Rais
 na Amiri Jeshi Mkuu Dk. John Magufuli amelipongeza Jeshi la Ulinzi la 
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake
 na kwa kutimiza wajibu wake jambo ambalo limeifanya Tanzania kuwa nchi 
ya amani.
Salamu za pongezi za Rais Magufuli amezitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kuandika, “Nalipongeza
 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutimiza miaka 53 
tangu kuanzishwa kwake. Kwa kipindi chote hiki Jeshi letu limeendelea 
kutimiza wajibu wake akiwa ni pamoja na kulinda amani ya nchi yetu kwa 
uzalendo, umahiri, ushupavu, uadilifu na nidhamu ya hali ya juu na hivyo
 kujijengea heshima ndani na nje ya nchi yetu. Najivunia kuwa Amiri 
Jeshi Mkuu wa JWTZ. Mungu ibariki Tanzania, Mungu libariki Jeshi letu.”
 

 
No comments:
Post a Comment