Marekani imefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya Iran mapema leo, hatua iliyojibiwa na Iran kwa kuyalenga mataifa ya Bahrain, Kuwait na Qatar. Hali hii inaongeza mvutano na kuhatarisha tena makubaliano ya muda yaliyolenga kutafuta njia ya kumaliza vita.
Jeshi la Marekani lilishambulia
maeneo mbalimbali ya kijeshi na miundombinu ya bandari mapema Jumatano,
kufuatia mashambulizi ya Iran dhidi ya meli kadhaa za biashara katika pwani ya
Oman, hali iliyosababisha Iran kujibu kwa mashambulizi mengine.
Mashambulizi
ya Marekani yalifanywa saa chache baada ya Rais wa Marekani
Donald Trump kusema makubaliano hayo yamefika mwisho kufuatia mashambulizi hayo
ya Iran.
Hata hivyo, mashambulizi ya
Alhamisi yalionekana kuwa makubwa zaidi kuliko ya awali huku Jeshi la Kuwait
likisema limezuia na kudungua droni pamoja na makombora yaliyoelekezwa nchini
humo.
Vyombo vya habari vya serikali ya
Iran viliripoti milipuko katika maeneo kadhaa, yakiwemo Bushehr, ambako kuna
kituo cha nishati ya nyuklia cha Iran, pamoja na miji ya bandari ya kusini ya
Chabahar, Konarak, Bandar Abbas na Sirik.
Chanzo: DW

No comments:
Post a Comment