Wednesday, October 7, 2026

MHE. PROF. GEORDAVIE: AMANI SI TU KUTOKUWEPO KWA MIGOGORO, AMANI NI UWEPO WA HAKI, UTU, FURSA, KUHESHIMIANA NA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA

Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa United Nations Peace Ambassadors Foundation (UN-PAF) amesema kuwa Ujenzi wa amani lazima uanze na mazungumzo ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa majukwaa imara zaidi ambapo serikali,wanadiplomasia, mashirika ya kiraia,viongozi wa dini, vijana na jamii wanaweza kuwasiliana kwa uwazi, heshima na kwa njia yenye kujenga.

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika mkutano UN-PAF Doha International Peace & Diplomatic Forum 2026, uliofanyika jijini Doha, Qatar ambapo alikuwa akizungumzia kuhusu umuhimu wa kuimarisha ujenzi wa amani katika ukanda wa Ghuba.

Katika hotuba yake Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amesema Ghuba ni eneo lenye umuhimu wa kimkakati kwa dunia, likiunganisha mataifa, tamaduni, uchumi na ustaarabu mbalimbali huku akiongeza kuwa kuendelea kwa utulivu wake si jukumu la kikanda pekee, bali ni maslahi ya dunia nzima. Pia, amesema kuwa kunapaswa kuimarishwa kwa diplomasia ya kuzuia migogorona kuongeza kuwa ni bora zaidi kutatua tofauti kupitia mazungumzo na uelewano kabla hazijageuka kuwa migogoro. 

Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie amesema Nchi za Ghuba zimeonesha kwamba diplomasia inaweza kuleta matokeo ya kushangaza. Tunapaswa kujenga juu ya utamaduni huu kwa kuendeleza mazungumzo ya kikanda, ushirikiano wa kibinadamu, uendelevu wa mazingira na utatuzi wa migogoro kwa njia ya aman. Amesema Amani si tu kutokuwepo kwa migogoro, Amani ni uwepo wa haki, utu, fursa, kuheshimiana na uwajibikaji wa pamoja.

“Kwa hiyo, tujenge madaraja badala ya kuta, tuimarishe mazungumzo badala ya mgawanyiko, na tuchague ushirikiano badala ya makabiliano”.

“Tukifanya kazi Pamoja kwa ujasiri, hekima na kujitolea kwa dhati tunaweza kujenga ukanda wa Ghuba ambako amani inadumishwa, maendeleo yanawafikia wote, na vizazi vijavyo vinarithi utulivu na ustawi”.

“Tufanye amani isiwe tu matarajio yetu, bali iwe jukumu letu la Pamoja”.

“Asanteni, na amani, ustawi na ushirikiano viendelee kuuongoza ukanda wa Ghuba na dunia”. Naibu Mwenyekiti (UN-PAF) Mhe. Prof. GeorDavie 

No comments:

Post a Comment