Friday, April 27, 2018

West Ham United kuwakabili Manchester city-Epl

West Ham United

Ligi kuu ya soka ya England inaendelea tena wikendi hii kwa michezo kadhaa,kesho jumamosi michezo saba inatarajiwa kuchezwa ambapo Liverpool wanacheza na Stoke city,Burnley dhidi ya Brighton,Crystal Palace ni mwenyeji wa Leceister City.

Huddersfield dhidi ya Everton,Newcastlle United wanachuana na West Bromwich Albion,Southampton na FC Bournemouth na Swansea city ni wenyeji wa Chelsea.
Idhaa ya Kiswahili ya bbc itakutangazia mchezo kati ya Crystal Palace Leicester kupitia matangazo ya Uimwengu wa soka.
Jumapili West Ham united watawakaribisha Manchester City na Manchester United ni wenyeji wa Arsenal ,
CHANZO BBC SWAHILI.
BY RICHARD SHIYO/RICH VOICE