Thursday, July 23, 2026


Kambi ya matibabu ya bure iliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, imefanikiwa kutoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 24,871, hatua inayoonyesha mwitikio mkubwa wa wananchi katika kupata huduma za afya za kibingwa na kibobezi. 

Idadi hiyo inaonesha mafanikio makubwa ya kambi hiyo iliyowaleta pamoja madaktari bingwa na wabobezi kutoka hospitali na taasisi mbalimbali nchini, wakitoa huduma za uchunguzi, matibabu, vipimo na ushauri wa afya bila malipo kwa wananchi kutoka Arusha na mikoa jirani. 

Makonda amesema kuwa,Kambi ya matibabu ya madaktari bingwa imefanikiwa kubaini wananchi 1,930 waliokuwa na shinikizo la juu la damu bila kufahamu hali zao za kiafya, hatua iliyotajwa kuwa muhimu katika kuzuia madhara ya magonjwa yasiyoambukiza kupitia uchunguzi wa mapema.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa kambi hiyo, Mbunge wa Arusha ambaye pia ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amesema jumla ya wananchi 6,070 walifanyiwa uchunguzi wa shinikizo la damu, ambapo asilimia 65 walibainika kuwa na tatizo hilo

Amesema kati yao, wananchi 1,930 waligundulika kwa mara ya kwanza kuwa na ugonjwa huo na wataendelea kufuatiliwa na wataalamu wa afya ili kupata matibabu na ushauri unaostahili.

No comments:

Post a Comment