Monday, July 27, 2026

MAAMBUKIZI YA EBOLA YAPINDUKIA 3,000 KONGO

 


Haya yanafanyika wakati ambapo maambukizi yameripotiwa kuongezeka kwa karibu 1,000 katika kipindi cha siku kumi tu.

Takwimu rasmi zinaonesha kuwa jumla ya visa 3,075 sasa vimethibitishwa katika mikoa mitano baada ya mlipuko huo wa Ebola kuvuka maambukizi 2,000 mnamo Julai 15.

Mamlaka zinasema ugunduzi wa maambukizi na juhudi za kupima zimechangia katika kugundua maambukizi zaidi.

Mlipuko huo uliotangazwa mnamo Mei 15, unasababishwa na aina ya kirusi cha Bundibugyo ambacho bado hakijapata chanjo au tiba.

Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, karibu asilimia 90 ya visa vimeripotiwa katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Ituri, ambao unapakana na Sudan Kusini na Uganda.

Mlipuko huo huenda ukadumu kwa miezi kadhaa zaidi kutokana na mgomo wa wahudumu wa afya wanaolalamikia kutolipwa mishara yao na kutatiza utoaji huduma katika baadhi ya hospitali.

No comments:

Post a Comment