Showing posts with label HABARI ZA HUDUMA. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA HUDUMA. Show all posts

Monday, August 3, 2026

UNAPOKUWA NA MOYO WA KUSHUKURU MUNGU ANAKUONGEZA AFYA, NGUVU, UWEZO NA FAIDA YA KUISHA NA WATU.

Imeelezwa kuwa unapokuwa na moyo wa kushukuru Mungu anakuongeza afya, nguvu, uwezo na faida ya kuisha na watu katika maisha yako.

Hayo yamesemwa na mchungaji kiongozi mama Anna Davie katika ibada ya chuo kikuu cha Manabii iliyofanyika jana katika nyumba ya matamko kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni ibada ya shukrani kuu mbele za Mungu.

Naye Askofu Msaidizi Ken Davie alipata nafasi ya kuzungumza katika ibada hiyo na amesema kuwa kila mmoja na wajibu wa kuupendezesha ufalme wa Mungu huku akiongeza kuwa hata shukrani zetu zinatakiwa ziwe harufu nzuri kwa mungu.

Mtume Rose Abel alitapanafasi ya kuhubiri na amemtaka kila mtu kuwa na utaratibu wa kumshukuru mungu hata anapopitia changamoto mbalimbali katika maisha.

Kwa upande wake kijana MeikoKing amesema SHUKRANI inampa mtu 'PROMOTION' katika maisha ya kila siku.




 

Tuesday, July 28, 2026

PROF. GEORDAVIE MAFANIKIO HAYAJAWEKWA KWA AJILI YA WATU FULANI


Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amewataka watu kutambua kwamba kufanikiwa hakuji tu na wala mafanikio hayajawekwa kwa ajili ya watu fulani.

Ameyaema hayo mwishoni mwa wiki {Julai 25, 2026} wakati akifundisha katika mkutano wa akili ya fedha uliofanyika katika ukumbi wa PAPU Tower uliopo Philips jijini Arusha.

Akifundisha Prof. GeorDavie amesema mafanikio hayajawekwa kwa ajili ya watu Fulani ni mtazamo jambo ambalo amesema ni tatizo linawasumbua watu wengi kutokana na Fikra za mambo yaliyopita.


                                                               Habari Na Beatrice Maina

Thursday, July 16, 2026

TANZANIA KUONGEZA KASI KATIKA HUDUMA YA UPANDIKIZAJI WA ULOTO


Serikali imeeleza dhamira yake ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za afya za kibingwa katika Afrika Mashariki na Kati huku ikitoa wito kwa Watanzania na wadau mbalimbali kushiriki kuchangia Mfuko wa Upandikizaji wa Figo na Uloto ili kuwawezesha wagonjwa wasiokuwa na uwezo kupata matibabu yanayookoa maisha.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb), wakati akiwasilisha taarifa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), katika hafla ya chakula cha pamoja cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kugharamia huduma za upandikizaji wa figo na uloto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, iliyofanyika jijini Dodoma.


Monday, July 13, 2026

MHE. NABII MKUU PROF. GEORDAVIE ATOA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 58

Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie leo ametoa kiasi cha shilingi milioni 58 ambapo shilingi milioni 53 ni kwa ajili ya kusapoti maono ya rais wa umoja wa makanisa ya kitume na kinabii tanzania Nabii Dkt. Joshua Mwantyala na shilingi milioni 5 kwa mchungaji hananja.

Ametoa fedha hizo alipokuwa akizungumza na mitume na manabii kupitia kongamano la kurejesha thamani lililofanyika Morogoro katika huduma ya Nabii Dkt. Joshua ambaye pia ndio muandaaji wa kongamano hilo ambapo shilingi miloni 50 ni kwa ajili ya kuendeleza maono, shilingi milioni tatu kwa ajili ya nh’ombe wa maziwa ikiwa ni zawadi ya kumbukizi yake ya siku ya kuzaliwa.

Amempongeza na kufurahishwa na maono yake na kusema kuwa kiasi hicho cha fedha amempa ili zimsaidie kuendeleza maono yake.

MHE. NABII MKUU PROF. GEORDAVIE AWATAKA WATUMISHI WA MUNGU KUWA NA UMOJA NA UPENDO

Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie mlezi wa umoja wa makanisa ya kitume na kinabii amewataka watumishi wa mungu kuwa na umoja na upendo ili mungu aweze kuonekana katika utumishi wao.

Ameyasema hayo jumapili ya July 12, 2026 alipokuwa akizungumza  na watumishi wa mungu, wachungaji, walimu, wainjilisti, mitume na manabii kupitia kongamano la kurejesha thamani lililofanyika Mkoani Morogoro.

Akizungumza Nabii Mkuu amesema kuwa upendo wa kweli unakosekana kwa watumishi ka sababu kuna mafarakano mengi ambayo yanasababisha Mungu asionekane.

Amesema watumishi wa Mungu watakaposhikana mungu ataonekana zaidi na watafanya kazi zaidi katika huduma zao.


Sunday, July 12, 2026

MHE. NABII MKUU PROF. GEORDAVIE AMEMUWEKA WAKFU MTUMISHI WA MUNGU NABII JOSHUA MWANTYALA


Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amemuweka Wakfu Mtumishi wa Mungu Nabii Joshua Mwantyala ambaye pia ni Rais wa umoja wa makanisa ya kitume na Kinabii Tanzania.

Zoezi hilo amelifanya kupitia siku ya mwisho ya kongamano la siku tatu la kurejesha thamani aliloliandaa mkoani Morogoro ambapo wakfu huo amemuweka kwa kummiminia mafuta yeye kama Madhabahu na kumpokea rasmi kama mtoto wake wa kiroho.

Akimuweka wakfu Nabii Mkuu ametamka ya kuwa majira mapya yanakuja huku akiachilia matamko kwa Nabii Joshua kuwa na baraka za uwepo wa Mungu, Baraka ya ulinzi, baraka ya uongozi ambapo na alimkabidhi kipaza sauti microphone kama baraka ya fimbo kwa musa na kwamba atakapoongea sauti yake itakwenda juu sana kwa nchi na itakuwa na mamlaka yenye utiisho.


Monday, November 27, 2023

NABII MKUU DKT.GEORDAVIE AKABIDHI GARI NA SHILINGI MIL 11.4 KWA MUANDAAJI YA MISS TANZANITE MANYARA.

Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie ametoa gari jipya aina ya Honda station wagon yenye namba za usajili T169 EEP kwa muandaaji wa mashindano ya Miss Tanzanite Manyara Bi. Aminata pamoja na shilingi milioni 11.4.

Nabii Mkuu amekabidhi gari hilo jana katika ibada ya chuo kikuu cha manabii baada ya Bi.Aminata kuelezea changamoto anazokutana nazo katika kazi yake ambapo Nabii Mkuu aliguswa na kuamua kumsapoti gari hilo na fedha hizo ili aweze kuendesha ofisi yake ikiwa ni pamoja na kuwalipa washindi na washiriki wa mashindano hayo.

Kwa upande wake Bi. Aminata amemshukuru Nabii Mkuu kwa moyo wa upendo wa kusaidia watu huku akimuombea Nabii Mkuu Aishi miaka mingi ili awasaidie watu wengine wanaokutana na changamoto mbalimbali maishani mwao.

Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA.



Sunday, November 17, 2019

#NENO LA WIKI HII KINABII LATANGAZWA/NABII MKUU KUWEPO TENA JUMAPILI IJAYO/WAGENI HAWA KUHUDHURIA

NABII MKUU TANZANIA MH DKT GEORDAVIE AMETANGAZA KUWA HII NI WIKI YA MAWAZO YAKO KUPATA KIBALI,

NABII MKUU AMETANGAZA NENO HILO HII LEO KATIKA IBADA YA CHUO KIKUU CHA MANABII HEMANI KISONGO ARUSHA AMBAPO ILIKUWA NI IBADA YA KUPATANISHWA NA MADHABAHU.

NA NABII MKUU AMESEMA HIVI

Monday, August 5, 2019

NABII MKUU TANZANIA ATIKISA #ARUSHA, ATOA ZAIDI YA SH MILLIONI 10 ,KWA WAFANYABISHARA WADOGO ,ATAKA WENGINE KUWA WATOAJI .


Image may contain: Mathias Lazaro, smiling, standing
NABII MKUU TANZANIA MH DKT GeorDavie Royal Mkuu AMEWASAPOTI FEDHA ZA MITAJI ,WAFANYA BIASHARA WADOGO WADOGO ,PAMOJA NA MADEREVA TOYO NDANI YA WILAYA YA #ARUMERU KATA YA #MATEVES ,KIJIJI CHA #NGORBOB ,ZAIDI YA MILIONI

Wednesday, June 19, 2019

Rais Magufuli Ang’ara Jarida la Forbes.... Aendelea kukubalika Kimataifa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, ameendelea kukubalika kimataifa baada ya Jarida maarufu Duniani la Forbes kubashiri kwamba ataivusha Tanzania na kuwa nchi yenye kipato cha kati kupitia ajenda yake ya Tanzania ya viwanda chini ya mpango wa maendeleo wa 2025.

Thursday, March 28, 2019

AJENGEWA NYUMBA, WENGINE WASAPOTIWA FEDHA..

Kanisa dogo la mkoani Kilimanjaro lililopatiwa msaada na Nabii Mkuu.

Nyumba mpya anayojengewa Bi. Nawasa ikiwa inaendelea na ujenzi.
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa msaada wa jumla ya sh. 2,300,000 (milioni mbili na laki tatu), kwa watu watatu tofauti huku mwingine akipata neema ya kujengewa nyumba.
Hayo yamejiri wiki hii baada ya Nabii Mkuu kuguswa kuwasaidia watu wawili tofauti mtaji wa sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kila mmoja kwa ajili ya kuwawezesha kupata mtaji wa kuanzisha biashara.
Kwa upande mwingine Mchungaji mmoja wa kanisa dogo mkoani Kilimanjaro (jina lake na la kanisa linahifadhiwa) amebarikiwa sh. 300,000 (laki tatu) mara baada ya Nabii Mkuu kuliona kanisa hilo la mbao (kama linavyoonekana pichani) wakati akipita na msafara wake na kuwakuta katika ibada yao ambapo aliguswa kushuka na kuwasapoti kifedha na kisha kuendelea na safari yake.
Mchungaji huyo pamoja na waumini wake wasiozidi kumi (10) wakizungumza mara baada ya kupokea baraka hiyo ya kifedha walionyesha furaha yao na kutoa shukurani zao za dhati kwa Nabii Mkuu kutokana na msaada huo.
Wakati huohuo mwanamke mmoja muumini wa huduma ya Ngurumo Ya Upako anayefahamika kwa jina la Nawasa Saibulu, amepata neema ya kipekee ya kujengewa nyumba na Nabii Mkuu (kama inavyoonekana pichani ikiwa inaendelea na ujenzi) baada ya nyumba ya awali aliyokuwa akiishi iliyokuwa ya udongo kuharibika na kuwa na tatizo la kuingiza maji kipindi cha mvua.
Mwanamke huyo ni miongoni mwa watu waliopata neema hiyo ya kuboreshewa makazi yao kwa mwaka huu wa 2019.
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali ya kifedha ambapo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2019 ametumia zaidi ya sh. 40,000,000 (milioni arobaini) katika kugusa mahitaji mbalimbali ya watu kutoka sehemu tofauti tofauti duniani.


NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Wednesday, March 27, 2019

WABARIKIWA FEDHA KWAAJILI YA KUKUZA BIASHARA ZAO..



Neema ya kifedha imewatembelea baadhi ya watu waliokuwa na mahitaji ya fedha kwaajili ya kukuza biashara zao pamoja na kulipa madeni, ambapo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie aliwapatia fedha taslimu kwaajili ya kukidhi mahitaji yao.
Ni siku ya jumapili katika Ibada ya jiji, iliyofanyika katika katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako.. Kisongo, Arusha ambapo jumla ya 1,200,000 (milioni moja na laki mbili) ilitolewa nae Nabii Mkuu kwaajili ya kuwa-support kwenye shughuli zao waweze kujikimu kimaisha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watu hao wameelezea ugumu waliokuwa wakiupata kiuchumi na wepesi waliouona mara baada ya kubarikiwa kifedha nae Nabii Mkuu na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanaitendea haki fedha waliyopewa na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie.
Aidha siku ya jumapili katika Ibada ya Chuo Kikuu Cha Manabii ilikuwa ibada ya "Kupatiwa uelekeo mpya na sahihi maishani" ambapo Nabii Mkuu alifanya Huduma ya Unabii wa mtu mmoja mmoja wa kupita katikati ya maelfu ya watu waliofika siku ya jana na kuwahudumia kila mmoja kwa nafasi yake.
Akizungumza Nabii Mkuu alisema kuwa watu wengi wanateseka maishani kwa sababu ya uelekeo mbaya/ usiokuwa sahihi waliokuwa nao ambao huwapelekea kuteseka kwa maumivu na vifungo mbalimbali vya nguvu za giza, ambapo Nabii Mkuu aliwafungua na kuwatamkia matamko mbalimbali ya kuwapatia uelekeo mpya.
Wakati huo huo Nabii Mkuu ametangaza kuwepo tena jumapili ya tarehe 31/3/019 itakayokuwa ibada kufidiwa muda uliopotea.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Tuesday, February 19, 2019

WAPEWA PESA ZA MITAJI MIDOGO...!!


Jumla ya sh. Milioni moja, laki tisa na elfu hamsini (1,950,000) zimetolewa na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie kwa watu takribani kumi (10) wenye uhitaji wa aina mbalimbali waliojitokeza.
Ni katika ibada ya Chuo Kikuu Cha Manabii iliyofanyika katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako, ambapo Nabii Mkuu aliwataka watu wenye uhitaji wa pesa za kujikimu kujitokeza ambapo watu hao walijitokeza na kuweza kupata Neema hiyo ya kusaidiwa na Nabii Mkuu.
Pia watu wengine tofauti tofauti kwa nyakati tofauti wameweza kufikiwa na neema ya kusaidiwa kifedha na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ambapo amekuwa akituma pesa kwa kadiri jinsi Roho Wa Mungu amekuwa akimuongoza kuwasaidia watu hao ambao wamekuwa wakimuelezea uhitaji wao pamoja na hali ngumu wanazopitia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kupitia namba ya kunyanyua mikono ya Nabii.
Aidha Nabii Mkuu anatarajia kuwepo siku ya ijumaa katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako, Kisongo, Arusha ambapo itakuwa ni siku ya International Partners (IP) siku ambayo ni maalum kwa wana-International Partners kuwasilisha michango yao kwaajili ya ku-support GeorDavie Tv mikononi mwa Nabii Mkuu.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Monday, February 4, 2019

ALIPIWA DENI, KODI NA MTAJI..

"Mungu amenikumbuka, ameniona na amenifuta machozi" ni kauli ambayo ilitolewa na mwanamama aliyesaidiwa na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie baada ya kulipiwa kodi ya nyumba ya mwaka mzima pamoja na miezi mingine minne aliyokuwa akidaiwa ambapo pia aliongezewa mtaji wa biashara yake.
Mwanamama huyo anayefanya biashara ndogo ndogo alifika akilia mbele ya Nabii Mkuu ambapo alisema kuwa amekimbiwa na mume na kuachiwa watoto wanne, wakiwa wanaishi katika chumba kimoja ambacho alikuwa akidaiwa kodi ya miezi minne pamoja na watoto wake.
Baada ya kujieleza Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie alitoa pesa taslimu na kumkabidhi ili aweze kulipa kodi hiyo aliyokuwa akidaiwa pamoja na kumuongezea nyingine kwa ajili ya mwaka mzima ambapo alimuongezea mtaji wake ili aweze kujikimu na maisha.
Akizungumzia hilo Nabii Mkuu amesema kuwa Serikali Tukufu Ya Ufalme Wa Mungu imeamua kugusa matatizo ya kifedha waliyonayo watu wake ili kuhakikisha shida zinawapungukia na hatimaye kuisha kabisa.
Hayo yamejiri siku ya jana katika ibada ya Chuo Kikuu Cha Manabii, Ngurumo Ya Upako, ambapo ilikuwa ni ibada ya "Kufuta kumbukumbu zote mbaya maishani" ikiongozwa nae Nabii Mkuu.
Akizungumza katika ibada hiyo Nabii Mkuu alisema kumbukumbu mbaya hufanya watu wasipige hatua katika maisha, waishi wakiwa na huzuni pamoja na chuki ambapo alitamka matamko ya Kinabii kwaajili ya kuwatenganisha watu na hali hiyo.
Wakati huo huo Nabii Mkuu anatarajia kuwepo katika kipindi cha "Q and A AKILI KUBWA" siku ya leo kuanzia saa mbili na nusu za usiku, kipindi kitakachoruka kwa kupitia 99.3 N.Y.U Radio pamoja na GeorDavie Tv ambapo jumla ya 2,000,000 (milioni mbili) zitatolewa kwa washindi watakaoweza kujibu maswali kwa ufasaha kabisa.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

Sunday, February 3, 2019

ZAIDI YA MILIONI 14 YATOLEWA KWA JAMII- JANUARY..



Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa zaidi ya sh. 14,490,000 (Milioni kumi na nne, laki nne na elfu tisini), kwa mwezi wa January kama zawadi na misaada kwa watu mbalimbali.
Fedha hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti tofauti kwa kupitia vipindi mbalimbali vilivyokuwa vikiruka kupitia 99.3 N.Y.U FM pamoja na GEORDAVIE TV lakini wengine wakiweza kujipatia zawadi zao kwa kupitia ibada za Chuo Kikuu Cha Manabii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya watu walioweza kujishindia zawadi hizo, wamemshukuru Nabii Mkuu kwa zawadi hizo huku wakieleza pia jinsi ambavyo fedha hizo zimeweza kuwasaidia katika maeneo mbalimbali maishani mwao ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo ambayo walikuwa nayo.
Katika mwaka huu wa 2019 ambao ni "Mwaka wa kujenga uwezo" Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie, amesema kuwa hizi ni Zama Mpya ambapo Serikali tukufu ya Ufalme wa Mungu inawagusa watu wenye mahitaji kwa njia ya tofauti ambayo ni ya kuwasaidia kifedha na huu ukiwa muendelezo wa zoezi hilo lililoanza mwishoni mwa mwaka jana na bado likiwa endelevu.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Friday, January 25, 2019

VITUO VYA WATOTO YATIMA VYAPOKEA MSAADA WA CHAKULA.




    Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa misaada ya vyakula vyenye thamani ya sh. 3,120,000 (milioni tatu laki moja na elfu ishirini) kwa vituo viwili vya watoto yatima siku ya leo.
   Misaada hiyo imekabidhiwa asubuhi ya leo kwa niaba ya Nabii Mkuu nae Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila kwa wasimamizi wa vituo vya Faraja Orphanage center, Bw. Faraja, pamoja na kwa msimamizi wa kituo cha Christian Woman Orphanage Care anayeitwa Mchungaji Zakia Hatib.
   Vitu vilivyotolewa ni pamoja na mchele kg. 600 wenye thamani ya sh. 1,320,000 (milioni moja, laki tatu na elfu ishirini), mafuta ya kupikia lita 300 yenye thamani ya sh. 1,200,000 (milioni moja na laki mbili) pamoja na sukari kg. 240 yenye thamani ya sh. 600,000 (laki sita).
   Wakizungumza baada ya kupokea misaada, wasimamizi wa vituo hivyo wametoa shukurani zao za dhati kwa Nabii Mkuu kwa upendo wake pamoja na moyo wa kusaidia alionao kwa watu wote bila kujali dhehebu, dini wala kabila.
   Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali katika vituo vya watoto yatima kila mwanzo wa mwaka ambapo zoezi hilo litaendelea kwa vituo vingine.

NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio




Pichani ni Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila (kushoto) akikabidhi misaada kwa niaba ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie,  kwa msimamizi wa kituo cha Faraja Orphanage.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa kama misaada katika vituo vya watoto yatıma.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa katika  vituo vya watoto yatima.

Baadhi ya vyakula vilivyotolewa kwa watoto yatima.

Katika picha ni Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila (kushoto) katika picha ya pamoja na Msimamizi wa kituo cha Christian Woman Orphanage Care, wakati akimkabidhi misaada kwa niaba ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie.

Tuesday, January 15, 2019

NABII MKUU MHE. DR. GEORDAVIE ATANGAZA WIKI YA USHINDI KATIKA MAENEO YOTE MAISHANI.




 KUTOKA IKULU YA NABII MKUU TANZANIA..

    Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametangaza kuwa hii ni wiki ya kuwa washindi katika maeneo yote maishani.
    Ameyasema hayo wakati akiongoza ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania, Ngurumo Ya Upako, Kisongo, Arusha.
   Katika ibada hiyo ambayo pia ilikuwa ni ibada ya Silver Partners, Nabii Mkuu alitamka baraka mbalimbali za Kinabii kwa wana-Partners wote ikiwemo baraka ya kushika pesa na kuheshimika.
   Aidha Nabii Mkuu alifundisha umuhimu wa kuwa mwana-Partners na faida zake huku akiwasisitizia watu wote kusapoti kazi ya Mungu kwa nguvu kwa kuna baraka ya kipekee wataipata kwa kufanya hivyo na kuwakumbusha kuwa ili kazi ya Mungu iwe nzuri na ithaminiwe ni lazima igharamikiwe ambapo alitoa nukuu isemayo "Cha gharama kina thamani kama hakina gharama hakina thamani" akimaanisha kuwa kitu chochote chenye thamani lazima kiwe cha gharama hakiwezi kuwa bure ikiwemo Nguvu Ya Mungu.
   Wakati huohuo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametangaza kuwepo katika kipindi cha Maswali Na Majibu  kitakachoruka LIVE kwa njia ya Radio,  99.3  N.Y.U FM pamoja na GEORDAVIE TV siku ya jumatano ambapo kwa siku hiyo yeye ndiye atakayeuliza maswali kwa wasikilizaji na watazamaji na kisha kutoa zawadi ya pesa taslimu kwa wale watakaopatia kwa kujibu maswali hayo vizuri. 


          NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

Tuesday, January 8, 2019

JE UNAFAHAMU KUWA MHE. DR. GEORDAVIE KATIKA MWAKA 2018 PEKEE AMETUMIA ZAIDI YA SH. MILIONI 143 KATIKA KUSAIDIA JAMII???


   Amekuwa akitambulika kama Mtumishi wa Mungu mtoaji zaidi Nabii wa Equator, Nabii Mkuu wa karne ya 21, si mwingine ni Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie kutoka Arusha, Tanzania.
  Na siku ya leo tunakuletea kwa uchache baadhi ya matukio ya utoaji aliyoweza kuyafanya kwa mwaka wa 2018 yaliyopelekea Nabii Mkuu ambaye amekuwa msaada na kipenzi cha wengi kutajwa kama Mtumishi Wa Mungu mtoaji zaidi.
  Katika ku-support Watumishi Wa Mungu kutoka katika makanisa mengine tofauti na Ngurumo Ya Upako yaliyo ndani na nje ya Tanzania, Nabii Mkuu ametumia zaidi ya Sh. Milioni 30 katika kuhakikisha anatoa misaada katika huduma hizo ambapo kwa asilimia kubwa zilikuwa haziridhishi kiuchumi (hazijamudu kujitegemea kiuchumi), Nabii Mkuu aliweza kuwasaidia ili kuhakikisha watumishi wanaweza kukidhi mahitaji yao lakini pia ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kujenga makanisa yao ili yawe katika hali ya kuridhisha.
  Katika upande mwingine wa kijamii, Nabii Mkuu amekuwa na kawaida ya kupeleka misaada sehemu mbali ikiwa ni pamoja na katika vituo vya watoto yatima ambapo kwa mwaka 2018 Nabii Mkuu amepeleka katika vituo vitatu tofauti hapa Tanzania.
   Mbali na hayo pia Nabii Mkuu ametoa misaada mingine ikiwemo kuwalipia ada wanafunzi wa ngazi mbalimbali mpaka chuo kikuu waliokwama kutokana na kukosekana kwa kipato ili kuwawezesha kuendelea na masomo yao.
  Aidha katika kusaidia watu pia Nabii Mkuu ametumia zaidi ya Milioni 20 katika kusaidia watu mbalimbali wenye mahitaji, ikiwemo wenye uhitaji wa mitaji lakini pia wenye biashara ndogo ndogo katika kuhakikisha wanaweza kuwa na kipato cha kujikimu kimaisha.
  Lakini pia katika upande mwingine Nabii Mkuu amekuwa akiwa-support watu wenye vipaji kwa namna mbalimbali ambapo baadhi ya waliopata neema hiyo ni pamoja na vijana wawili walionunuliwa ngoma na mwingine spika ,kila mmoja kwa wakati wake pamoja na waimbaji wa nyimbo za injili kutoka sehemu mbalimbali.
  Hakuishia hapo katika kusaidia tu, Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa akitoa zawadi mbalimbali kwa watu ambapo kwa mwaka wa 2018 ametoa zawadi ya magari nane (8) kwa watu tofauti tofauti wa ndani na nje ya nchi kwa mwaka huo yenye thamani ya jumla milioni 88.
  Aidha katika msimu wa sikukuu mpaka sasa Nabii Mkuu ametoa zawadi kwa njia ya pesa taslimu za zaidi ya sh. Milioni 5 kwa watu mbalimbali ambao walijishindia kwa njia ya kupiga simu kwenye vipindi vilivyokuwa vikiruka kupitia 99.3 N.Y.U FM Radio pamoja na GeorDavie Tv (zoezi hilo linaendelea mpaka sasa) na wengine wakijishindia kupitia mitandao ya kijamii.
  Akizungumzia utoaji huo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amesema haya "hiyo ni njia ya Ufalme Wa Mungu kuwabariki watu wake kwakuwa nao wamekuwa wakitoa kwa Ufalme Wa Mungu hivyo sasa ni wakati wao kubarikiwa pia" mwisho wa kunukuu.
         NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

Tuesday, December 25, 2018

NABII MKUU MHE. DR. GEORDAVIE AMEWATAKA WATU KUTOKUANGALIA MAZINGIRA YANASEMA NINI BALI WAANGALIE KUSUDI LA MUNGU KATIKA MAISHA YAO.





   Jumapili ya tarehe 23.12.018 Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie aliongoza ibada ya jiji katika Chuo Kikuu Cha Manabii Ngurumo Ya Upako Arusha, ambapo ilikuwa ni ibada ya Christmas ya kudhihirisha kusudi la Mungu maishani.

   Akifundisha somo lenye kichwa kisemacho "Usiangalie mazingira bali kusudi la Mungu" Nabii Mkuu amesema kuwa kuna wakati mazingira yanaweza kueleza kitu kingine lakini pia Mungu akawa na kusudi maishani mwako ambapo alimtolea mfano Yesu Kristo na kusema kuwa kuzaliwa kwake katika hori la ng'ombe haikuwa sababu ya kusudi alilokuwa nalo kupotea.
   Aidha Nabii Mkuu amesema kuwa katika maisha kuna vitu vitatu.. Mazingira, Wakati na Kusudi na kuongeza kwamba "Mazingira hukabiliwa na wakati" ikiwa siyo wakati wa Mungu huwezi kulazimisha na pia ikiwa ni wakati wa Mungu huwezi kuuzuia.

   Mbali na hayo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeoDavie alifungua watu mbalimbali waliofika wakiwa na vifungo vya nguvu za giza, na pia kutamka maneno ya baraka kwa watu wote ili wazidi kuinuka, kubarikiwa, kung'aa na kufanikiwa.

   Pia Nabii Mkuu ametangaza kuwepo tena katika katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako siku ya jumatano ya tarehe 26.12.018 ambapo itakuwa ni ibada ya hitimisho la Siku kuu ya kukusanya (SKYK) ambapo watu wote wametakiwa kufika wakiwa wamefunga pamoja na bajeti zao za mwaka 2019.


    NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.