Timu za Taifa za soka za
wanawake za Morocco na Algeria zimeanza vyema kampeni zao za Kombe la Mataifa
ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 kwa kuibuka na ushindi katika michezo yao
ya kwanza ya hatua ya makundi.
Wenyeji Morocco
wameonyesha ubora kwa kuichapa Kenya (Harambee Starlets) mabao 4-0 katika
mchezo wa Kundi A, huku Algeria ikiifunga Senegal mabao 2-0 na kuanza michuano
hiyo kwa pointi tatu muhimu.
Michuano hiyo inaendelea
leo ambapo Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, itashuka dimbani
kuivaa Afrika Kusini katika mchezo wa Kundi B utakaochezwa saa 2:00 usiku.

No comments:
Post a Comment