Tuesday, July 7, 2026
Monday, July 6, 2026
HUENDA WACHEZAJI HAWA TUSIWAONE FANALI ZA WORLD CUP 2030
Hizi ni Picha za Ma-legendi kutoka Mataifa mbali mbali yaliyoshiriki kombe la Dunia 2026 Huko Mexico, Marekani na Canada na tayari wameshaondolewa
Christiano Ronaldo Mwenye Miaka 41 Ureno
Luca Modric Mwenye Miaka 40 Croatia
Manuel Neur Mwenye Miaka 40 Ujerumani
Neymar Santos Jr Miaka 34 Brazil
Ma-legendi hawa wote huenda tusiwaone katika Kombe la Dunia 2030 kwani tayari baadhi yao wametangaza kustafu soka la kimataifa wakiwa timu na
zao za taifa
Tizama wanavyohuzunika
RAIS DKT. SAMIA AMTEMBELEA PACOME HOSPITALINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtembelea kiungo wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Pacome alilazwa hospitalini baada ya kupata majeraha ya mguu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, ambapo Yanga SC ilicheza dhidi ya JKT Tanzania. Tukio hilo lilitokea Juni 30, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
RONALDO NA URENO YAKE YAONDOLEWA KOMBE LA DUNIA NA UHISPANIA
Cristiano na na wenzake wa
Ureno wameaga mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 kufuatia kipigo cha 1-0
dhidi ya Uhispania kwenye hatua ya 16 bora katika dimba la Dallas, Texas
Marekani.
Uhispania imetinga hatua ya robo fainali na itachuana na mshindi wa mchezo
mwingine wa hatua ya 16 bora kati ya wenyeji, Marekani dhidi ya Ubelgiji.
FT: Portugal 🇵🇹 0-1 🇪🇸
Spain
⚽ 90+1’ Merino.
Cristiano na na wenzake wa
Ureno wameaga mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 kufuatia kipigo cha 1-0
dhidi ya Uhispania kwenye hatua ya 16 bora katika dimba la Dallas, Texas
Marekani.
Uhispania imetinga hatua ya robo fainali na itachuana na mshindi wa mchezo
mwingine wa hatua ya 16 bora kati ya wenyeji, Marekani dhidi ya Ubelgiji.
FT: Portugal 🇵🇹 0-1 🇪🇸
Spain
⚽ 90+1’ Merino.
WENYEJI MAREKANI WATUPWA NJE WORLD CUP, UBELGIJI IKIIFUATA HISPANIA ROBO FAINALI
Timu ya Taifa ya Ubelgiji ‘The Red Devils’ imetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji wenza wa michuano hiyo, Marekani katika dimba la Seattle, Washington kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.
Ubelgiji itachuana na Uhispania kwenye hatua ya robo fainali, Uhispania ikitinga hatua baada ya kuisukumiza nje Ureno kwenye hatua ya 16 bora.
MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI YAANZA RASMI BURUNDI KWA MIJADALA YA KITAALUMA
Maadhimisho ya 5 ya Siku ya Kiswahili Duniani (MASIKIDU), yanayofanyika tarehe 5 hadi 7 Julai 2026, yamefunguliwa rasmi Nchini Burundi ikiwa ni hatua muhimu ya kihistoria ya kuendeleza lugha ya Kiswahili, yakifanyika sambamba na Kongamano la 3 la Kimataifa la Kiswahili kupitia Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki (KAKAMA), yakiwakutanisha wadau wa Kiswahili kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwingineko duniani.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo, Waziri wa Vijana, Michezo na Utamaduni wa Jamhuri ya Burundi, Bi. Lydia Nsekela, amesisitiza kuwa Kiswahili ni nyenzo muhimu ya kuimarisha mshikamano wa kikanda, kukuza utamaduni na kuendeleza ushirikiano kati ya mataifa ya Afrika Mashariki.
Aliongeza kuwa serikali ya Burundi itaendelea kuunga mkono
juhudi za kukuza na kueneza matumizi ya Kiswahili katika sekta mbalimbali,
ikiwemo elimu, utamaduni na teknolojia.
Maadhimisho hayo yanafanyika chini ya kaulimbiu isemayo
“Kiswahili, Wingi-Lugha, na Akili Unde (Kiswahili, Multilingualism and
Artificial Intelligence)”, ambapo washiriki wanashiriki mijadala ya kitaaluma,
mawasilisho ya mada mbalimbali pamoja na maonesho ya teknolojia yanayoonesha
nafasi ya Akili Unde katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili.
Kongamano hilo linafanyika likilenga kutoa mapendekezo
yatakayochochea matumizi ya Kiswahili katika elimu, utafiti, ubunifu wa
kidijitali na ushirikiano wa kimataifa.
kilele cha maadhimisho hayo ni Julai 7, 2026, ambapo
shughuli rasmi zitahitimishwa kama sehemu ya kuendeleza ajenda ya kukifanya
Kiswahili kuwa lugha ya kimataifa inayochochea maendeleo na umoja wa Afrika
Mashariki.
Sunday, July 5, 2026
MTU MWENYE IMANI HUMWABUDU MUNGU KWA UTULIVU
Kwa upande wake Mwalimu wa neno la Mungu Isaya Benson
akifundisha kuhusu somo lililokuwa na kichwa kisemacho Mapito yamebeba hatma
yako amesema kuwa watu wengi wanakimbia mapito wakati ndio njia ya kuwapeleka
katika hatma yao.
Naye Mngojezi wa Nabii Mkuu Claudia Silayo akifundisha
ibadani hapo amesema kuwa wazazi wahawatakiwi kuwa legelege kwenye malezi ya
Watoto.
Pia Mtumishi mwanafunzi Abel Likinjie amepata nafasi ya katika ibada hiyo ambapo amewataka kuwa wavumilivu ili matamko ya kinabii waliyotamkiwa yaweze kutimia maishani mwao na Baba wa kiroho ajivunie wao.
NORWAY YAIFUATA ENGLAND ROBO FAINALI, HAALAND APELEKA KILIO BRAZIL
Norway imeandika historia kwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuifunga Brazil mabao 2-1 katika mchezo wa hatua ya 16 bora uliochezwa Julai 5,2026
Nyota wa
Norway, Erling Haaland, alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga mabao
yote mawili katika dakika za 79 na 90, na kuipeleka nchi yake robo fainali ya
Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia.
Brazil ilipata nafasi kadhaa za kufunga lakini ilishindwa kuzitumia, ikiwemo mkwaju wa penalti uliokoswa kipindi cha kwanza. Neymar aliifungia Brazil bao la kufutia machozi kwa penalti katika muda wa nyongeza.
Kwa ushindi huo, Norway sasa inasonga mbele kusubiri mshindi wa mchezo kati ya Mexico na England katika hatua ya robo fainali, huku Brazil wakiaga mshindano.

















%20Facebook.png)
%20Facebook.png)








%20Instagram.png)











