Monday, April 9, 2018

Mzozo Syria: Israel yashutumiwa kutekeleza shambulio dhidi ya uwanja wa ndege

Wanajeshi wanaounga mkono serikali ya Syria, yanakaendelea na vita katika juhudi za kuwafurusha waasi kutoka mji wa Douma
Serikali ya Syria na mshirika wake Urusi zimeishutumu Israel kwa shambulio baya katika uwanja wa ndege za kijeshi za Syria.



Shambulio hilo la Jumatatu liliulenga uwanja wa ndege za kivita wa Tiyas unaofahamika kwa umaarufu kama T4, karibu na mji wa Homs. Waangalizi wanasema watu 14 wameuawa.
Israel, ambayo awali iliwahi kuyelnga maeneo nchini Syria bado haijatoa tamko lolote. Awali Syria iliilaumu Marekani kwa shambulio hilo.
Tukio hilo limetekelezwa huku jamii ya kimataifa ikiendelea kulaani shambulio la kemikali ambalo lilitekelezwa katika mji wa Douma ambao unashikiliwa na waasi. Marekani na Ufaransa zimetishia kulipiza kisasi.
Rais wa Marekani Donald Trump alimweleza Rais wa Syria kama "nduli" Jumapili na kuonya kwamba yeye pamoja na washirika wake Iran na Urusi "watalipia sana".
Bw Trump na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron walitoa taarifa siku hiyo na kuapa "kuchukua hatua kali na ya pamoja" kuhusiana na shambulio hilo.
Lakini maafisa wa Marekani wamekanusha uwezekano kwamba Marekani ndiyo iliyotekeleza shambulio hilo.
"Kwa sasa, Wizara ya Ulinzi haitekelezi mashambulio yoyote ya angani Syria," Pentagon imesema kupitia taarifa.
A child is treated after a suspected chemical attack in Syria's Eastern Ghouta district, 8 April 2018
"Hata hivyo, tunaendelea kufuatilia kwa karibu na kuunga mkono juhudi za kidiplomasia zinazoendelea za kuwawajibisha wote wanaotumia silaha za kemikali, nchini Syria na kwingineko, kuhakikisha wanaadhibiwa."

Aprili mwaka 2017, Marekani ilirusha makombora 59 aina ya Tomahawk katika uwanja wa ndege za kivita wa Shayrat nchini Syria baada ya shambulio la kemikali kutekelezwa katika mji wa Khan Sheikhoun uliokuwa unashikiliwa na waasi.
Israel ilitekeleza pia mashambulio mengine makubwa dhidi ya Syria mapema mwezi huu.
Nini kilitokea Douma?
Duru za kimatibabu zinasema watu wengi walifariki katika shambulio hilo la Douma, mlinalopatikana Ghouta Mashariki.
Video moja ambayo imekuwa ikisambaa ambayo ilirekodiwa na wahudumu wa kujitolea wafahamikao kama White Helmets linawaonesha maiti za wanaume, wanawake na watoto kadha ndani ya jumba moja, maiti nyingi zikiwa na povu mdomoni.
Hata hivyo, imekuwa vigumu kubaini hasa nini kilitokea na idadi kamili ya waliofariki.
Children are given medical checks in what is said to be the rebel-held Syrian town of Douma, 7 April 
Syria na Urusi wote wamekana taarifa kwamba shambulio la kemikali lilitekelezwa, na wameafikiana mkataba wa kuwahamisha waasi ambao walikuwa wakishikilia mji wa Douma.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana Jumatatu kujadili mzozo huo.

No comments:

Post a Comment