Thursday, July 16, 2026

TANZANIA KUONGEZA KASI KATIKA HUDUMA YA UPANDIKIZAJI WA ULOTO


Serikali imeeleza dhamira yake ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za afya za kibingwa katika Afrika Mashariki na Kati huku ikitoa wito kwa Watanzania na wadau mbalimbali kushiriki kuchangia Mfuko wa Upandikizaji wa Figo na Uloto ili kuwawezesha wagonjwa wasiokuwa na uwezo kupata matibabu yanayookoa maisha.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb), wakati akiwasilisha taarifa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), katika hafla ya chakula cha pamoja cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kugharamia huduma za upandikizaji wa figo na uloto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, iliyofanyika jijini Dodoma.


No comments:

Post a Comment