Tuesday, June 12, 2018

Anthony Joshua: Deontay Wilder amekubali pigano la kuunganisha mikanda Uingereza

Deontay Wilder kuzipiga na Anthtony Joshua 
Bingwa wa uzani mzito duniani Deontay Wilder anadai kwamba amekubali kuzipiga dhidi ya Anthony Joshua nchini Uingereza

ACT – Wazalendo kuibua mjadala mkuu wa Kitaifa uchambuzi wa bajeti (+video)

Chama cha ACT- Wazalendo kupitia Katibu Kamati ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu kimepanga kuja na majadala wa uchambuzi

Viongozi wa dini msiwe na wasemaji ambao sio viongozi – Rais Magufuli (+video)




Vifo vyaongezeka Ajali ya wanafunzi UDSM


Majeruhi mmoja kati ya wawili wa ajali iliyotokea eneo la River Side jijini Dar es Salaam ikihusisha gari la wagonjwa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amefariki dunia leo Juni 12, 2018.

Updates: Trump aridhika na mazungumzo pamoja na Kim, Wasaini Makubaliano Maalumu


Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamemaliza mazungumzo ya kwanza ya kihistoria kwa kutia saini taarifa juu ya ahadi za kuangamiza silaha za nuklia za Korea Kaskaizni.

Saturday, June 9, 2018

KARIA AWAPA YANGA SAA 48 KUTENGUA KAULI YA KUJITOA KOMBE LA KAGAME, VINGINEVYO…



RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ameutaka uongozi wa klabu ya Yanga kutoa jibu linaloeleweka hadi kufika Jumapili juu ya kujitoa kwao kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Kauli hiyo ya Karia leo, inafuatia Yanga kuiandikia barua TFF kuwaarifu kutoshiriki michuano hiyo kutokana na kubanwa na ratiba ya mashindano mengine.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya June 9

Waziri Mkuu Ataka Wanaotoa Taarifa Za Uongo Wadhibitiwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wawachukulie hatua kali wananchi wote wanaotumia vibaya namba za mawasiliano za jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu matukio ya majanga ya moto.

Friday, June 8, 2018

Mfumuko Wa Bei Nchini Waendelea Kupungua Toka Asilimia 3.8 Hadi Asilimia 3.6

Na. Eliphace Marwa – Maelezo
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo imetoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa mwezi Mei mwaka huu ambao umepungua hadi kufikia asilimia 3.6 ikilinganishwa na asilimia 3.8 ilivyokuwa kwa mwezi Aprili mwaka huu.

Waziri wa Elimu: Serikali Haitavumilia Walimu Wanaoshiriki Vitendo Vya Udhalilishaji Kwa Wanafunzi

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako Ndalichako ameweka wazi kwamba serikali haiwezi kuvumilia vitendo vya udhalilishaji  ambavyo vimeonekana kufanywa na mwalimu wa shule St. Florence iliyopo jijini Dar es salaam.

Waziri Mkuu Afungua Mkutano Wa Mawaziri Wa Madini Na Kuzindua Maabara Ya Kisasa Ya Madini........Inauwezo wa kutambua aina za madini na yalikotoka

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua maabara ya kisasa ya na ya kwanza barani Afrika yenye uwezo wa kupima na kutambua aina mbalimbali za madini.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 8

Mkuu Wa Majeshi Ahamasisha Vijana Kujiunga Jkt Kupata Stadi Za Kazi Ziwasaidie Kujiajiri

Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.

Thursday, June 7, 2018

Waziri Mkuu: Kutangaza Nyongeza Ya Mishahara Hadharani Kuna Madhara


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi kuwa suala la kutangaza nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma hadharani husababisha athari kwa jamii nzima na kwa wale ambao siyo watumishi.

Waziri Mkuu Asisitiza Kuzichukulia Hatua Asasi Za Kiraia


Mbunge wa Longido (CCM) Dkt. Steven Kiruswa ameitaka Serikali kuyafutia usajili Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) ambayo huongeza uchochezi nchini kwa kujishughulisha katika masuala ya siasa na hivyo kuhatarisha amani ya watanzania