Wednesday, April 4, 2018

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 04.04.2018

Chelsea wanatarajia kumteua kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri
Chelsea wanatarajia kumteua kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri, kuwa meneja wa mpya mwishoni mwa msimu lakini kama itashindikana mazungumzo na meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique. (Star)

Klabu ya Real Sociedad ya nchini Hispania, inayosuasua kwenye ligi ya nchini humo inamtaka meneja wa Newcastle Rafael Benitez kuwa meneja wake mpya. (Mirror)
Eden Hazard winga wa Chelsea
Real Madrid inaangalia uwezekano wa kufanya kufanya uhamisho wa kiasi cha pauni milioni 100 wa kumsajili Eden Hazard kutoka Chelsea katika dirisha la majira ya joto.(Evening Standard)
Chelsea the Blues wanataka kumsajili kipa kinda wa Kituruki Berke Ozer mwenye umri wa miaka 17 kutoka timu ya daraja la pili ya Altinordu. (Sun)
Manchester City wako katika mikakati ya kumsajili kiungo chipukizi wa Barcelona Robert Navarro, mwenye miaka 15, Barcelona bado hawajampa kiungo huyo mkataba.(Sport)
Wagonga nyundo wa London klabu ya West Ham United wataendelea kusalia na meneja wao David Moyes, meneja huyo wa zamani wa vilabu vya Everton na Manchester United, amewaondoka West Ham katika mstari wa timu zinazoshuka daraja.(Mirror)
Mikel Merino anataka kuondoka New Castle
Kiungo wa Newcastle,Mikel Merino, mwenye umri wa miaka 21, ameiambia klabu yake kuwa nataka kujiunga na Athletic Bilbao, ya nchini Hispania (TeamTalk)
Vilabu vya Bournemouth, Leicester na Aston Villa wanamfutilia kwa ukaribu mshambuliaji wa Southampton, Charlie Austin, kuweza kumsajili kama timu yake itashuka daraja mwishoni mwa msimu huu(Mirror)
Winga wa Stoke City raia wa Misri Ramadan Sobhi anamatumaini ya kufanya vyema katika michuano ya kombe la dunia ili kuongeza nafasi ya kuondoka Stoke katika dirisha lijalo la usajili (Stoke Sentinel)
Mwenyekiti wa timu ya Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha atasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa tiketi 60, za ugenini kwa wafuasi wa klabu yake itakapokuwa ikienda kucheza na Newcastle United. (LCFC.com)
Steven Pienaar apewa ubalozi wa klabu ya Everton



Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Steven Pienaar amekuwa balozi wa kwanza wa klabu hiyo kimataifa. (Liverpool Echo)

CHANZO-BBC SWAHILI


No comments:

Post a Comment