Tuesday, September 26, 2017

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO Jumatano,Sept27,2017.


NAIBU WAZIRI WAMBURA AHITIMISHA MASHINDANO YA FLATEI JIMBO CUP MBULU

Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo ya michezo wakati wa kupanga mipango miji kwa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipokuwa akifunga fainali ya mashindano ya Jimbo Cup inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay iliyochezwa katika eneo la kata ya Dongobesh Wilaya ya Mbulu Mkoani wa Manyara.
“Natoa wito kwa Halmashauri zote ikiwemo halmashauri yenu ya wilaya ya Mbulu wakati wa kupanga matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya mipango miji mkumbuke kutenga maeneo ya michezo, Baraza la Michezo la Taifa litatoa mafunzo ya michezo na utaalam” alisema Naibu Waziri Wambura.

Daktari Atoa Uhahidi Mahakamani, Kadai Manji Yupo Hatarini na Anaweza Kufa Muda Wowote

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mustapha Bapumia (62) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anashangaa mtu mwenye umri mdogo kama Yusuf Manji (41) kuwa na vyuma vinne kwenye moyo.

Monday, September 25, 2017

Waliomuita Nkosazana Dlamini-Zuma kuwa "mke wa zamani wa Zuma" waomba msamaha

Rais Zuma ameoa wake wengi na Bi Dlamini-Zuma alikuwa mmoja wa wake zake watatu hadi Dlamini alipomtaliki mwaka 1998. 











Kituo cha taifa cha habari nchini Afrika Kusini kimemuomba msamaha mama anayetarajiwa kuwania urais Nkosazana Dlamini-Zuma, kwa kumuita "mke wa zamani wa Zuma"

Mwanamke aliyetajwa kuwa mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki

A picture of her at the start of treatment, bedbound and another more upright and alert after weight lossMwanamke raia wa Misri ambaye aliaminiwa kuwa mtu mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki kwenye hospitali moja katika umoja wa falme za kiarabu
Eman Ahmed Abd El Aty alikuwa amepelekwa nchini India kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili.

Rais Magufuli Kuongoza Vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - NEC Kwa Siku Mbili Dar


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa, anatarajia kuongoza kikao cha  Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam, Septemba 30 hadi Oktoba 1, 2017.

Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 25 Septemba, 2017 amemaliza ziara yake ya siku 6 katika Mkoa wa Arusha.

Waziri wa Afya Aipiga Marufuku Muhimbili kutoa rufaa za nje hata kwa Rais Maguful

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa agizo kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhakikisha haitoi rufaa ya matibabu nje ya nchi ikiwa wana uwezo wa kutibu maradhi husika hapa nchini.

NASSARY ADAI ATAJIUUZULU UBUNGE KAMA???????????????

Mbunge wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ameweka rehani ubunge wake  baada ya Rais John Magufuli kumpokea aliyekuwa diwani wa chama hicho aliyejiuzulu akisema ni kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za Rais.

Peter Msigwa Kaachiwa kwa Dhamana, Kuripoti kwa RCO Leo

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Msigwa ameachiwa huru jana usiku  kwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Ndugai: Tundu Lissu ana Bima ya Bunge, Hapaswi Kutibiwa kwa Michango

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu hayawezi kufanyika kwa kuchangishana michango kwa kuwa ana bima yake na haki zake ndani ya Bunge.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Septemba 25

Utafiti: Yafahamu magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa mbegu ya parachichi

Parachichi ni tunda linalopendwa na watu wengi haswa kwa jinsi lilivyo na virutubisho vingi, lakini hata hivyo wataalamu wa afya wameeleza kuwa mbegu iliyo katikati ya parachichi ambayo hutupwa ndio yenye virutubisho maradufu kuliko tunda lenyewe.

Tuesday, September 19, 2017

IBADA YA CHUO KIKUU CHA MANABII.

Watu mbalimbali wamehudhuria ibada ya chuo cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania kisongo Arusha Tanzania, ambapo watu waliohudhuria wamepokea nguvu ya Mungu kutoka kwa watumishi wa Mungu wanaotumika chini ya Nabii mkuu Mh. Dk. GeorDavie.
Pia katika ibada hiyo Gadinali wa kwanza wa huduma ya Ngurumo ya upako Mtume Gaudensia Luila amewakumbusha watu juu ya kuwasilisha michango yao kwa ajili ya kusapoti GeorDavie Tv.
Katika Ibada hiyo chungaji Rispar Asheri amesema ili uweze kupiga hatua katika maeneo mbalimbali ni lazima uwe mnyenyekevu mbele ya Mungu.
NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA IBADA HIYO..

MKURUGENZI MTENDAJI TANECO ALIMWA BARUA YA KUJIELEZA.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani amemtaka Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk Tito Mwinuka kuandika barua kujieleza ni kwa nini ameshindwa kuanza ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Kigamboni.
Dk Kalemani ametoa agizo hilo baada ya kutembelea vituo vya kupoozea umeme vya Gongo la Mboto, Kurasini na Kigamboni.

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO Jumanne,Sept19,2017.


RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI AJALI YA UGANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi aliyewahi kuwa Naibu Waziri na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Gregory Teu kufuatia vifo vya watu 13 ambao ni ndugu wa familia yake waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea nchini Uganda.
Watu hao wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye sherehe ya harusi kugongana na lori  tarehe 17 Septemba, 2017 majira ya saa

Friday, September 15, 2017

SERIKALI YAUNDA KIKOSI MAALUMU KUDHIBITI MASHAMBILIZI YA RISASI NCHINI.

Wiki moja baada ya kujeruhiwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu Serikali imeunda kikosi kazi kushughulikia uvunjifu wa amani nchini.
Kikosi hicho kinachoshirikisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama pia kinashughulika na kukusanya silaha za kivita ambazo zimekuwa zikitumika.

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO Alhamis,September15,2017.


Wednesday, September 13, 2017

RAIS MAGUFULI AVUNJA MAMLAKA YA UENDELEZAJI WA MJI WA KIGAMBONI (KDA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amevunja Mamlaka ya uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) kuanzia leo Septemba 13, 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa amethibitisha hilo na kusema kuwa Rais Magufuli ni msikivu kwani amesikia kilio cha watu wa Kigamboni na
kuamua kuivunja mamlaka hiyo ya Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA).
"Usikivu ni sehemu ya utatuzi hatimaye Rais wa Jamhuli ya Muungano wa

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI GERSON LWENGE

Waziri wa Maji na umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema Serikali inatekeleza ujenzi wa mradi wa bomba la maji safi kutoka ziwa viktoria kuelekea katika mji wa Ngudu na vijiji vinavyopitiwa na mradi huo  ili kuwapunguzia wananchi adha ya maji wanayoipata.


Waziri Gerson Lwenge amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Machimba Mashauri Ndaki mbunge wa Maswa Magharibi aliyetaka kujua