Kamishna wa Polisi
Zanzibar CP Kombo Khamis Kombo amewataka Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi
kuendelea kuwa nguzo imara katika kuelimisha na kuhabarisha umma kuhusu masuala
ya ulinzi na usalama.
Hayo amezungumza Septemba
28, wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa Maafisa Habari wa Jeshi la
Polisi wa Makao Makuu ya Polisi, Mikoa, Vikosi na Vyuo vya Polisi katika Shule
ya Polisi Tanzania (TPS) Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.
CP Kombo, amehimiza
nafasi ya Maafisa Habari katika kujenga na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya
Jeshi la Polisi na jamii, huku akiwataka kutumia taaluma yao kuhakikisha umma
unapata elimu na taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu Jeshi la Polisi ikiwemo
kazi na mafanikio.
Naye, Kamishna wa Polisi Jamii CP Alex Mkama, amesema kuwa kitengo cha habari na uhusiano ndani ya Jeshi la Polisi kimekuwa na mchango mkubwa katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwani jamii imekuwa ikihabarishwa na kujengewa uwezo wa kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu kabla haujatokea katika maeneo yao.



No comments:
Post a Comment