Thursday, April 26, 2018

REAL MADRID YAITUNGUA BAYERN MUNICH, RONALDO AKIANDIKA REKODI MPYA


Mchezo wa nusu fainali ya pili UEFA Champions Leag, mkondo wa kwabza kati ya Bayern Munichen dhidi ya Real Madrid, ulipigwa usiku wa kuamkia leo huko Allianzi Arena huku Madrid wakiibuka wababe katika mchezo huo.

Madrid walishinda mabao 2-1, huku mabao ya Madrid yakipachikwa na Marcelo pamoja nae Marcos Asensio ilhali bao pekee la Bayern likiwekwa kimiani na Joshua Kimichi mapema tuu dakika ya 28 ya mchezo huo.
Katika hatua nyingine nyota wa Madrid Christiano Ronaldo, amefanikiwa kuweka rekodi mpya katika michuano hiyo kwa kuwa mchezaji aliyeshinda michezo mingi ya UEFA akishinda michezo 96, huku akimzidi Iker Casilas aliyeshinda michezo 95, Xavi 91 wakati Raul Gonzales na Andres Iniesta wakishinda michezo 79 kila mmoja.
Ronaldo pia ameshindwa kuendeleza rekodi yake ya kufunga katika kila mchezo wa michuano hiyo kwa msimu huu wa 2017-18, wakati Joshua Kimichi ikiwa ndiyo mchezo wa kwanza kuanza kufunga na timu yake kupoteza baadae.

by richard shiyo/rich voice

No comments:

Post a Comment