Monday, April 9, 2018

Chelsea 'wanaelekea kucheza Europa League' baada ya sare na West Ham

Mlinzi wa timu ya Chelsea Cesar Azpilicuet 



Kushinda kombe la FA hakutatosha "kunusuru" msimu wa klabu ya Chelsea, kwa mujibu wa beki wa klabu hiyo Cesar Azpilicueta.

Amesema hayo huku ikionekana wazi kwamba itakuwa mwujiza kwao kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Hii ni baada yao kutoka sare ya 1-1 West Ham na hivyo kudidimiza zaidi matumaini ya klabu hiyo kumaliza katika nafasi nne za kwanza Ligi Kuu ya England msimu huu.
Kutoka sare kwa timu hiyo Jumapili kumeiacha Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Premia wakiwa pointi 10 nyuma ya Liverpool na Tottenham katika nafasi ya tatu na ya nne.
Bao la kusawazisha la Javier Hernandez la kipindi cha nusu ya pili ya mchezo liliinua matarajio ya West Ham ya kuendelea kubakia katika michuano ya Ligi ya Premia dakika ya 73 lakini likawaumbua Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge.
Eden Hazard
Inamaanisha kuwa huenda wasifuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
"Tuko nyuma sana," alisema Azpilicueta, aliyekuwa amefungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 36.
''Ni kauli kubwa na kwa kiasi fulani aliyoitoa Azpilicueta... nimeipenda, anajivunia klabu yake na anafahamu fika malengo ya Chealsea, na kutoa kauli hiyo inamaanisha kuwa amevunjika moyo kwa mahala walipo sasa,'' alisema mchanganuzi wa mechi za siku Jermaine Jenas katika mazungumzo na BBC.
Image caption Mustakabali wa kocha wa sasa wa Chelsea Antonio Conte haueleweki baada ya timu yake kuteteleka katika msimu huu wa Ligi ya Premia
Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho alifutwa kazi wakati wa msimu wa mwaka 2015-16, wakati timu hiyo ilipomaliza ikiwa katika nafasi ya 10 katika Ligi ya Premia.
Na maswali pia yanaibuka juu ya mustakabali wa kocha wa sasa Antonio Conte, ambaye ameongoza timu hiyo baada ya kushinda taji mwaka jana.
Huku zikiwa zimesalia mechi sita, kihesabu Chelsea inaweza kufika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, ingawa itabidi timu za Liverpool (ambao wamesalia na mechi tano) na Tottenham (ambao bado wana mechi sita za kucheza) ziporomoke.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bao la kusawazisha la Javier Hernandez la kipindi cha nusu ya pili ya mchezo liliinua matarajio ya West Ham ya kuendelea kubakia katika michuano ya Ligi ya Primia
Lakini hata kama wataweza kusonga mbele na kushinda Kombe la FA halitakuwa liwazo kamili machoni mwa Azpilicueta, 28.
"Kombe la FA ni kombe kubwa lenye historia kubwa lakini halitoshi kwetu," mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya taifa ya Uhispania aliambia BBC.
" Tutajaribu kulishinda lakini kombe halitunusuru kwenye msimu," aliongeza.
Azpilicueta, ambaye goli lake la kipindi cha kwanza cha mchezo wa Jumapili lilifutwa na goli za kusawazisha la Javier Hernandez katika kipindi cha pili aliongeza: "Kupata sare nyumbani katika uwanja mwingine wa London ni suala linaloleta mfadhaiko kwetu sote na kwa mashabiki wetu. Hatujafurahi.''
"Cha maana ni matokeo ya mwisho ya mechi, nimesikitika sana leo. Tulifaa kushinda mechi hii."
"Tulidhibiti mechi , tulikuwa na fursa za kutosha kushinda lakini tulihangaika hadi mwisho na labda wangeweza kushinda.
Imekuwa vigumu sana tena sana kwa kila mchezo unaochezwa."

No comments:

Post a Comment