Sunday, June 26, 2016

Breaking News: Rais Magufuli Afanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na Afanya Mabadiliko Madogo ya Wakuu wa Mikoa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko

Ugonjwa Usiofahamika Ulioibuka mkoani Dodoma Na Kuwaathiri watu 32 Wafahamika

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema ugonjwa usiofahamika ulioibuka mkoani Dodoma, unatokana na sumukuvu inayopatikana kwenye nafaka.

Akizungumza jijini, Dar es Salaam jana, Ummy alitolea ufafanuzi kuhusu ugonjwa huo na kuongeza ndani ya wiki moja, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa 11 na kufanya jumla ya wagonjwa kufikia 32, ingawa idadi ya vifo haijaongezeka.

Alisema majibu kuhusu ugonjwa huo yanatokana na uchunguzi wa awali uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) na kwamba serikali imechukua nafaka kadhaa zinazopatikana mkoani Dodoma ili kuzipeleka Atlanta, Marekani kwa uchunguzi zaidi.

“Tulitoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo Juni 19 mwaka huu ambao ulipatikana wilaya za Chemba na Kondoa, kulikokuwa na wagonjwa 21 na vifo saba, hata hivyo mpaka kufikia juzi wagonjwa waliokumbwa na ugonjwa huo wameongezeka na kufikia 32 na idadi ya vifo imebakia saba,” alisema Ummy.

Alisema katika jitihada za kutambua kiini cha ugonjwa huo, Wizara imepeleka jopo la wataalamu huko Dodoma ili waweze kushirikiana na wenzao walioko huko kufanya uchunguzi wa kina wa ugonjwa huo.

Alisema sampuli mbalimbali za damu, haja ndogo, haja kubwa, vinyama vya ini na sampuli za vyakula, zilipelekwa katika maabara za Mkemia Mkuu wa Serikali, maabara ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Maabara ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu na maabara ya Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Vile vile sampuli nyingine kesho zitapelekwa Marekani katika maabara ya Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Marekani (CDC) kilichopo Atlanta kwa uchunguzi zaidi,” alisema Ummy.

Aidha alisema, “kuna uwezekano mkubwa kwamba ugonjwa huu umesababishwa na ulaji wa chakula kilichokuwa na sumukuvu na kuleta madhara, ili kuwa na uhakika na jambo hilo Wizara yangu inasubiri matokeo ya vipimo vya damu na haja ndogo vilivyopelekwa katika Maabara ya CDC matarajio yetu ni kupata majibu hayo katika kipindi kisichozidi wiki moja.”

Alisema tangu ugonjwa huo ulipoibuka, wagonjwa 12 wametibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na 18 wametibiwa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

Tuesday, June 21, 2016

Bemba ahukumiwa miaka 18 jela

Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono.

Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi kwa makoso ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.



Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo.

Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.
                  wafuasi wa bwana Bemba wakifuatilia hukumu yake kutokea DRC
Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.

VIDEO

BREAKING NEWS: GHASIA MBAYA ZASHUHUDIWA AFRIKA YA KUSINI

Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzua ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.
Taarifa ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu, inasema kuwa maafisa wa polisi walifyatuliwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao kwa mawe.

Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC kugombea uchaguzi mwezi Agosti.

Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.

Serikali ya Afrika Kusini imeoamba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo.

WABUNGE UPINZANI WAENDELEA KUGOMEA VIKAO VYA BUNGE, LEO WATOKA KIMYAKIMYA

Wabunge wa Ukawa wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Dk Tulia Ackson, lakini leo wametoka kimyakimya bila mbwembwe kama za jana.

Kwa sasa kamati ya uongozi ya umoja huo imeingia kufanya kikao kujadili mustakabali wao.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema watatoa taarifa kamili baada ya kumaliza kikao hicho.

Tuesday, April 26, 2016

RAIS MAGUFULI AMEIVUNJA BODI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)

Rais  Magufuli ameivunja Bodi ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simbakutokana na

Monday, April 25, 2016

IBADA YA JPILI TAR 24 APRIL 2016.


Nabii Mkuu Muheshimiwa Dr.GeorDavie ametangaza siku  ishirini na moja za kufuta kila aina ya maneno mabaya yaliyotamkwa kinyume kwa watu wote wanaomuamini Nabii,Na kusema kuwa

Friday, February 5, 2016

SERIKALI YABAINISHA VIKWAZO VYA MAENDELEO YA TAIFA

Serikali Imesema tatizo la ukuajiwa uchumi usioenda na maisha halisi ya mtanzani umechangiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kasi kubwa ya

Monday, February 1, 2016

IBADA YA JPILI TAR 31 JANUARY 2016

Wito umetolewa kwa Wanangurumo kudumisha moyo wa utoaji kwani hakuna ufalme wa mungu hauwezi kuendelea pasipo wana wa

Tuesday, January 26, 2016

BUNGE LA 11 MKUTANO WA PILI UMEANZA RASMI MJINI DODOMA


Bunge la 11 mkutano wa pili kikao cha kwanza la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limeanza leo mjini Dodoma ambapo limefunguliwa kwa