Serikali imetangaza kuunda timu ya wataalamu itakayochunguza migogoro ya ardhi
nchini kwa kuangalia vyanzo vyake, ilipofikia na namna ya kuishughulikia.
Timu hiyo itakuwa na wataalamu watakaopitia migogoro hiyo kwa
upana, kubaini vyanzo vyake, hatua ilipofikia na hatua zinazoweza kuchukuliwa
kuitatua.
Hayo yamebainishwa Septemba 30, 2026 na Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo wakati wa maadhimisho ya
miaka 40 wa Habitat for Humanity Tanzania.
Dkt. Akwilapo amesema Serikali inatambua uwepo wa migogoro ya
ardhi na inaendelea kuchukua hatua kuishughulikia.
Amesema kuna migogoro ya aina tofauti ya ardhi akibainisha kuwa baadhi ni halisi huku mingine ikiwa ni migogoro inayotengenezwa, lakini yote inaendelea kushughulikiwa.

No comments:
Post a Comment