Monday, February 1, 2016

IBADA YA JPILI TAR 31 JANUARY 2016

Wito umetolewa kwa Wanangurumo kudumisha moyo wa utoaji kwani hakuna ufalme wa mungu hauwezi kuendelea pasipo wana wa
ufalme kujitikita katika utoa.

Wito huo umetolewa na Kiongozi mkuu wa huduma ya ngurumo ya upako Duniani Baba Mh Nabii Mkuu Dr GeorDavie katika ibada ya chuo kikuu cha manabii katika hema la kukutania Ngurumo ya Upako Chuo Kikuu Cha Manabii Kisongo Arusha.


Aidha Nabii mkuu amebainisha kuwa nabii hawezi kufanya kazi yake vema huku akiwa anadaiwa, hivyo kila mtu lazima afanye kazi yake kwa uaminifu, yeye atoe upako na waamini watoe pesa ili kuujenga ufalme wa mungu


Ibada ya chuo cha manabii hapo jana iliongozwa na jumuia ya watoto ambapo walihitimisha mfululizo wa ibada za jumuia katika chuo kikuu cha manabii, ambapo hapo awali ibada za jumuia zilianzishwa na jumuia ya wababa, wamama na kisha kufuatiwa na jumuia ya vijana hatimaye jana kusitishwa na jumuia za watoto.
Awali katika ibada ya jana nabii mkuu ameitaja wiki hii kuwa ni wiki ya furaha na kicheko.


NENO LA KINABII LA WIKI....SIKILIZA /DOWNLOAD






...

No comments:

Post a Comment