwa vita''.

Ameambia maripota kwamba Jeshi la Marekani litatetea taifa hilo kutoka kwa shambulio lolote wakati wowote na kutoka kwa taifa lolote.

Pia aliwahakikisha raia wa Guam ,ambapo kuna kambi za kijeshi za Marekani kwamba takriban watu 160,000 wanalindwa na akasema iwapo kombora litarushwa ''tutalitibua''.

Chanzo BBC 

Minusma yalengwa na mashambulizi mawili mabaya

media 
 Gari ya kijeshi ya Minusma, Timbuktu, Septemba 19, 2016. SEBASTIEN RIEUSSEC / AFP

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali ililengwa na mashambulizi mawili siku ya Jumatatu Agosti 14. Shambulio la kwanza lilifanyika katikati mwa nchi, katika eneo la Douentza, shambulio la pili liliendeshwa kaskazini magharibi, katika mji wa Timbuktu.

Kaskazini magharibi mwa Mali, watu wanaoshukiwa kuwa magaidi (wanne hadi sita, kulingana na vyanzo mbali mbali) wakati mwengine walisafirishwa kwa gari. Watu hao waliokua walijihami kwa mabomu na silaha za kivita, walitembea kwa miguu kwenye maeno ambayo yalionekana ni vigumu kwa gari kutumia barabara. Baada ya kuwasili katika makao makuu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa katika mji wa Timbuktu,walianza kuwafyatulia risase walinzi wa usalama wa kampuni binafsi inayofanya kazi kwa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma). Walinzi sita wa usalama waliuawa.
Washambuliaji wawili walifaulu kuingia ndani ya kambi ya kikosi cha Umoja wa Mataifa (Minusma) kwa kutumia silaha zao. Hata hivyo waliuawa na vikosi vya Minusma. Inaarifiwa kuwa askari kadhaa wa kikosi hiki cha Umoja wa Mataifa walijeruhiwa, huku mmoja akiwa akiwa katia hali mbaya. Vikosi vya jeshi la Mali pia viliingilia kati na kuweza kuwaua magaidi wengine.
Watu wawili wauawa katika eneo la Mopti
Mapema siku ya Jumatatu, katikati mwa Mali, katika mji wa Douentza, makao makuu ya ya Umoja wa Mataifa nchini Mali, yalishambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi. Katika shambulio hilo askari mmoja wa Minusma na askari wa Mali waliuawa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mashambulizi hayo.
Matukio haya yanatokea siku moja baada ya mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Burkina Faso. Kwa kuonyesha mshikamano wake na wananchi wa Burkina Faso, Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta anazuru Jumanne hii mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Zuma: Kulikuwa na njama za kutaka kuniuwa


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini wikendi iliopita alizungumzia kuhusu jaribio la kumuua akisema kuwa aliwekewa sumu na karibu afariki kutokana na msimamo wake wa kiuchumi na marekebisho ya umiliki wa ardhi.
Niliwekewa sumu na ningefariki kwa sababu Afrika Kusini ilijiunga na Muungano wa Brics unaounganisha mataifa ya Brazil, Urusi, India, China na jamii ya kibiashara ya Afrika kusini chini ya uongozi wake.
''Walisema nilikuwa nina mpango wa kuharibu nchi'', alisema Zuyma.
Akihutubia mkutano wa wanachama wa ANC huko Phongolo, Kwa Zulu Natal siku ya Jumapili, rais huyo alisema kuwa alilengwa alipotaka kuweka kwa marekebisho makali ya kiuchumi.
Kulingana na ripoti hiyo kulikuwa na majaribio matatu ya kumuuwa.
Katika kanda hiyo hakusema ni nani aliyejaribu kumuua lakini anasema ni mtu wake wa karibu.

Rais Kabore na Macron walaani shambulizi la kigaidi jijini Ouagadougou

media  
Hali ilivyokuwa baada ya shambulizi la kigaidi jijini Ouagadougou Reuters

Rais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kabore amelaani shambulizi la kigaidi lilisababisha watu 18 kupoteza maisha jijini Ouagadougou.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron naye pia amelaani mauaji hayo ambayo pia yamesababisha raia mmoja wa Ufaransa kupoteza maisha.
Watu waliokuwa wamejihami kwa silaha walivamia Mkahawa unamilikiwa na raia wa Uturuki na kuanza kuwapiga risasi wateja.
Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha shambulizi hilo ambalo limezua hali ya wasiwasi jijini Ouagadougou.
Watu walioshuhudia shambulizi hili wamenukuliwa wakisema kwamba watu watatu waliokuwa na bunduki waliwafyatulia risasi wateja waliokuwa nje ya hoteli hiyo.
Kuna wasiwasi kwamba shambulio hilo huenda limetekelezwa na moja ya washirika wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda ambao bado wanaendesha shughuli zao katika eneo la Sahel.
Waziri wa mawasiliano wa Burkina Faso Remis Dandjinou amesema haijabainika ni washambuliaji wangapi hasa waliohusika.

 

 

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia akanusha mashtaka ya uhaini

media Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema (Aliyevaa fulana nyekundu) akifika Mahakamani Agosti 14 2017 https://twitter.com/upndzm?lang=en

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, amefikishwa Mahakamani jijini Lusaka, na kukanusha mashtaka ya uhaini.

Hichilema ambaye amekuwa akizuiliwa kwa miezi kadhaa sasa, amefunguliwa mashtaka kwa kuzuia msafara wa rais Edgar Lungu.
Kesi yake imeratibiwa kuendelea siku ya Jumatano wiki hii.
Tangu mwezi Aprili alipozuiliwa, mwanasiasa huyo ameendelea kudai kuwa alishinda Uchaguzi wa mwaka uliopita na kusisitiza kuwa mashtaka dhidi yake ni ya kisiasa.
Zambia imeendelea kuwa katika wasiwasi wa kisiasa tangu kuzuiliwa kwa Hichilema, na kusababisha rais Lungu kutangaza hali ya hatari nchini humo kwa kile alichokisema  ni kwa sababu za kiusalama.
Ikiwa atapatikana na kosa, kiongozi huyo wa upinzani atahukumiwa jela miaka 15 au hata kuhukumiwa kifo.
Rais Lungu amekanusha madai ya kumlenga kisiasa Hichilema.
Upinzani umeendelea kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wao, wito ambao pia umekuwa ukitolewa na viongozi wa Kanisa Katoliki nchini humo.



Polisi ya DRC yaonyesha wafuasi wa Bundu dia Kongo wanaotuhumiwa mauaji.
media Polisi wakizunguka miili ya wafuasi wa kundi la Bundu dia Kongo walioendesha mashambulizi siku ya Jumatatu, Agosti 7 mjini Kinshasa. JOHN WESSELS / AFP

Siku ya Jumatano, Agosti 9, mjini Kishasa, polisi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilionyesha wafuasi thelathini wa kundi la Bundu dia Kongo wanaoshtumiwa kuendesha mashambulizi siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Wanawake watatu ni miongoni mwa watuhumiwa hao. Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, washambuliaji walikua na nia ya kutoatangazo kwenye runinga ya taifa.
Watuhumiwa hao walisafirishwa na gari la polisi hadi kwenye makao makuu ya polisi, huku wakishindikizwa na kikosi kikubwa cha askari waliojihami kwa silaha za kivita. Wengi wao walikua walivaa vitambaa vyekundu kichwani. Na wengine walikua na beji zenye nembo ya kundi la bundu dia Kongo (BDK). Wote walikua miguu peku, huku nyele zao zikwa hivyo.
Msemaji wa polisi Kanali Ezéchiel Pierrot Rombaut Muanamputu alisema watu hao ni magaidi walioofanya mauaji katika mji mkuu wa DR COngo, Kinshasa siku ya Jumatatu Agosti 7, 2017.
Ameongeza kuwa watu hao ni wafuasi wa Ne Muanda Nsemi, kiongozi wa kiroho wa na kidini wa kundi la Bundu dia Kongo.
Wanawake watatu ambao walionyeshwa katika kundi hilo kama manabii wa kundi la Bundu dia Kongo. Mifuko miwili ya hirizi wa inayodaiwa kuwa ya kundi hilo ilioneshwa.
Vikosi vya usalama viliweza kudhibiti hali ya mabo na kurejesha utulivu kwa muda wa saa zisizozidi mbili, alisema Muanamputu Kanali.





Thursday, July 20, 2017 

SENETA JOHN MCCAIN APATIKANA NA SARATANI YA UBONGO.

Seneta wa chama cha Republican John McCain amepatikana na saratani ya ubongo na anatafuta matibabu kulingana na duru za offisi yake.
Matibabu hayo huenda yakashirikisha matumizi ya dawa ama mionzi kulingana na daktari wake.
Aliyekuwa mgombea wa urais nchini Marekani John McCain apatikana na saratani ya ubongo
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 80 yuko katika hali nzuri akiendelea kupata afueni nyumbani.
Uvumbe huo ulipatikana wakati wa upasuaji wa kuondoa damu ilioganda juu ya jicho lake la kushoto.
McCain ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita nchini Vietnam pia alitumikia miaka mitano jela.
Seneta huyo aliyehudumu kwa mihula sita na kuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican 2008 alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Phoenix katika jimbo la Arizona siku ya Ijumaa.
Uchunguzi wa tishu ulibaini kwamba uvimbe wa ubongo unaojulikana kama glioblastoma ulisababisha damu hiyo kuganda kulingana na taarifa ya kliniki hiyo ya Mayo.
Madaktari wa Seneta huyo wanasema kuwa anaendelea kupona kutoka kwa upasuaji huo na afya yake iko shwari, iliongezea.
Matibabu yake yatashirikisha utumiaji wa dawa na mionzi.
Glioblastoma ni uvimbe mbaya wa ubongo na huongezeka kutokana na umri wa mtu ukiwaathiri wanaume wengi zaidi ya wanawake.
Bwana McCain ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya sineti kuhusu hudumu za jeshi alikuwa katika hali nzuri huku akiendelea kupona nyumbani na familia yake, afisi yake ilisema.

MAREKANI NA CHINA ZAKOSA KUAFIKIANA KIBIASHARA

Marekani na China zimekamilisha mkutano wa kibiashara kuhusu maswala tata mjini Washington bila maafikiano.

Pande zote mbili hazikutoa taarifa ya pamoja ama hata mpango baada ya mkutano huo na kufutilia mbali mikutano na vyombo vya habari iliotarajiwa kufanyika.
 Meli ya mizigo ya China

Marekani ilikosoa biashara ya China na kutaka makubaliano ya kibiashara ambayo hayatapendelea upande mmoja.
Rais Donald Trump amesema kuwa ushuru kuhusu vyuma vya China bado huenda ukatekelezwa.
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo wa kibiashara kati ya mataifa ya China na Marekani, katibu wa biashara nchini Marekani Wilbur Ross aliikosoa biashara ya ziada ya China yenye thamani ya dola bilioni 347 akisema kuwa haitokani na mvutano wa kisoko.
Katika taarifa fupi, bi Ross na katibu katika wizara ya fedha Steven Mnuchin alitoa maelezo machache na ishara kuhusu hatua zilizopigwa kuhusu maswala tata.
''China ilitambua kwamba pendekezo letu la kupunguza tofauti ya kibiashara kati ya pande zote mbili litaafikiwa'', taarifa hiyo ilisema.
Swala tata la kodi itakayotozwa vyuma vya China lilitarajiwa kuwa mjadala mgumu katika mkutano huo, lakini pande zote mbili hazikutoa taarifa yoyote.
Marekani inalaumu biashara ya ziada ya vyuma vya China ambayo inaathiri wazalishaji wa Marekani na sasa imeonya kuweka kodi.
Kampuni za kuuza vyuma nchini Marekani hazikufanya biashara nzuri huku wawekezaji wakidhani kwamba Marekani huenda ikaitoza kodi China kwa biashara ya ziada ya vyuma vyao vinavyoingia Marekani.
Baada ya soko kufungwa, rais Trump aliwaambia maripota kwamba kodi ya vyuma inaweza kutekelezwa kulingana na chombo cha habari cha Reuters.



Jumatano,July19,2017

MAUAJI YA WACHUNGUZI WA UN, DRC

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema kuwa huenda wanajeshi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo au wapiganaji wa waasi nchini humo walihusika na mauaji ya wenzao wawili. 
Wapiganaji nchini DRC
Michael Sharp, raia wa Marekani na Zaida Catalan, mwenye uraia wa Uswizi na Chile waliuawa
Machi mwaka huu walipokuwa wakifanya utafiti kuhusu hali ya usalama nchini Congo.
Wachunguzi wanasema wenzao hao walipanga kukutana na kiongozi wa wanamgambo, siku moja kabla ya kuuawa.
Chanzo: BBC 
 Habari: Kimataifa

 

JUMANNE 18/07/2017  

Barafu inayoyeyuka nchini Uswisi imefichua miili miwili inayoaminiwa kuwa ya mtu na mkewe waliotoweka miaka 75 iliyopita. Marcelin na Francine Dumoulin walitoweka wakati walienda kuchunga ng'ombe wao katika milima ya Alps mwaka 1942.

The spot where the two bodies were found in glacier

Watu hao walikuwa na watoto saba.Mtoto wao wa mwisho wa kike ambaye sasa ana umri wa 79, anasema habari hizo zimemletea utulivu na anataka kuwafanyia maziko mema.
"Tulitumia maisha yetu yote kuwatafuta," alisema Marceline Udry-Dumoulin.
Uchunguzi wa DNA unatarajiwa kufanywa.
Polisi wanasema kuwa miili hiyo iligunduliwa wiki iliyopita katika eneo la Tsanfleuron na mfanyakazi kutoka kampuni ya kuteleza kwa barafu ya Glacier 3000.
Habari: Kimataifa

 

 TRUMP AIONYA VENEZUELA.



Rais wa Marekani Donald Trump amesema Venezuela itakabiliwa na hatua za kiuchumi iwapo itaendelea na mipango yake ya kutaka kuandika upya katiba ya nchi hiyo.


Kufuatia onyo hilo alilolitoa, Rais Trump pia ameupongeza upinzani nchini humo kutokana na kupigania kwake demokrasia na kumuelezea Rais Nicolas Maduro kama kiongozi mbaya ambaye anaota ndoto za kuwa dikteta.

Upinzani nchini Venezuela umetoa wito wa kufanyika mgomo wa siku moja nchi nzima siku ya Alhamisi kama sehemu ya kampeni zake kupinga uamuzi huo wa Rais Maduro kubadili katiba.


Siku ya Jumapili mamilioni ya Wavenezuela walijitokeza kupiga kura ya maoni isiyo rasmi kupinga pendekezo hilo, lakini hata hivyo serikali ya nchi hiyo, ikasema zoezi hilo la upigaji kura si halali.

  Habari: Kimataifa

JUMANNE 18/07/2017

JUHUDI ZA KUBADILISHA OBAMA CARE WAKWAMA.



Maseneta wengine wawili wa chama cha Republican wanasema kuwa wanapinga mpango wa chama chao, wa kuubadilisha muswada wa afya wa Obamacare hatua iliowawacha viongozi wa Republican na uchache wa kura kufanya mabadiliko hayo.

Mike Lee na Jerry Moran wote walitangaza kwamba hawawezi kuunga mkono muswada huo kama ulivyo.

Viongozi wa Republican wanashikilia viti 52 katika bunge hilo lenye wanachama 100, na huku wanachama wawili wa Republican wakiupinga muswada huo hawangeweza kuruhusu viongozi wengine kuupinga.


Rais Trump aliahidi kuubadilisha muswada wa afya wa rais Obama kama ahadi yake wakati wa kampeni

Maseneta hao wawili walitangaza hatua yao mara moja.

Huku wakisema kuwa kulikuwa na matatizo mbalimbali kuhusu muswada wa Obamacare, waliongezea kuwa ''hawawezi kuidhinisha sera mbaya''.


 Maseneta wengine wawili, Rand Paul na Susan Collins



Hatua hiyo inaendeleza kuwatoza kodi muhimu matajiri huku ikiwaondolea mzigo watoaji huduma za bima ili kuweza kuwapunguzia malipo watu masikini wanaohitaji huduma ya afya.


Maseneta wengine wawili, Rand Paul na Susan Collins tayari walikuwa wametangaza kuupinga musawada huo.

Democrats walikuwa wamesema kuwa hawatakubali kuubadilisha muswada huo wa Obamacare lakini wanaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kuufanya kuwa imara.

Viongozi wa Republican na ikulu ya Whitehouse sasa watalazimika kuamua iwapo watauandika upya mpango huo ama kuanzisha juhudi mpya bila kupendelea chama chochote kuangazia matatizo yaliopatikana na vyama vyote viwili katika muswada wa Obamacare, ama kuangazia maswala mengine kama vile mabadiliko ya kodi.

Akiongea kuhusu kile kimetajwa kuwa pigo kubwa ,rais Trump amewataka Republicans kuubadilisha muswada huo wa Obamacare na kuanza juhudi za kutengeza muswada mwengine wa afya ambao utaungwa mkono na Democrats.

Bunge la seneti limekuwa likichelewesha likizo yao kwa lengo la kubadilisha muswada huo wa aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama.

  Habari: Kimataifa

 

JAJI ADHOOFISHA MARUFUKU YA TRUMP DHIDI YA MATAIFA 6 YA KIISLAMU
Bibi na babu pamoja na jamaa wengine wa watu wa familia zinazoishi Marekani hawawezi kuzuiwa kuingia nchini humo chini ya marufuku ya rais Trump , jaji mmoja ameamuru.

Agizo hilo la jaji wa wilaya Judge Derrick Watson katika jimbo la Hawaii, ni pigo jipya kwa marufuku hiyo.
Jaji huyo alisema kuwa marufuku hiyo haikuelewa vizuri agizo la mahakama ya juu .
Uamuzi huo uliotolewa mwezi uliopita, uliidhinisha kwa uchache marufuku hiyo dhidi ya wakimbizi na wanaozuru taifa hil kutoka kwa mataifa sita ya kiislamu.
Bibi na babu pamoja na jamaa wengine wa watu wa familia zinazoishi Marekani hawawezi kuzuiwa kuingia nchini humo chini ya marufuku ya rais TrumpUlisema kuwa wale walio na familia zao wataruhusiwa kuingia Marekani.
Lakini utawala wa Trump uliamua kwamba uamuzi huo haukuhusisha bibi na babu pamoja na wajukuu, mashemeji ,wajomba, mashangazi, mpwa wa kiume na wa kike na binamu.
Jaji huyo alishutumu uelewa wa serikali kuhusu watu wa karibu wa familia.
Ukweli ni kwamba, kwa mfano watu wa karibu wa familia wanashirikisha bibi na babu.
Bibi na Babu ndio chanzo cha watu wa karibu wa familia,aliandika.
Mahakama ya juu bado inaangazia jaribio la kuwazuia raia wa Iran,Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen kuingia nchini Marekani.
Mahakama iliamuru marufuku ya muda kutekelezwa mnamo mwezi Mei.
Bwana Trump anasema kuwa vikwazo hivyo vinahitajika ili kuimarisha usalama wa Marekani dhidi ya mashambulio ya kigaidi.
Hatahivyo wakosoaji ikiwemo majimbo na makundi yanayopigania makundi ya wakimbizi yamesema kuwa marufuku hiyo inawabagua Waislamu.

Habari: Kimataifa

SHIMO LENYE UREFU WA KINA CHA MITA TANO LAWAKWAMISHA WATU WAWILI WASITOKE.

Kitengo cha dharura nchini Mexico kinafanya juhudi za makusudi kutaka kuwaokoa watu wawili waliokuwa wameabiri gari ambao wamenaswa katika gari ambalo lililotumbukia katika shimo lenye urefu wa kina cha mita tano .

Shimo hilo lilionekana baada ya mvua kubwa iliyonyesha katika barabara kubwa iliyozinduliwa hivi karibuni ambayo ni kiungo baina ya mji wa Cuernavaca na Mexico City.
Gari hilo na pikipiki vilitumbukia katika shimo hilo ambalo linadhaniwa kujitengeneza kutokana na mvua kubwa Kuingilia sehemu ya barabara kuu iliyofanyiwa ukarabati kabla ya majira ya mvua.


Trump atoa ishara za kubadili msimama kuhusu tabia nchi Ufaransa  

Rais wa Ufaransa Manuel Macron amesema kuwa anaheshimu uamuzi wa rais Trump kujitoa katika makubaliano ya tabia nchi ya Paris na kwamba Ufaransa itaendelea na juhudi zake kuhusu makubaliano hayo.

''Kuhusu tabia nchi tunajua tofauti yetu'', Bwana Macron alisema mjini Paris siku ya Alhamisi , akiongezea: Ni muhimu kusonga mbele.

Akizungumza pamoja na Macron, rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba huenda Marekani ikabadili msimamo wake lakini hakutoa maelezo ya zaidi.

''Kitu kitafanyika kwa heshima ya makubaliano ya Paris''.

Bwana Trump aliongezea: Tutaona kile kitakachofanyika.

Rais huyo wa Marekani alijiondoa katika makubaliano hayo 2015 mwezi uliopita, akitaka kujadili upya kwa makubaliano hayo ili kutoiweka Marekani katika hatua isiyo na manufaa kwake kibiashara.

Bwana Macron alisema kuwa ni muhimu kuweka makubaliano hayo kando huku viongozi hao wawili wakizungumza vile watakavyofanya kazi kuhusu maswala kama vile kusitishwa kwa mapigano nchini Syria na ushirikiano wa kibiashara.

Tuna tofauti zetu; Bwana Trump ana ahadi za uchaguzi alizowapatia raia wa tafa lake na pia mimi nilikuwa na ahadi, je vitu hivi vinapaswa kuturudisha nyuma katika maswala yote? Hapana, alisema Macron.

Bwana Macron na Trump baadaye walizungumza kuhusu juhudi za pamoja za mataifa hayo katika kukabiliana na ugaidi na hususan kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq.

"Marekani inahusishwa pakubwa katika vita vinavyoendelea nchini Iraq'', alisema Macron, ''ningependa kumshukuru rais kwa kila kitu kinachofanywa na wanajeshi wa Marekani katika eneo hili''.

''Tumekubaliana tuendeleze na juhudi zetu za pamoja'' ,aliongezea ''husuasan mipango baada ya vita''.

Bwana Macron alisema kuwa Ufaransa itaweka mikakati kadhaa ili kusaidia kuimarisha uthabiti katika eneo hilo.

Habari: Kimataifa

JESHI LA CHINA LAELEKEA KUWEKA KAMBI YA KWANZA YA KIGENI DJIBOUTI

Meli zinazowasafirisha wanajeshi wa China zinaelekea nchini Djibouti kuweka kambi ya jeshi ya China ambayo ndiyo ya kwanza ya kigeni.

China inasema kuwa kambi hiyo itatumiwa kwa huduma za kulida amani na za kibinadamu barani Afrika na magharibi mwa Asia.

Pia itatumiwa kwa ushikiano wa kijeshi, mazoezi ya kijeshi na huduma za uokoaji.
China imewekezaa katika nchi za kiafrika na pia imeboresha kwa haraka jeshi lake miaka ya hivi karibuni.

















Shirika la habari ya Xinhua lilisema kuwa meli hizo ziliondoka bandari ya Zhanjiang katika mkoa wa kusini wa Guangdong siku ya Jumanne.
Halikutaja idadi ya wanajeshi au meli zilizoplelekwa Djibouti au ni lini kituo hicho kitaanza kutangaza huduma zake.
    Xinhua linasema kuwa kituoa hicho cha Djibouti kinabuniwa kufuatia mazungumzo kati ya nchi hizo mbili.
    Kituo hicho kinaonekana kama hatua ya China ya kuwa na usemi wa kijeshi eneo hilo.
    Habari: Kimataifa

    Trump ashtakiwa kwa kuwazuia wakosoaji katika Twitter


    Rais wa Marekani Donald Trump kwa muda wa miaka 30 amekabiliwa na zaidi ya na kesi 4,000
    Na sasa mwanabiashara huyo ambaye sasa ni Rais, ameshtakiwa kwa mara nyingine, baada ya watu saba kumshtaki kwa kuwazuia kwenye akaunti yake ya twitter.

    Bwana Trump ni mtumiaji mkubwa wa mitandao ya kijami ambayo anaituma kuwapongeza washirika na kuwashambulia mahasimu wake.
    Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na taasi ya Knight First Amendment Institute, ambalo ni kundi la kupigania uhuru wa kusema katika chuo cha Columbia.
    Watumiaji hao saba walisema kuwa akaunti zao zilifungwa na rais au wasaidizi wake, baada ya wao kukejeli au kukosoa ujumbe alioandika Trump.
    Watumiaji wa Twitter hawan uwezo wa kuona au kujibu ujumbe katika akaunti zinazowazuia.
    Mashtaka hayo ni kuwa kwa kuwazuia watu hawa, Bwana Trump amewazuia kujiunga na majadiliano ya mtandaoni.

    Habari: Kimataifa

    Mzee mwenye watoto 100 anasema ana nia ya kuongeza watoto zaidi



    Wakati ulimwengu ulipoadhimisha siku ya idadia ya watu duniani mwanamume mmoja alikuwa na sababu 100 za kusherehekea.
    Kofi Asilenu mwenye umri wa miaka 80 ni baba wa watoto 100 na wake 12.
    Anaishi na familia yake katika kijiji chaAmankrom kilicho umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu Acca.
    Familia yake ni thuluthi moja ya watu 600 katika kijiji hicho.
    Anasema kuwa anataka familia kubwa kwa sababu hakuwa na ndugu.
    Sina kaka wala shangazi,ndio sababu niliamua kuwa na watoto wengi ndio wapate kunipa maziko yaliyo mazuri nikifa.
    Familia hiyo yake hata hivyoy imemgharimu pakubwa. anasema alikuwa mtu mwenye mali, lakini male hiyo ilipungua kutokana na gharama ya kuitunza familia yake kubwa
    Kofi Asilenu anaonekama kuwa mwenye afya nzuri na hata anasema kuwa na watoto zaidi.

    Bemba ahukumiwa miaka 18 jela

    Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono.
    Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi kwa makoso ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.
    Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo.

    Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.

     

    wafuasi wa Bemba wakifuatilia hukumu yake kutokea DRC  ..................................................................

    Ghasia zazuka Afrika ya Kusini

    Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzua ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.

    Taarifa ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu, inasema kuwa maafisa wa polisi walifyatuliwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao kwa mawe.

    Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC kugombea uchaguzi mwezi Agosti.

    Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.
    Serikali ya Afrika Kusini imeoamba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo.

     

    Niger yachagua vita dhidi ya Boko Haram.

    Bunge la Niger limepiga kura kwa kauli moja, kutuma vikosi nchini Nigeria kujiunga na mapambano ya kikanda dhidi ya kundi la Boko Haram. Kulingana na azimio la bunge hilo, Niger itatuma wanajeshi 750 nchini Nigeria. 

    Wavuvi hawaendi tena ziwani kuvua, wakulima hawaendi tena mashambani, shule zimefungwa. Wakaazi wa maeneo ya mpakani ya Diffa na Bosso, kusini mwa Niger wamejawa na hofu, kutokana na magaidi waliojigeuza wapiganaji wa jihadi, ambao wanatishia usalama wa taifa lao." Hao ni makatili tu wasioheshimu sheria, wanaiba, kuuwa, na kubaka," alisema Abdou Lokoko, mfanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali nchini Niger.

         Kwa mara ya kwanza wapiganaji hao kutoka kaskazini mwa Nigeria wameshambulia maeneo ya upande wa Niger katika siku chache zilizopita. Siku ya Jumatatu, wakati bunge likijiandaa na kura hiyo, Boko Haram waliushambulia mji wa Diffa wenye wakaazi 60,000 na kuuwa watu watano.

    Jeshi lilifanikiwa kuwafurusha, kwa mujibu wa maelezo yake, lakini muda mfupi baadae, ilifuatia miripuko ya mabomu.Katika mashambulizi sawa na hayo wiki iliyopita, mamia ya wapiganaji wa Boko Haram waliripotiwa kuuawa katika miji ya Diffa na Bosso, pia wanajeshi kadhaa na raia pia walipoteza maisha.
          "Tuna ushahidi wa Boko Haram kuendesha harakati zake ndani ya Niger, na hiyo ni tangu mwaka 2012, wakati washukiwa kadhaa wa Boko harama walipokamatwa na maafisa wa idara ya usalama ya Niger, hasa katika mikoa wa Zinder na Diffa iliyoko mpakani na Nigeria," alisema Ryan Cummings, mchambuzi wa masuala ya usalama wa shirika la ushauri la red.24 la Afrika Kusini, ambalo ni sehemu ya mtandao wa usalama wa Nigeria.

    Kikosi cha pamoja dhidi ya Boko Haram
    Mwishoni mwa wiki Nigeria na majirani zake - Chad, Niger, Cameroon na Benin, zilikubaliana kuunda kikosi cha wanajeshi, polisi na watalaamu wa kiraia 8,700, kwa ajili ya mapambano dhidi ya Boko Haram. Idadi hii ni kubwa kuliko iliyopendekezwa na Umoja wa Afrika. Tayari wanajeshi wa Chad wako katika eneo la mpakani wakipambana na Boko Haram tangu mwezi Januari. Cameroon nayo imeanza kujitayarisha.
    "Yeyote anaetaka amani laazima ajiandae na vita hivi," alisema Abdou Lokoko, ambaye pamoja na shirika lake wamekuwa wakitoa wito wa kujenga kikosi cha pamoja dhidi ya Boko Haram. "Ikiwa hatutofanya chochote, basi wataendelea kutushambulia. Wanajeshi wetu ni mashujaa na wako tayari kwa mapambano. Mungu akipenda watatulinda."

    Jeshi kamili la magaidi
    Lakini kumuamini Mungu tu hakutowasaidia wanajeshi hao. Taarifa mpya za mashirika ya ujasusi ya Marekani zinaonyesha kuwa Boko Haram ina wapiganaji kati ya 4000 na 6000. Katika maeneo yaliyoko chini ya udhibiti wake, kundi hilo lina mtandao wa miji na vijiji 30, ambako linaweza kuwandikisha wapiganaji.
    Idadi hii haimshangazi mtaalamu wa masuala ya usalama Ryan Cummings. Anasema huenda wapiganaji wa Boko Haram ni wengi zaidi kuliko idadi hiyo. "Hao ndiyo wale wapiganaji wa itikadi kali waliofunzwa vizuri. Kuna wapiganaji wa ziada, ambao ama wanaandikishwa kwa nguvu, au wanalipwa.Kuna uvumi pia kuwa kundi hilo linakodi magenge yenye silaha."
    Kwa hilo kundi hilo la kigaidi limeunda jeshi kamili tangu muda mrefu. Na pia lina kiongozi anaependa kujionyesha kwa jamii kama mtu asiye na mzaha.Katika mkanda wake wa video wa karibuni, Abubakar Shekau anaonekana akiapa kukishinda vibaya kikosi hicho cha kanda.
    "Tutamkamata mmoja baada ya mweingine," alitishia Shekau, akiyalenga mataifa yanayoshiriki operesheni dhidi ya kundi lake. Lakini Mchambuzi Ryan Cummings anaamini jeshi la pamoja litaweza kuidhofisha Boko Haram.



    "Kundi hilo litalaazimika kwa mara ya kwanza kupambana kwenye nyanja tofauti kwa wakati mmoja. Hadi sasa Boko Haram ilikuwa inapambana na jeshi la Nigeria kutokea upande wa magharibi. Kwa nchi za Chad, Cameroon, Benin na Niger kujiunga na mapambano hayo, kundi hilo sasa litakabiliwa kwenye maeneo ya mashariki na kaskazini.
    Changamoto zinazowakabili washirika
    Lakini hilo linahitaji rasilimali: Wanajeshi, silaha, na vifaa vingine. Hilo litalipa kundi hilo changamoto kubwa na linaweza kudhoofisha kwa kiasi kikubwa, anasema Cummings. Lakini kikosi hicho cha kimataifa kinakabiliwa na changamoto kubwa sana. Ukosefu wa kuaminiana kati ya mataifa washirika, mizozo inayotokana na eneo lenye utajiri wa rasilimali kwenye ziwa Chad, ni vikwazo tosha.
    Lakini suala la ufadhili haliko bayana. Umoja wa Mataifa ulitaka kushiriki kwa kuwezesha usafiri, Umoja wa Afrika ulikuwa bado haufikia uamuzi wowote.