Showing posts with label HABARI ZA KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA KITAIFA. Show all posts

Friday, July 31, 2026

RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI ANGOLA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Luanda, Angola ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Hospitali iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tarehe 31 Julai.




Tuesday, July 28, 2026

UMEME JUA KISHAPU AWAMU YA PILI KUIONGEZEA TANZANIA MEGAWATI 100 ZA NISHATI JADIDIFU

Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeingia hatua mpya ya kuongeza vyanzo vya uzalishaji umeme baada ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa umeme kwa nguvu ya Jua Kishapu utakaozalisha jumla ya megawati 100.

Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 50 na kuingizwa katika Gridi ya Taifa, jambo lililoongeza uwezo na uthabiti wa gridi hiyo na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo Julai 27, 2026, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema sekta ya nishati ni mhimili wa maendeleo ya Taifa ambapo Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuongeza vyanzo mseto vya uzalishaji wa umeme (Energy Mix) ili kuhakikisha Tanzania haitegemei chanzo kimoja pekee cha uzalishaji wa umeme.


Thursday, July 23, 2026


Kambi ya matibabu ya bure iliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, imefanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 24,871, hatua inayoonyesha mwitikio mkubwa wa wananchi katika kupata huduma za afya za kibingwa na kibobezi. 

Idadi hiyo inaonesha mafanikio makubwa ya kambi hiyo iliyowaleta pamoja madaktari bingwa na wabobezi kutoka hospitali na taasisi mbalimbali nchini, wakitoa huduma za uchunguzi, matibabu, vipimo na ushauri wa afya bila malipo kwa wananchi kutoka Arusha na mikoa jirani. 

Makonda amesema kuwa,Kambi ya matibabu ya madaktari bingwa imefanikiwa kubaini wananchi 1,930 waliokuwa na shinikizo la juu la damu bila kufahamu hali zao za kiafya, hatua iliyotajwa kuwa muhimu katika kuzuia madhara ya magonjwa yasiyoambukiza kupitia uchunguzi wa mapema.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa kambi hiyo, Mbunge wa Arusha ambaye pia ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema jumla ya wananchi 6,070 walifanyiwa uchunguzi wa shinikizo la damu, ambapo asilimia 65 walibainika kuwa na tatizo hilo

Amesema kati yao, wananchi 1,930 waligundulika kwa mara ya kwanza kuwa na ugonjwa huo na wataendelea kufuatiliwa na wataalamu wa afya ili kupata matibabu na ushauri unaostahili.

Thursday, July 16, 2026

TANZANIA KUONGEZA KASI KATIKA HUDUMA YA UPANDIKIZAJI WA ULOTO


Serikali imeeleza dhamira yake ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za afya za kibingwa katika Afrika Mashariki na Kati huku ikitoa wito kwa Watanzania na wadau mbalimbali kushiriki kuchangia Mfuko wa Upandikizaji wa Figo na Uloto ili kuwawezesha wagonjwa wasiokuwa na uwezo kupata matibabu yanayookoa maisha.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb), wakati akiwasilisha taarifa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), katika hafla ya chakula cha pamoja cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kugharamia huduma za upandikizaji wa figo na uloto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, iliyofanyika jijini Dodoma.


Sunday, July 12, 2026

WAZIRI DEUS SANGU AWAOMBA WATUMISHI WA MUNGU KUENDELEA KUDUMISHA AMANI YA NCHI


Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri mkuu, kazi, ajira na mahusiano ya kazi Deusi Sangu amewaomba watumishi wa mungu waendelee kudumisha umaadili, mshikamano na amani ya nchi.

Ameyasema hayo katika kongamano la kurejesha thamani, lililofanyika Mkoani Morogoro ambalo pia lilikuwa na lengo la kuiombea nchi ambapo ameongeza kuwa serikali inawatambua na kuwathamani watumishi wa mungu.

Amesema katika kuishi dhamira hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani wakati akizindua bunge la 13 aliipa wizara yake jukumu la kuratibu mahusiano baina ya serikali na makundi ya kijamii ambapo uratibu huo unahusisha wadau wa siasa, taasisi za dini, Asasi za Kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali na kwamba wanafanya kazi na wadau hao wote kwa karibu ili kuhakikisha wanaimarisha amani, utulivu upendo, mshikamano na maridhiano ya kitaifa.

Amesema mambo hayo ndio nguzo kuu na mahusiano na dhamira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2026.


Monday, July 6, 2026

MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI YAANZA RASMI BURUNDI KWA MIJADALA YA KITAALUMA

Maadhimisho ya 5 ya Siku ya Kiswahili Duniani (MASIKIDU), yanayofanyika tarehe 5 hadi 7 Julai 2026, yamefunguliwa rasmi Nchini Burundi ikiwa ni hatua muhimu ya kihistoria ya kuendeleza lugha ya Kiswahili, yakifanyika sambamba na Kongamano la 3 la Kimataifa la Kiswahili kupitia Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA), yakiwakutanisha wadau wa Kiswahili kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko duniani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo, Waziri wa Vijana, Michezo na Utamaduni wa Jamhuri ya Burundi, Bi. Lydia Nsekela, amesisitiza kuwa Kiswahili ni nyenzo muhimu ya kuimarisha mshikamano wa kikanda, kukuza utamaduni na kuendeleza ushirikiano kati ya mataifa ya Afrika Mashariki.

Aliongeza kuwa serikali ya Burundi itaendelea kuunga mkono juhudi za kukuza na kueneza matumizi ya Kiswahili katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu, utamaduni na teknolojia.

Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya kaulimbiu isemayo “Kiswahili, Wingi-Lugha, na Akili Unde (Kiswahili, Multilingualism and Artificial Intelligence)”, ambapo washiriki wanashiriki mijadala ya kitaaluma, mawasilisho ya mada mbalimbali pamoja na maonesho ya teknolojia yanayoonesha nafasi ya Akili Unde katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili.

Kongamano hilo linafanyika likilenga kutoa mapendekezo yatakayochochea matumizi ya Kiswahili katika elimu, utafiti, ubunifu wa kidijitali na ushirikiano wa kimataifa.

kilele cha maadhimisho hayo ni Julai 7, 2026, ambapo shughuli rasmi zitahitimishwa kama sehemu ya kuendeleza ajenda ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya kimataifa inayochochea maendeleo na umoja wa Afrika Mashariki.

 



Tuesday, July 9, 2019

Simanzi: Sala ya kuaga miili ya wafanyakazi watano wa Azam Tv yafanyika

Marehemu wafanyakazi wa Azam Tv wamepewa heshima za mwisho


Vilio na simanzi vimetawala katika ofisi za makao makuu ya kampuni ya Azam TV hii leo ambapo wafanyakazi watano wa kampuni hiyo wanaagwa baada ya kufariki kwenye ajali ya barabarani.
Ajali iliyogharimu maisha ya wafanyakazi hao ilitokea Shelui mkoani Singida asubuhi ya Jumatatu Juni 8.

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Ahudhiria Mkutano Wa 12 Wa Dharura Wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,  ameshiriki katika Mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) unaofanyika jijini Niamey nchini Niger.

Bunge la Tanzania kuwa mwenyeji wa vikao vya Kamati ya Uongozi na ya Bajeti za Chama cha Wabunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola–Kanda ya Afrika


Bunge la Tanzania linatarajia kuwa mwenyeji wa vikao vya Kamati ya Uongozi na ya Bajeti za Chama cha Wabunge wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola–Kanda ya Afrika (CPA-AFRICA REGION) vitakavyofanyika tarehe 9 hadi 14, Julai, 2019 katika Ofisi Ndogo za Bunge la Tanzania, Jijini Dar es Salaam.

Upandaji holela wa miti katika njia za umeme Kahama watajwa kusababisha nishati ya umeme kukatika.



Upandaji holela wa miti katika njia kuu za Umeme Wilayani kahama mkoani Shinyanga umetajwa kuchangia kusababisha Nishati hiyo kukatika mara kwa mara kutoka na miti hiyo kugusa nyanya za Umeme.

Wednesday, July 3, 2019

HOSPITALI YA HAYDOM YANUNUA X RAY MPYA YA KISASA

HOSPITALI ya rufaa ya Haydom Wilayani Mbulu, Mkoani Manyara imenunua mashine mpya ya kisasa ya uchunguzi (X-ray) kwa lengo la kuhudumia wagonjwa wengi, kuongeza ufanisi na kutoa huduma kwa urahisi zaidi.

WIZARA YA VIWANDA YAJIPANGA KUKUZA MASOKO NDANI NA NJE YA NCHI


MAONESHO ya 43 ya biashara maarufu kama sabasaba yenye  kauli mbiu ya usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo ya viwanda yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam huku masuala ya utafutaji wa masoko pamoja na kuelimimisha wafanyabiashara kuhusiana na kliniki ya biashara yakitiliwa mkazo.

NUNDU APIGA HESABU ZA UBUNGE JIMBO LA TANGA 2020

ALIYEKUWA Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano katika serikali ya awamu ya nne Mhandisi Omari Nundu ametangaza nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Tanga mwaka 2020 mara baada ya kipenga kutangazwa rasmi. 

Mawaziri Bara, Zanzibar Wasaini Makubaliano ya Ushirikiano



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar  Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume wamesaini makubaliano ya ushirikiano katika kusimamia na kutekeleza sekta za Habari, Utamaduni,Sanaa na michezo ili kuongeza tija.

IGP Sirro Aongoza Kikao Cha Utendaji Cha Maofisa Wakuu Wa Jeshi La Polisi


Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (katikati), akiongoza Kikao cha Utendaji cha Maofisa Wakuu  wa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam, kujadili utendaji wa kazi za Polisi, kufanya tathmini, Mafanikio, Changamoto na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi hususan kulinda maisha ya raia na mali zao.

Sunday, June 23, 2019

Katibu Mkuu CCM Dr. Bashiru ahoji maswali Haya kwa wanaosema uchumi wa Tanzania haukui


NA RICH VOICE.
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Bashiru Ally amezindua ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mkoani Pwani,ambapo amechangisha zaidi ya milioni 25 na vifaa mbalimbali.

Wednesday, June 19, 2019

Pierre Liquid A.KA "Konki Fire" Katua Tena Bungeni....Tazama Hapa Akisalimiana na Waziri Mkuu


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii Pierre Liquid kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 19, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii Pierre Liquid kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 19, 2019.  Wa pili kulia ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Mhandisi Ramo Makani.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali Kutoa Tamko Rasmi Kuhusu Ugonjwa wa Dengue


Serikali imeeleza kuwa inatarajia kuja na utaratibu mpya wa kutibu ugonjwa wa Dengue ambao umezuka katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Dar es Salaam na kupelekea vifo kwa baadhi ya watu na wengine kuugua.

DK.MABODI NA UGENI WA FRELIMO

UJUMBE wa Viongozi wa Chama Tawala cha Msumbiji cha FRELIMO wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Roque Silva Samuel wakipewa maelezo katika Eneo la Kihistoria alipouawa kwa kupigwa Risasi na Wapinga Maendeleo Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume April 7, Mwaka 1972.

POLISI WAMSHIKILIA KIJANA WA MIAKA 19 KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWANAFUNZI JIJINI DAR

*

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inamshikilia kijana mweye umri 19 Ernest Joseph kwa tuhuma za mauji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU) kilichopo Gongolamboto jijini Anifa Mgaya(21).