Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia taarifa za utabiri wa hali ya hewa na
tahadhari zinazotolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili kulinda maisha na mali za wananchi.
Jaji Mshibe aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau kutoka sekta mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa PSSSF, Dodoma, tarehe 19 Oktoba 2026 kwa ajili ya kujadili athari na ushauri kwa kila sekta. Hii ni moja ya hatua za maandalizi ya kutoa Utabiri wa Mvua za Msimu Novemba, 2026 hadi Aprili 2027.
Akizungumzia hatua za
kukabiliana na maafa, alisisitiza kuwa uokozi wenye tija ni ule unaofanyika
kabla athari hazijatokea, hapo unakuwa umeiokoa jamii, na mwisho alitoa wito
kwa wadau kutumia tahadhari za hali ya hewa kupanga hatua za kinga na kujiandaa
mapema, badala ya kusubiri maafa yatokee.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko
ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a, Alisisitiza,
umuhimu kwa wananchi kuendelea kufuatilia na kuzingatia utabiri na tahadhari za
matukio ya hali mbaya ya hewa.


No comments:
Post a Comment