Sunday, September 20, 2026

WATU WAPASWA KUKAZA KATIKA KUMFUATA MTU ALIYEBEBA KUSUDI LA MAISHA YAO

Imeelezwa kuwa adui anajua mtu aliyebeba hatma ya maisha ya watu ndio maana anapiga vita watu kumfuata mtu aliyebeba hatma ya maisha yao.

Hayo yamesemwa hii leo na Mwalimu wa Neno la Mungu Isaya Benson wakati akihubiri katika ibada ya kusanyiko la vituo juu ya mwamba ya maandalizi ya ibada kuu ya tar 27 sept ambayo Nabii Mkuu Mhe. Prof. GeorDavie atakuwepo.

Amesema kuwa watu wanapaswa kukaza katika kumfuata Mtu aliyebeba kusudi kwa sababu hatma Mungu ameiunganisha na Mtu Mkuu wa Mungu ambaye ni Nabii Mkuu.

Kwa upande wake Mchungaji Restituta Melchiades amesema ili tuweze kupokea kile anachokuja nacho Mtu Mkuu wa Mungu ni lazima tujiweke katika utii, umoja, nidhamu na utakatifu huku tukiwa na Moyo safi na Imani ya kupokea kutoka kwa Mtu Mkuu wa Mungu.

Awali wasimamizi wa vituo juu ya mwamba wamepata nafasi ya kufundisha neno ambapo wamewataka watu kuendelea kuwa watii, wanyenyekevu na kuyashika matamko ya kinabii ili waweze kufanikiwa maeneo mbalimbali maishani mwao.

No comments:

Post a Comment