Friday, February 5, 2016

SERIKALI YABAINISHA VIKWAZO VYA MAENDELEO YA TAIFA

Serikali Imesema tatizo la ukuajiwa uchumi usioenda na maisha halisi ya mtanzani umechangiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kasi kubwa ya
ongezeko la watu na kilimo duni.

Hayo yamesemwa leo bungeni mjini Dodoma na waziri wa fedha na mipango Dr.Philip Mpango wakati akizungumzia mkakati wa taifa wa  maendeleo  endelevu  katika mwaka wa fedha 2015-2017.

Dr. mpango amesema ili kuhakikisha uchumi unakua ni vyema mfumo wa utumiaji fedha za nje urekebishwa ili kuendana na tangazo la serikali mwaka 2007 lililokuwa linaelekeza malipo yote yalipwe kwa mfumo wa shilingi  kwani ufumo uliopo sasa umekuwa ni changamoto katika ukuaji wa uchumi hapa nchini.

Hata hivyo  mpango amesema kuwa thamani ya  shilingi imeshuku kwa kipindi cha mwaka 2014-2015 kutokana na kuimarika kwa dola na viwango  fedha tofauti na shilingi hivyo ni vyema  ukawepo uthibiti wa fedha za kigeni na uongezaji thamani ya mauzo yanayofanywa nje ya nchi.  

Katika hatua nyinge serikali leo imetoa ufafafauzi kuhusu hatua zilizochukuliwa kufutia kitendo cha uzalilishwaji mwanafunzi mtanzania anayesoma nchini india ambapo waziri wa mambo ya Nje Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dk. Augustino Mahig amesema kuwa ubalozi wa Tanzania  Nchini India umekutana na uongozi wa wizara ya  mambo ya nje inchini humo na kuhakikisha kuwa wote walitekelaza vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kisheria na serikali ya nchi hiyo imeahidi kutoa ulinzi kwa watanzania wanafunzi wanaosomea kozi mbalimbali nchini humo. 

No comments:

Post a Comment