Watu wametakiwa kuendelea kufungua macho na kumtazama Nabii Mkuu Mhe. Prof. GeorDavie kwa sababu Yesu Kristo yu ndani yake.
Hayo yamesemwa hii leo na
Mchungaji Kiongozi Mama Anna Davie wakati akiongoza ibada ya chuo kikuu cha
manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko ngurumo ya upako kisongo Arusha
ambapo ilikuwa ni ibada ya kumshukuru Mungu kwa kumuweka Nabii Mkuu katika
Taifa letu.
Naye Mtume Modekai katika
somo lake la kufungua mioyo ya watu waliofunga kwa ajili yako amesema kuwa ipo
mioyo wa watu iliyofungwa kwa ajili yako ili usiweze kuvuka na kufanikiwa.
Kwa upande wake kijana
Teresia Teit amesema kuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumuweka Nabii
Mkuu katika Taifa hili la Tanzania.
Kijana Moses Elias pia
alipata nafasi ya kufundisha katika ibada hiyo kuhusu Hofu na kusema kuwa hofu ni
hisia ya asili, wasiwasi au woga unaomjia mtu na inawatesa watu wengi.



No comments:
Post a Comment