Friday, January 29, 2016

JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA LATOA MWALIKO KWA NABII MKUU Mh. Dr. GeorDavie.

Kiongozi mkuu wa huduma ya Ngurumo ya upako duniani Mh Nabii Mkuu Dr GeorDavie, amepata mualiko wa
heshma wa kushiriki katika hafla ya Jeshi  la polisi mkoani Arusha.
Mwaliko huu wa heshma ameupookea kutoka kwa kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi ambaye pia ni kamandawa polisi mkoani Arusha bwana Liberatus Sabas, mapema wiki hii.

Hafla hiyo itakayofanyika leo jioni itahusisha viongozi wa kada mbalimbali ikiwemo viongozi wa kiserikali, lengo likiwa kuwakaribisha maafisa wapya na kuwaaga wastaafu wa jeshi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Nabii Mkuu Mh Dr GeorDavie, imeeleza kupokea taarifa hiyo, huku nabii mkuu akithibitisha kuhudhuria hafla hiyo.


Jeshi la polisi mkoani Arusha limekuwa na utaratibu wa kufanya halfa kila mwanzo wa mwaka lengo likiwa ni kuwakaribisha maafisa wapya waliohamia katika mkoa wa Arusha kutoka mikoa mingine na kuwaaga wastaafu wa jeshi hilo waliostaafu kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment