Wednesday, July 8, 2026

MANCHESTER UNITED YAANGUKIA KWA ANDREY SANTOS BAADA YA KUMKOSA MATEUS FERNANDES


Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na Chelsea juu ya kumsajili kiungo, Andrey Santos kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 56 pamoja na nyongeza ya Euro milioni 2.4 huku Chelsea akipachika kifungu cha asilimia 10 za mauzo ya siku za usoni.

Santos 22, raia wa Brazil tayari amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na mashetani hao Wekundu na tayari amepata ruhusa ya kufanya vipimo vya afya kabla ya kukamilika uhamisho huo.

Mashetani hao Wekundu ambao pia wanatarajiwa kumtangaza, Mbrazil mwingine, Ederson kama mchezaji mpya walilazimika kutafuta kiungo mwingine kwa ajili ya kurithi mikoba ya Casemiro ikiwa ni baada ya kuangukia pua katika jitihada zao za kuinasa saini ya Mateus Fernandes aliyetimkia Tottenham Hotspur.

No comments:

Post a Comment