Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekataa ombi la kujiuzulu kwa Waziri wa Usalama wa Ndani, kufuatia ghasia zilizozuka nchini humo.
Macron amesema waziri
Laurent Nunez, anapaswa kuendelea kuhudumu katika wadhfa wake na kutafuta
suluhisho za kukabiliana na waandamanaji waliohusika na ghasia haraka
iwezekanavyo.
Macron ameilaumu idara ya
usalama kwa kushindwa kukusanya taarifa za kijasusi mapema, hali iliyochangia
kuzuka kwa vurugu hizo.
Ghasia hizo zilitokea
baada ya maandamano makubwa kufanyika, kupinga kupanda kwa gharama za maisha na
kudorora kwa huduma za umma.
Mkutano wa dharura wa
serikali unatarajiwa kufanyika hii leo kujadili yaliyotokea.
Macron ameonya kuwa wote
waliohusika na ghasia hizo watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

No comments:
Post a Comment